2022
Ibrahimu na Sara
Februari 2022


“Ibrahimu na Sara,” Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki, Februari 2022

“Ibrahimu na Sara”

Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki, Februari 2022

Ibrahimu na Sara

Picha
Ibrahimu na Sara ndani ya hema

Vielelezo na Apryl Stott

Ibrahimu alikuwa nabii. Mungu alifanya agano na Ibrahimu pamoja na mkewe, Sara.

Picha
Ibrahimu na Sara wakiwa na huzuni

Mungu aliahidi kuwabariki. Aliwaambia watakuwa na watoto. Ibrahimu na Sara waliahidi kumfuata Mungu.

Picha
Ibrahimu na Sara

Ibrahimu na Sara walitunza ahadi yao. Lakini hawakuwa na watoto kwa muda mrefu. Walizidi kuwa wazee sana.

Picha
Ibrahimu na Sara wakiwa na mtoto Isaka

Hatimaye, Ibrahimu alipokuwa na umri wa miaka 100 na Sara akiwa na miaka 90, walipata mtoto wa kiume. Walimwita Isaka. Walijua Mungu alikuwa amewabariki.

Picha
mtoto kupanda mbegu

Ninaweza kumwamini Mungu. Wakati mwingine baraka haziji papo hapo. Lakini Mungu daima hutimiza ahadi zake.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Ninaweza kumwamini Mungu

Picha
mtoto akisali

Bonyeza kwenye picha ili kupakua.

Kielelezo na Apryl Stott

Je, ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni amekusaidia ulipokuwa unaogopa au mwenye huzuni?

Chapisha