“Ruthu na Naomi,” Jumbe za kila mwezi za gazeti la Rafiki, Juni 2022
“Ruthu na Naomi”
Jumbe za kila mwezi za gazeti la Rafiki Juni 2022
Ruthu na Naomi
Naomi na familia yake walikwenda kwenye nchi mpya kwa sababu ya njaa. Walikutana na binti aliyeitwa Ruthu. Ruthu aliolewa na mwana wa Naomi.
Kisha mume wa Ruthu alifariki. Ruthu alikuwa na huzuni sana.
Naomi naye alihuzunika sana. Hakuwa amebaki na familia ya kumtunza. Naomi aliamua kurejea katika nchi aliyotoka.
Naomi akamwambia Ruthu arejee kwa familia yake. Lakini Ruthu alimpenda Naomi. Aliahidi kuambatana na Naomi na kumtunza.
Ruthu na Naomi walikuwa maskini. Kwa hiyo Ruthu alifanya kazi kwa bidii ili kutafuta chakula.
Siku moja mwanaume anayeitwa Boazi alimwona Ruthu akikusanya mabaki ya nafaka katika moja ya shamba lake.
Boazi alikuwa mwema. Aliwaambia wafanyakazi wake wamuachie Ruthu chakula cha ziada.
Baadaye Ruthu na Boazi walioana. Walipata mtoto wa kiume. Naomi alisaidia kwenye kumtunza.
Ninaweza kusaidia kuwatunza wengine. Ninaweza kuwa mkarimu kwa wenye uhitaji.
© 2022 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, June 2022. Swahili. 18315 743