“Majina Mengi ya Yesu” Ujumbe wa Kila Mwezi wa Gazeti la Rafiki, Disemba 2022
“Majina Mengi ya Yesu”
Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki, Disemba 2022
Majina Mengi ya Yesu
Manabii wengi walifundisha kuhusu Yesu Kristo. Walisema Angezaliwa ili kutuonyesha jinsi ya kuishi. Walitumia majina mengi kufundisha kuhusu Yeye.
Wakati mwingine katika maandiko Yesu anaitwa Imanueli. Jina hilo humaanisha “Mungu pamoja nasi.”
Yesu pia anaitwa Masihi. Masihi humaanisha “Mpakwa mafuta.” Yesu alikufa kwa ajili yetu ili kwamba tuweze kuishi na Mungu tena.
Yesu ni Mwokozi wetu. Hutuokoa kutoka dhambi na kifo.
Jina lingine la Yesu ni Mfalme wa Amani. Wakati tunapopatwa na woga au kukata tamaa, Anaweza kutusaidia kuhisi amani kupitia Roho Mtakatifu.
Nampenda Yesu Kristo. Ninaweza kujifunza kuhusu maisha na upendo Wake katika maandiko.
© 2022 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, December 2022. Swahili. 18318 743