“Yesu Anamponya Mwanamke,” Jumbe za Kila mwezi za gazeti la Rafiki, February 2023
Yesu Anamponya Mwanamke”
Jumbe za kila mwezi za gazeti la Rafiki, Februari 2023
Yesu Anamponya Mwanamke
Siku moja Yesu alikuwa akitembea kwenye mtaa wenye shughuli nyingi. Katika umati ule alikuwepo mwanamke aliyeugua kwa muda wa miaka 12.
Mwanamke yule alikuwa na imani kwamba Yesu angeweza kumponya. Hivyo alisogea na kugusa vazi Lake. Mara moja aliponywa!
“Nani aliyegusa nguo yangu?” Yesu aliuliza. Mwanamke alikuwa na hofu. Alipiga magoti mbele ya Yesu na kumwambia kile kilichotokea.
Yesu alikuwa mwenye upendo. Alisema, “Uwe na amani.” Alimwambia kwamba ameponywa kwasababu ya imani yake.
Ninaweza kuwa na imani katika Yesu Kristo. Upendo wake unaweza kunisaidia na kuniletea amani.
© 2023 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, February 2023. Language. 18910, 743