“Toba Ni Ya Shangwe!” Rafiki, Septemba 2024, 2–3.
Kutoka Urais wa Kwanza
Toba Ni Ya Shangwe!
Imetoholewa kutoka “Kutakaswa kwa Toba, Liahona, Mei 2019, 91–94.
Toba ni ya shangwe. Ni sehemu muhimu ya mpango wa Mungu. Sisi sote tunahitaji kutubu.
Ili kutubu, lazima sisi tuanze na imani katika Yesu Kristo. Lazima tuziache dhambi zetu na kiziungama Hii inamaanisha kutambua tulifanya makosa, kusema pole kwa wale tuliowaumiza na kuchagua kufanya chaguzi bora. Tunapaswa pia kupokea sakramenti kila siku ya Sabato.
Tunapotubu, tutasafishwa. Bwana anaahidi kwamba “hatazikumbuka tena [dhambi zetu]” (Mafundisho na Maagano 58:42). Ni ahadi iliyoje! Ni muujiza ulioje! Ni baraka iliyoje!
Mwokozi wetu mpendwa anafungua mikono Yake kupokea wote wanaotubu na kumfuata Yeye.
Msafi Tena
Fanya shughuli hii kukusaidia kujifunza kuhusu toba!
-
Jaza chombo safi kwa maji. Kisha tumbukiza kiasi cha mawe na uchafu ndani ya maji. Hii inawakilisha chaguzi zisizo sahihi tunazozifanya.
-
Ili kuwa msafi tena, tunahitaji kuacha kile kilicho makosa. Ili kuwakilisha hili, toa mawe kutoka kwenye chombo. Ni kwa jinsi gani maji yanavyoonekana sasa? Je, bado ni machafu?
-
Ili kutubu kikamilifu, tunamhitaji Yesu Kristo. Tunahitaji kuwa na imani katika Yeye na Upatanisho Wake. Shikilia chombo cha maji chini ya bomba Acha maji safi yapite ndani ya chombo mpaka maji yote machafu yote yamwagike nje ya chombo! Hii inawakilisha nguvu ya Yesu Kristo inavyotusaidia kuwa wasafi.