Rafiki
Maafa ya Dati
Septemba 2024


“Maafa ya Dati,” Rafiki, September 2024, 4–36.

Maafa ya Datsi

Je Daniel alikuwa jasiri vya kutosha kusema ukweli?

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Daniel alitoa mfuniko wa zamani wa sanduku la mwanasesere la Babu yake na kuchungulia ndani Binamu zake walikusanyika kuangalia. Walipenda kucheza pamoja nyumbani kwa Babu!

Ndani yake mlikuwa na wanasesere wengi ambao mama na shangazi wa Daniel waliwachezea walipokuwa watoto.

“Hizo ni nini?” Binamu wa Daniel, Noah alionesha kwenye dati sita zinazong’aa za mtindo wa kizamani. Zilikuwa na miisho yenye kuchongoka na bendera zenye rangi—baadhi nyekundu na baadhi njano.

Daniel alinyanyua mojawapo. “Mama yangu aliniambia kuhusu hizi,” alisema. “Unatengeneza duara kwenye nyasi. Kisha mnachukuwa zamu kuzirusha hewani na kujaribu kuzifanya ziangukie ndani ya duara.”

“Safi sana!” alisema Noah. Alikuwa tayari akikimbia kuelekea kwenye uwanja kuutayarisha mchezo.

Mara Daniel na binamu zake walikuwa wakirusha dati za chuma angani kuzunguka uwanja mzima wa Babu. Daniel alipenda wakati dati zilipotua kwa kishindo na kukwama katika nyasi.

“Nakuhakikishia naweza kutupa zangu juu zaidi kuliko zako,” alisema binamu wa Daniel aitwaye Lily.

Watoto walicheka na walirusha dati juu na juu.

Kisha Daniel akawa na wazo. “Nakuhakikishia naweza kurusha zangu kwenye njia nzima mpaka itumbukie ndani ya duara!” alisema. Alikimbilia upande mwingine wa njia na alirusha dati kwa nguvu sana.

Dati iliruka juu hewani, lakini haikutua ndani ya nyasi. Badala yake ilianguka kwenye gari jipya kabisa la shangazi Robilyn kwa sauti kubwa ya KISHINDO.

Mvulana akirusha dati kwenye gari

“Oh hapana!” Noah alipiga kelele.

Daniel alichukua dati ile. Kulikuwa na mbonyeo mkubwa mno kwenye gari pale ilipoangukia.

Watoto walitazamana kwa kuogopa sana. Kisha, bila kusema chochote, waliziacha dati kwenye uwanja na wakakimbilia ndani.

Baadaye mchana ule, kila mmoja aliingia kwenye magari yao kwenda nyumbani. Shangazi wa Daniel aligundua mbonyeo kwenye gari lake. “Kilitokea nini?” aliuliza.

Tumbo la Daniel likahisi kuwa zito. Lakini hakusema chochote. Aliingia tu kwenye gari na akapunga kwaheri kwa binamu zake.

Wakiwa njiani kurejea nyumbani, Daniel alikaa kimya kwenye kiti cha nyuma. Alijaribu kusoma kitabu chake. Lakini hakuweza kufokasi. Alijihisi vibaya ndani kuhusu kile kilichotokea. Alijua kuwa mwaminifu kulikuwa kitu sahihi cha kufanya. Lakini kusema ukweli kutakuwa ni kitu cha kutisha! Wazazi wake watakuwa wakali mno juu yake. Na ndivyo itakavyokuwa kwa shangazi yake.

Kisha Daniel alikumbuka kuhusu shujaa wake mpendwa wa maandiko. Daniel katika Agano la Kale alitupwa ndani ya tundu la simba kwa ajili ya kuchagua kilicho sahihi. Alikuwa jasiri. Inawezekana Daniel angeweza kuwa shujaa pia.

“Mama?” Daniel alisema. “Nilitupa dati ya uwanja na ilipiga gari la Shangazi Robilyn na kutengeneza mbonyeo. Ilikuwa ni kosa langu,”

Mama alimtazama katika kioo cha kuangalia nyuma. Hakuwa na hasira kali kama Daniel alivyofikiri angekuwa. “Asante kwa kuniambia ukweli,” alisema.

Mama na mvulana ndani ya gari

Daniel alivuta pumzi mzito. “Naweza kumwita Shangazi Robilyn tutakapofika nyumbani?” Daniel aliuliza. “Ninataka kusema samahani. Na nitafanya kazi kwa nguvu kupata fedha ya kulipia na kutengeneza gari lake.”

Mama alitabasamu. “Hilo ni wazo zuri sana.”

Hisia nzito tumboni mwake ilikuwa haipo tena, na Daniel alihisi amani. Amekuwa jasiri vya kutosha kueleza ukweli. Kwa sababu ya Yesu Kristo, aliweza kutubu na kufanya mambo kuwa sawa.

alt text

Vielelezo na Josh Talbot