“Siku Isiyo na Furaha kwa Patrik,” Rafiki, Septemba. 2024, 10–11.
Siku Isiyo na Furaha kwa Patrik ya Patrik
Kaka wakubwa wa Patrik walikuwa daima wenye shughuli nyingi hadi kutomjali.
Hadithi hii ilitokea huko Marekani.
Patrik aliangalia juu darini alipokuwa akijibwaga kwenye kitanda chake. Alikuwa amechoshwa. Alikuwa tayari amesoma vitabu vyake vya wanyama, aliruka kwenye turubai na kuendesha baisikeli yake kuzunguka ujirani. Nini angeweza kufanya sasa?
Patrik aliamka na alitembea kwenda kwenye chumba cha kaka yake mkubwa Daniel. “Utacheza na mimi?” Patrik aliuliza.
“Samahani, siwezi. Ninahitaji kujifunza,” Daniel alisema. Daniel hata hakubandua macho kutoka kwenye kitabu alichokuwa anakisoma.
Patrik alihisi moyo wake ukizama. Danieli alikuwa daima akijifunza. Je, asingeweza kupumzika?
Oh vyema. Daniel alikuwa na shughuli nyingi, lakini Patrik angeweza kumwomba kaka yake mwingine, Simon. “Sina furaha. Unaweza kucheza na mimi?” Patrik aliuliza.
Hapana, sio leo. Ninatoka na marafiki zangu.” Simoni alivaa jaketi lake na akatoka kupitia mlango wa mbele.
Patrik alikasirika sana! Moyo wake ulidunda kwa kasi. Kaka zake wakubwa walikuwa daima wenye shughuli nyingi kiasi cha kutomjali. Alikimbilia kwenye chumba chake cha kulala na kufunga mlango kwa nguvu.
“Sio haki! Patrik alifikiria.
Aligonga chini kwa mguu wake na kujitupatupa kwenye kitanda chake. Alihisi kifua chake kikibana. Alikuwa mpweke sana! Lakini alihisi hasira nyingi akifikiria juu ya kitu cha kufanya.
Kisha alikumbuka kitu fulani alichojifunza shuleni. Mwalimu wake aliwafundisha kwamba kuvuta hewa nyingi kungewasaidia kuhisi utulivu.
“Ni vigumu kutengeneza chochote wakati una hasira,”alikwisha sema. Pengine kama angetulia, Patrik angeweza kufikiri njia ya ufumbuzi wa tatizo lake la kutokuwa na furaha.
Kwa hiyo Patrik alivuta pumzi kubwa, pumzi ya kina. Kisha alichukua nyingine. Baada ya dakika chache, kifua chake hakikuhisi kubana tena. Lakini bado hakujua nini cha kufanya.
Alikaa na aliangalia picha ya Yesu Kristo kwenye ukuta wake. Nini Angetaka Patrik afanye?
Patrik alipiga magoti. “Baba wa Mbinguni, tafadhali msaidie Daniel anapojifunza,” alisema. “Msaidie Simion kupata burudani pamoja na rafiki zake. Na tafadhali nisaidie kutokuwa mwenye uweke sana.”
Wakati alipomaliza sala yake, Patrik hakuwa na wazo. Alikimbia chini kwenye chumba cha Daniel.
“Daniel, wakati utakapomaliza, tunaweza kucheza pamoja?”
Daniel akiangalia juu kutoka kwenye kitabu chake kwenye saa ya ukutani. Ninaweza kupumzika takribani dakika 30. Kisha tungeweza kwenda nje. “Je, unataka kufanya hivyo?”
“Ndiyo!” Patrik alitabasamu na alikimbia kurudi kwenye chumba chake. Alipata kitabu cha wanyama kuhusu chui alichopenda kukitazama. Baada ya kukisoma kwa muda, alicheza na tofali. Mara muda ulikuwa umepita, na yeye na Daniel walielekea kwenye miti karibu na nyumba yao.
“Je, unataka kucheza wapiganaji katika anga au wagunduzi katika msituni?” Daniel aliuliza.
“Mimi sijali. Nina furaha kwamba tunaweza kutumia muda pamoja. Ni vyema zaidi kuliko kuwa mpweke,” Patrik alisema.
Daniel alikenua meno. “Vyema, kucheza pamoja nawe ni burudani zaidi kuliko kusoma kwa ajili ya mtihani.”
Patrik alihisi furaha wakati yeye na Daniel walipotambaa kwenye nyasi. Kutulia kumemsaidia kufikiri zaidi kwa uwazi ili kupata ufumbuzi wa tatizo lake. Na Baba wa Mbinguni amemsaidia kuwa zaidi kama Yesu Kristo. Iliishia kuwa siku nzuri baada ya yote.