Rafiki
Kama Nikisiliza kwa Moyo Wangu
Septemba 2024


“Kama Nikisiliza kwa Moyo Wangu,”Rafiki, Septemba 2024, 13.

Ninaweza Kuupiga

Kama Nikisiliza kwa Moyo Wangu

Kwa kutafakari [robo noti] = 88–104

PDF

1. Kama ningekuwa mtoto mdogo wakati Yesu alipoishi duniani.

Ningependa kutembea pamoja Naye na kusikiliza maneno Yake,

Lakini ninapopekua maandiko ninaweza kusikia maneno Yake ya amani.

Na kama ninasikiliza kwa moyo wangu ninasikia sauti ya Mwokozi.

2. Namsikia nabii aliye hai akisema mambo ambayo Kristo angeyasema.

Kama angekuwa hapa duniani kusema na mimi leo.

Nabii anafundisha jinsi ya kuishi kwa uadilifu na amani.

Na kama ninasikiliza kwa moyo wangu ninasikia sauti ya Mwokozi.

3. Ninamhisi Roho Mtakatifu anapofundisha ukweli na usahihi.

Ananifariji katika nyakati za mahitaji, Anamshuhudia Kristo.

Anasema na mimi katika njia za ukimya ambazo zinajaza nafsi yangu na amani.

Na kama ninasikiliza kwa moyo wangu ninasikia sauti ya Mwokozi.