Rafiki
Mradi wa Sayansi
Septemba 2024


“Mradi wa Sayansi,” Rafiki, September 2024, 18–19.

Mradi wa Sayansi

“Baba wa Mbinguni anataka sisi tuendelee kujaribu.”

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Mvulana akichezea mchanga

Bradley alitupa kikombe kingine cha mchanga kwenye ndoo yake. Alikuwa anahitaji mwingi!

Maonyesho ya sayansi ya shule yake yalikuwa yanakaribia. Bradley alikuwa anatengeneza aina ambayo inaonesha jinsi tsunami zilivyofanya kazi. Alijifunza kwamba tsunami ni wimbi kubwa la maji linalosababishwa na tetemeko la ardhi ndani ya bahari. Alitaka mradi wake uwe kamili. Pengine angeweza kushinda zawadi!

Wakati ndoo yake ilipojaa, Bradley alikusanya baadhi ya vijiti. Kisha alipata pipa la plastiki na nyumba ndogo za mwanasesere katika ghorofa ya chini ya nyumba yao.

Bradley alimwaga mchanga ndani ya pipa kutengeneza adthi. Kwa umakini aliweka nyumba hizo na miti. Ilifuatia sehemu inayofurahisha—maji. Mara alipoyamwaga ndani, angeweza kusukuma kipande cha kadibodi kupitia maji kutengeneza wimbi.

Lakini kisha alifanya kosa kubwa. Alimwaga ndani maji mengi sana. Nyumba zilijaa mafuriko—na alikuwa bado hata hajatengeneza wimbi bado. Udongo uliolowa ulitengeneza tope la kunata, lenye takataka.

Mvulana akifanya kazi kwenye mradi.

Bradley alimwita mama yake jikoni. “Nitafanya nini sasa? Niliweka maji mengi ndani.”

“Hiyo ni SAWA. Unaweza tu kuanza upya,” alisema Mama. “Acha tufanye pamoja na tuweke maji kidogo kila wakati.”

“SAWA.” Bradley aliinamisha kichwa chake na alikwenda nje kuchukua mchanga zaidi.

Wakati huu kwa umakini walipima kiasi sahihi cha maji na wakayamwaga ndani. Bradley aliondoa kadibodi na akaangalia mawimbi yakigonga mchanga. Imetokea!

Kisha Bradley na Mama walifanya kazi ya kuandaa bango lake. Alianza kuandika baadhi ya kweli za kuburudisha kuhusu tsunami. Lakini maneno hayakukaa vyema kwenye ukurasa.

“Sitaki kuyaandika tena!” Bradley alisema. Kichwa chake kilianza kuuma.

“Hatuhitaji kuyaandika upya yote,” alisema Mama. “Tunaweza tu kuandika maneno mapya yatakayokaa vyema kwenye ukurasa.”

Bradley aliguna. Bango lake halikuonekana kabisa kama alivyotaka liwe. “Sitaki kufanya hivyo. Litaonekana baya kama maneno hayakai kikamilifu.”

Mvulana akifanya kazi kwenye mradi

“Kujifunza kunaweza kuwa kugumu.” Mama alimkumbatia. “Nyakati fulani tufanya makosa. Lakini kitu muhimu ni kwamba hatukati tamaa. Baba wa Mbinguni anataka sisi tuendelee kujaribu. Kwa hiyo acha tupumzike na tumalizie asubuhi.”

Asubuhi iliyofuata, walimalizia bango lake. Halikuwa kamilifu, lakini Bradley alijihisi vizuri kidogo.

Mwishowe siku ya maonyesho ya sayansi ilifika. Mama alimpeleka Bradley shuleni. “Kumbuka,” mama alisema, “umefanya kazi kwa bidii kwenye mradi wako na umejifunza mengi. Na hicho ndicho kinachotakiwa.”

Bradley alibeba mradi wake kwenye chumba kikubwa cha mazoezi ya viungo. Chumba kilijaa miradi na mabango Wanadarasa wote wa darasa la nne walikuwa wamekaa chini na kungojea zamu yao kuonesha mradi wao.

Punde iliwadia zamu ya Bradley. Moyo wake ulipiga kwa kasi alipokuwa anaenda mbele. Vipi kama kila kitu kikienda vibaya?

Bradley alisukuma kadibodi kupitia maji na aliwaonesha waamuzi jinsi mawimbi yalivyogonga ardhi.

“Nini kinasababisha mawimbi hayo makubwa katika bahari?” mmoja wa waamuzi aliuliza.

“Mawimbi makubwa yanasababishwa na . . .” Akili za Bradley hazikuwa na jibu. “Siwezi kukumbuka. Lakini ninaweza kukuelezea baadhi ya kweli za kuburudisha kuhusu tsunami.” Alizisoma kweli kwenye bango lake.

Mvulana akiwasilisha mradi

Baada ya shule Bradley aliingia ndani ya gari pamoja na mradi wake.

“Ilienda vipi?” Mama aliuliza.

“Sio sawa sawa kama nilivyotaka.” Bradley alitabasanu. “Lakini nilifanya kwa uwezo wangu na kuendelea kujaribu.”

PDF

Vielelezo na Adam Koford