Rafiki
Kushangilia Timu Zote Mbili
Septemba 2024


“Kushangilia Timu Zote Mbili,” Rafiki, Septemba. 2024, 30–31.

Kushangilia Timu Zote Mbili

Jayne alikunja uso. Hakutaka timu pinzani ishinde!

Hadithi hii ilitokea huko Korea ya Kusini.

Jayne alikula kijiko kimoja cha mwisho cha tambi zake. Mmmm. Tamu sana!

“Acha tucheze Yut Nori!” Mjomba Ji-Ho alisema.

Ulikuwa muda ule wa mwaka tena! Familia yake ilikuwa inasherehekea Chuseok, Sikukuu ya Kikorea ya Kutoa Shukrani. Familia ya Jayne leo imekusanyika kula vyakula vingi na kucheza Yut Nori pamoja. Yut Nori ulikuwa mchezo pendwa wa Jayne.

Kila mtu alikaa katika mduara kwenye sakafu. Jayne aliangalia huku na huko. NI timu gani alitaka kuwamo ndani yake? Alienda mbio kukaa karibu na Mjomba Ji-Ho. “Ninataka kuwa kwenye timu yako!” alisema. “Tutakuwa washindi wakubwa!”

Mjomba Ji-Ho alicheka. “Tukiwa na wewe kwenye timu yetu, tuna hakika ya nafasi nzuri!”

Mama wa Jayne aliuweka ubao wa mchezo katikati ya mduara. Jayne alimsaidia kuweka vyema vipande. Waliwapasia vijiti vinne timu ambayo itakwenda kuanza.

Ndugu wa Jayne Ana alikuwa wa kwanza. Alirusha vijiti hewani. Jinsi vijiti vilivyotua vilionesha nafasi ngapi ambazo timu ingeweza kusogea kwenye ubao wa michezo. Vijiti vyote vinne vilikuwa vina tazama chini, ambayo ilimaanisha kwamba Ana alipata Yut! Aliinuka kusogeza vipande vya timu yake mbele nafasi nne na alipata zamu nyingine ya ziada ya kucheza.

Lakini Ana hakuwa kwenye timu ya Jayne.

Jayne akakunja mikono yake na kukunja paji la uso wake. “Nilikuwa nategemea asingekuwa na mrusho mzuri,” alinong’ona kwa Mjomba Ji-Ho.

“Shangilia!” Mjomba Ji-Ho alisema. “Mchezo ndio tu umeanza.” Alimpa tabasamu la kumtia nguvu.

Baada ya zamu ya pili ya Ana timu ya Jayne ilitupa vijiti. Lakini hawakupata kusogeza vipande vyao mbali ya timu ya Ana ilivyofanya.

Na kila zamu, wanafamilia ya Jayne walishangilia na kucheka. Jayne aliangalia vipande vya mchezo vikisogea kuzunguka ubao. Kila mtu alikuwa na furaha.

Familia ikicheza mchezo

Kila mmoja isipokuwa Jayne. Timu yake bado ilikuwa inapoteza.

Hatimaye ilikuwa zamu ya Jayne. Alirusha vijiti hewani, lakini kimoja tuu kilitua uso chini. Vipande vya timu yake vilisogea mbele nafasi moja tu.

Jayne akakunja mikono yake. “Sitaki kuendelea” alipaza sauti. “Ninataka sisi tushinde.”

Ghafla, kila mtu alikuwa kimya. Alipoangalia juu, familia yake ilikuwa ikimtazama yeye. Walionekana kushangazwa kwamba alikuwa amekasirika sana.

Uso wa Jayne ulihisi moto. Alijihisi vibaya kwamba hakuwa mwenye furaha kwa ajili ya familia yake. Kwa kawaida hakuwa na hasira sana. Alisimama wima kuondoka kwenye duara.

Mjomba Ji-Ho aliinua mkono wake. “Huhitaji kuondoka,” alisema. “Kushinda sio kila kitu. Jaribu tu kuburudika.”

“SAWA.” Jayne alikaa chini tena. Alitaka kuburudika kama watu wengine. Alivuta pumzi kwa nguvu na alimwangalia binamu yake Ben akitupa juu vijiti.

“mrusho mzuri Ben!” Mjomba Ji-Ho alisema. Alionekana kuwa mwenye furaha.

Jayne alimwangalia Mjomba Ji-Ho kwa kumkazia macho. Alikuwa anashangilia timu nyingine! Inawezekana kwamba hiyo ndiyo sababu alikuwa anaburudika sana.

Wakati zamu iliyofuata ilipoanza, Jayne aliamua kumshangilia kila mtu kwenye timu zote mbili. Mjomba Ji-Ho alikuwa sahihi. Kushinda hakukuwa kila kitu. Yesu angeweza kumsaidia yeye kuwa na furaha kwa ajili ya wanafamilia yake hata kama alipoteza.

Wakati ilipokuwa zamu ya Ana tena, Jayne alitabasamu kwake. “Kila la heri!. Umeipata hii!”

Kutoka kwenye mduara, Ana alimrudishia tabasamu. Jayne alihisi vizuri moyoni. Alikuwa tayari kupata burudani!

PDF

Kielelezo na Uran Duo