Rafiki
Wewe ni Nani Hasa
Septemba 2024


“Wewe ni Nani Hasa,” Rafiki, Septemba. 2024, 32– 33.

Rafiki kwa Rafiki

Wewe ni Nani Hasa

Mzee Kevin W. Pearson

Kutoka kwenye mahojiano na Olivia Kitterman na Diana Evelyn Nielson.

Yesu Kristo pamoja na watoto

Baba Yetu wa Mbinguni anatupenda. Yeye anataka kutusaidia tujue sisi ni kina nani. Yeye aliumba nafsi zetu kabla hatujaja kuishi duniani. Sisi sote ni wana na mabinti wa Mungu.

Wakati mwingine tunaweza kuhisi wapweke au wenye wasiwasi kwamba kamwe hatutakuwa wema vya kutosha. Yesu Kristo anajua kikweli jinsi gani tunavyohisi. Yeye atatusaidia kushinda changamoto yoyote. Mambo magumu ambayo tunakabiliana nayo katika maisha haya yanaweza kutusaidia kuwa zaidi kama Yesu Kristo kama tukimgeukia.

Injili hutusaidia sisi kujiona wenyewe kama Baba wa Mbinguni anavyotuona. Kupitia imani yetu katika Yesu Kristo, majaribu yetu yanaweza kugeuka kuwa baraka. Kujua wewe ni nani na jinsi Mungu anavyokuona kutambariki yeyote katika umri wowote!

Tunapokuja kujua sisi ni kina nani kama watoto wa Mungu, tutaweza kulenga kwenye ni nani Baba wa Mbinguni anatutaka sisi tuwe. Tutakabiliana na changamoto zetu pamoja naye. Hata kama sisi sio wakamilifu na tutafanya makosa, tunaweza kupata matumaini katika kujua sisi ni watoto wa Mungu.

Tafuta Uvipendavyo

Sisi sote tu tofauti. Tuna vipawa tofauti, tuvipendavyo na tusivyovipenda. Sisi sote ni watoto wa Mungu!

Tumia vidokezo kujaza chati na tafuta nini kila mmoja wa marafiki hawa anapendelea. Dokezo: Weka X kwa kile unachojua ni sio kweli. Cha kwanza kimefanywa kwa ajili yako. Utakapomaliza, kila mraba unapaswa kuwa na mraba mmoja mtupu!

  1. Mpiga kinanda sio Amara au Jade.

  2. Max hapendi hisabati.

  3. Hakuna kati ya wavulana anayecheza chombo cha mziki au kucheza karate.

  4. Msichana anayependa wanyama sio Amara.

  5. Kai ni mmoja tu anayependa mpira wa kikapu.

PDF

Vielelezo na Sabrina Gabrielli