Rafiki
Nefi Anasali kwa ajili ya Watu
Septemba 2024


“Nefi Akisali kwa ajili ya Watu,” Rafiki, Septemba 2024, 26–27.

Hadithi za Maandiko

Nefi Anasali kwa ajili ya Watu

Nabii Nefi

Nefi alikuwa nabii. Alipewa jina kama jina la Nefi aliyepata mabamba ya shaba. Alikuwa na wasiwasi kuhusu watu. Walikuwa wameacha kumfuata Mungu.

Nefi akisali kwenye bustani yake

Nefi alikwenda kwenye bustani yake. Alipanda mnara katika bustani yake na alisali kwa Mungu. Alisali kwa ajili ya watu.

Watu wakimtazama Nefi akisali

Baadhi ya watu walimwona Nefi juu ya mnara. Walisimama kusikiliza na waliwakusanya wengine kusikiliza. Nefi alipomaliza kusali, aliwaona walikuwa wanaangalia na alianza kuwafundisha.

Nefi akiwafundisha watu

Nefi aliwaomba watu kutubu. Baadhi yao hawakupenda kile Nefi alichofundisha. Lakini wengine wengi walisikiliza! Walichagua kutubu na walibadilisha njia zao.

Watu wakisali
PDF

Vielelezo na Andrew Bosley