Rafiki
Shughuli za Njoo, Unifuate
Septemba 2024


“Shughuli za Njoo, Unifuate,” Rafiki, Septemba. 2024, 28–29.

Shughuli za Njoo, Unifuate

Kwa ajili ya jioni ya nyumbani, au kujifunza maandiko—au kwa ajili ya burudani tu!

Agosti 26–Septemba 1

Misingi Thabiti

Kwa ajili ya Helamani 1–6

A bird feeder on a rock and knocked down.

Helamani alifundisha wanawe kujenga maisha yao juu ya Mwamba imara wa Yesu Kristo (ona Helamani 5:12). Msingi ni kitu kile ambapo juu yake hujengwa kitu fulani. Msingi imara unafanya jengo zima kuwa imara, hata katika dhoruba. Jenga minara miwili—mmoja juu ya msingi imara na mmoja juu ya msingi dhaifu. Mnara gani ni thabiti zaidi? Ni kwa jinsi gani tunaweza kujenga maisha yetu juu ya Yesu Kristo?

Septemba 2–8

Ushuhuda wa Kristo

Kwa ajili ya Helamani 7–12

A girl reads something to a boy sitting on a couch.

Watu wengi katika maandiko walifundisha na kushuhudia juu ya Yesu Kristo (ona Helemani 8:16–20). Wewe pia unaweza kuanza kujenga ushuhuda wako kuhusu Yeye! Ushuhuda ni kitu fulani unachoamini au kujua ni cha kweli kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Andika ushuhuda wako na kuwa na desturi ya kuushiriki na familia yako au marafiki.

Septemba 9–15

Samweli Akipanda Ukuta

Kwa ajili ya Helamani 13–16

A boy and a girl cutting out and creating crafts.

Samweli alikuwa nabii aliyefundisha kuhusu Yesu Kristo juu ya ukuta wa mji (ona Helemani 13:4). Nenda kwenye ukurasa wa 12 na fanya sanaa kukusaidia kuelezea hadithi ya Samweli.

Septemba 16–22

Mchezo wa Kukusanya

Kwa ajili ya 3 Nefi 1–7

Children playing a game, one of them has a hand raised.

Yesu Kristo aliahidi atawakusanya watoto Wake wote kwa sababu Yeye anampenda kila mtu na anawataka wawe na injili (ona 3 Nefi 5:24) Cheza mchezo kuhusu kukusanya. Wafanye wachezaji wasimame katika duara. Mtu mmoja katikati anasema ukweli kuhusu wao, kama rangi yao wanayoipenda. Kiuhalisia hiyo ni kweli kwa yoyote kwenye mchezo, wote wanakuja katikati pia. Endelea mpaka kila mmoja amekusanyika katikati.

Septemba 23–29

Yesu ni Nuru

Kwa ajili ya 3 Nefi 8–11

A boy drawing at a table.

Yesu Kristo ni “nuru na uzima wa ulimwengu” (3 Nephi 9:18). Angalia mawio au machweo pamoja na familia yako. Kisha chora picha ya kile ulichokiona. Wakati unapochora, zungumza kuhusu sababu unazompendea Yesu Kristo na jinsi Yeye anavyokuletea nuru.

PDF

Vielelezo na Katy Dockrill