“Sanduku la Hofu,” Rafiki, September 2024, 36–36.
Sanduku la Hofu
Olivia alifikiria kuhusu hofu yake sana.
Hadithi hii ilitokea huko Marekani.
Olivia alitoka kwa haraka nje ya darasa lake kabla shule haijaisha. Alijaribu kutomwangalia yeyote machoni.
Leo ilikuwa siku ya kwanza ya Olivia ya matibabu. Mama yake alielezea kwamba atakuwa anakutana na daktari ambaye angeweza kumsaidia na hofu yake. Olivia alihisi kuwa na hofu mno. Wakati mwingine alihisi hofu mno kiasi kwamba ilikuwa vigumu kulala au kuburudika na marafiki zake.
Oliva aliingia ndani ya gari pamoja na Mama na alikaa kivivu katika kiti chake.
“Je, uko SAWA?” Mama aliuliza.
Olivia hakujibu kwa dakika chache. “Kwa nini ninahitaji kwenda kwa daktari?”
Mama alianza kuendesha gari. “Baba wa Mbinguni hutupa madaktari kutusaidia. Kama vile jinsi Yeye anavyotupa vitu vingine kutusaidia, kama marafiki na maandiko. Unakumbuka mnyororo wa maandiko tulioutengeneza?”
Olivia aliitikia kwa kichwa. Mama alikuwa amemsaidia kupata mistari ya maandiko ambayo ilimsaidia na hofu yake. Kwenye kila mstari, Mama aliandika mahali pa kupata mstari unaofuata. Wakati Olivia alipokuwa na hofu usiku aliweza kusema sala na kupata moja ya mistari katika maandiko. Kisha alisoma mistari mingine katika mnyororo mpaka aliweza kulala.
Wakati Olivia na Mama walipoingia katika ofisi ya daktari, Dkt. Posy alijitambulisha mwenyewe. Alimuuliza Olivia kuhusu hisia zake. Olivia akamwambia kidogo tu kuhusu hofu yake.
“Watu wengi wana kitu fulani kinachoitwa wasiwasi,” Dkt. Posy alisema. “Wanakuwa na hofu mno kama wewe ulivyo. Lakini unaweza kufanya baadhi ya vitu fulani kukusaidia kuhisi hofu kidogo. Unaweza kujaribu mojawapo ya hayo pamoja nami?”
Olivia alitazama viatu vyake na alikubali kwa kichwa.
Dkt. Posy alimpa Olivia sanduku dogo. “Hili ni sanduku la hofu. Linaondoa hofu yetu kwa usalama, ili tusiwezi kufikiria kuihusu.
Olivia aliligeuza sanduku mikononi mwake. Halikuonekana kama kitu chochote maalumu.
“Wakati mwingine ukihisi woga, andika hofu yako kwenye kipande cha karatasi na weka ndani ya sanduku,” Dr. Posy alisema. “Kisha tafufa muda kufungua sanduku kila siku kwa ajili ya muda wa hofu. Kama una hofu kuhusu chochote kabla ya muda wa hofu, sema, ‘Sihitaji kufikiri kuhusu hili sasa hivi.”
“SAWA,” Olivia alisema. Dkt. Posy alimsaidia kuandika hofu yake kubwa, na Olivia aliziingiza mwenye sanduku.
Baadaye siku ile, moja ya hofu ya Olivia ilijitokeza kwenye kichwa chake. Upo kwenye sanduku la hofu, alijiambia mwenyewe. Nitakuwa na hofu kuhusu hilo baadaye. Alijaribu kuacha kufikiria kuhusu hilo. Badala yake alijaribu kucheza na kaka yake.
Wakati ulipofika wa kwenda kulala, Olivia alihisi woga. Muda wa usiku ulikuwa ndipo hofu yake inakuwa mbaya sana. Aliweka sanduku lake la hofu na maandiko karibu na kichwa chake na alimwita Mama.
“Vipi kama haifanyi kazi?” aliuliza.
Mama alimpa kumbatio. “Tutaendelea kujaribu. Baba wa Mbinguni atakusaidia kupata njia zingine ambazo zinasaidia.”
Olivia alikubali kwa kichwa. “Inawezekana ninapaswa kuandika hilo kwa ajili ya sanduku la hofu pia.
“Wazo zuri,” Mama alisema. Alisali pamoja na Olivia. Hiyo ilimsaidia Olivia kijihisi vizuri kidogo.
Kitambo kidogo baada ya Mama kuzima taa, hofu ilijitokeza ndani ya kichwa cha Olivia Aliwasha taa yake. Aliandika hofu na kuweka kwenye sanduku kwa ajili ya baadaye. Alisali sala nyingine kumwomba Baba wa Mbinguni kumfariji.
Kisha aliyafungua maandiko yake na kutafuta mistari iliyoangaziwa kutoka mnyororo wa maandiko yake. Wa kwanza alioupata ulikuwa Isaya 41:10. Ulisema, “Usiogope; kwani Mimi niko pamoja nawe.”
Karibu na mstari, Mama alikuwa ameandika “Mafundisho na Maagano 6:36.” Olivia alipekua maandiko yale na aliyasoma kwa sauti. “Nitegemeeni katika kila wazo; msitie shaka, msiogope.”
Olivia alihisi amani. Alijua kuwa atakuwa pengine anafikiri juu ya hofu zaidi. Lakini Baba wa Mbinguni amempa vitu vingi kumsaidia kujihisi vizuri zaidi. Alikuwa amejibu sala zake. Na hiyo ilimsaidia sana!