“Mnyororo wa Kusoma Maandiko,” Rafiki, September 2024, 38.
Kitu cha kuburudisha
Mnyororo wa Kusoma Maandiko
Maandiko yanaweza kutusaidia kuhisi faraja na upendo kutoka kwa Baba wa Mbinguni. Unaweza kutengeneza mnyororo wa kusoma maandiko wakati unapohisi kuwa na hofu au huzuni.
Maumbo ya zambarau yana baadhi ya mistari ya maandiko unayoweza kutumia. Unaweza kuongeza uvipendavyo pia.
Mwombe mzazi au kiongozi wa Darasa la Watoto kwa msaada!
-
Tengeneza orodha yako ya mistari ya maandiko unayoipenda.
-
Katika maandiko yako, tafuta mstari wa kwanza kwenye orodha yako. Tumia penseli ya rangi kupakaa juu ya mstari.
-
Karibu yake, andika mrejeo wa maandiko (au namba ya ukurasa, kama hiyo ni rahisi kwako) kwa ajili ya mstri wa maandiko unaofuata kutoka kwenye orodha. Kisha nenda kwenye mstari ule na upakie rangi pia.
-
Endelea kupaka rangi mistari na kuandika marejeo kwa ajili ya maandiko yanayofuata. Utakapopaka rangi ule wa mwisho kwenye orodha yako, andika marejeo ya maandiko kwa ajili ya maandiko ya kwanza uliyoyapakia rangi.
-
Yohana 14:27: “Amani nawaachieni, amani yangu nawapa: niwapavyo mimi, sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike.”
-
Mafundisho na Maagano 68:6: “Kwa hiyo, changamkeni, na msiogope, kwani Mimi Bwana nipo pamoja nanyi, na nitasimama karibu yenu;
-
Mithali 3:5 “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote.”
-
M&M 121:7: ”Amani iwe katika nafsi yako; taabu yako na mateso yako yatakuwa kwa muda mfupi.”
-
M&M 45:62: “Kwani amini ninawaambia, kwamba mambo makubwa yanawasubiri.”
-
Mithali 3:24: “Wakati utakapolala, kamwe usiogope: ndiyo:utalala, na usingizi wako utakuwa mtamu.”