“Liahona,” Rafiki, Feb. 2024, 26–27.
Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki, Februari 2024
Liahona
Bwana alimwambia Lehi kwenda kwenye nchi ya ahadi pamoja na familia yake. Lakini hawakuwa na uhakika wa jinsi gani ya kufika huko.
Bwana alimpa Lehi kifaa maalumu. Kilikuwa kama dira. Kilionesha njia ambayo walitakiwa kwenda. Walikiita Liahona.
Walipozishika amri, Liahona ilifanya kazi. Iliwaongoza kwenye chakula na usalama. Lakini walipobishana na kutotii, iliacha kufanya kazi.
Familia ya Lehi waliifuata Liahona , hivyo waliweza kufika kwenye nchi ya ahadi. Tunapofanya uchaguzi ulio sahihi, Baba yetu wa Mbinguni Atatuongoza pia.
© 2024 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, February 2024. Language. 19276 743