“Vijana Askari Mashujaa,” Rafiki, Agosti 2024, 26-27.
Ujumbe wa Kila Mweziwa Jarida la Rafiki la Agosti 2024
Vijana Askari Mashujaa
Vielelezo na Andrew Bosley
Watu ambao Amoni na kaka zake waliwafundisha walitaka kumfuata Yesu Kristo. Walizika silaha zao na kumuahidi Mungu kwamba kamwe hawatapigana tena.
Lakini punde walihitaji kulinda familia zao. Akina baba waliozika silaha zao hawakutaka kuvunja ahadi yao na Mungu. Hivyo wana wao walijiandaa kupigana badala yao. Waliitwa wale askari vijana elfu mbili. Mvulana humaanisha “kijana.”
Vijana askari hawakuwahi kupigana vita hapo awali. Lakini mama zao walisaidia kuwaandaa na kuwafundisha kumtumaini Mungu.
Walimchagua Helamani kuwa kiongozi wao. Walikuwa jasiri, na Mungu aliwasaidia. Wote waliumizwa, lakini walisaidiana. Mungu aliheshimu imani yao, na wote waliishi!
Ukurasa wa Kupaka Rangi
Maandiko Yanaweza Kunisaidia Mimi Kila Siku.
Kielelezo na Adam Koford
Ni hadithi gani ya maandiko unayoipenda?
© 2024 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, Agosti 2024 Swahili. 19290 743