Rafiki
Nefi Anamwona Mtoto Yesu
Desemba 2024


“Nefi Anamwona Mtoto Yesu,” Rafiki, Desemba 2024, 26–27.

Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki, Desemba 2024

Nefi Anamwona Mtoto Yesu

Lehi akimfundisha Nefi, na Nefi akisali

Vielelezo na Andrew Bosley

Baba yake Nefi, Lehi, aliona ono la Yesu Kristo. Nefi alitaka kuona ono hili pia. Aliomba na kuuliza kuona kile baba yake alichokiona.

Nefi akimwona Mariamu katika ono

Roho Mtakatifu alimwonyesha Nefi ono hilo hilo. Nefi alimwona msichana aitwaye Mariamu. Roho Mtakatifu alisema angekuwa mama wa Mwana wa Mungu, Yesu Kristo.

Nefi anamwona Mariamu na Mtoto Yesu katika ono

Nefi alimwona mtoto Yesu akiwa na Mariamu. Roho Mtakatifu alisema kwamba Yesu angekuja duniani kuwasaidia watoto wa Baba wa Mbinguni.

Nefi akiandika ono lake; msichana akisoma maandiko

Nefi aliona maisha ya Yesu Kristo. Alimwona akiwatumikia na kuwafundisha watu. Nefi alijifunza mambo mengi kuhusu Mwokozi. Unaweza pia kujifunza kuhusu Yeye kwa kusoma maandiko.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Krismasi Ni kuhusu Yesu

Ukurasa wa Kupaka rangi

Kielelezo na Adam Koford

“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume” (Isaya 9:6).