2022
Mapatriaki: Walikuwa Watu Gani na Kwa Nini Ni Muhimu
Februari 2022


“Mapatriaki: Walikuwa Watu Gani na Kwa Nini Ni Muhimu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Feb. 2022.

Ujumbe wa kila mwezi Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Februari 2022

Mwanzo 11–50

Mapatriaki

Mapatriaki: Walikuwa Watu Gani na Kwa Nini Ni Muhimu

Labda umesikia kuhusu Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Tunasoma kuwahusu mara kwa mara katika Kitabu cha Mormoni na bila shaka utasikia zaidi kuwahusu unapojifunza Agano la Kale mwaka huu. Kwa wingi wa umakini unaotolewa kwao, lazima wawe ni wa muhimu sana, sivyo? Lakini unaweza kujiuliza, “Kwa nini wanaume watatu walioishi maelfu ya miaka iliyopita wana umuhimu leo?” Naam, umuhimu wa jibu hilo upo katika maagano ya milele na baraka zilizoahidiwa ambazo Mungu aliwapa.

Ibrahimu

Picha
Ibrahimu

Vielelezo na Jarom Vogel

Ibrahimu alikuwa nabii mkuu. Alikuwa mwadilifu na mtiifu kwa amri za Mungu.

Alibatizwa, akapokea ukuhani na aliunganishwa pamoja na mkewe Sarah kwa milele yote.

Mungu alifanya agano na Ibrahimu kwamba uzao wake ungekuwa mkubwa na wangepata baraka sawa na zile alizopokea Ibrahimu.

Wangepeleka utimilifu wa injili ya Yesu Kristo kwa mataifa ya dunia.

Isaka

Picha
Isaka

Isaka alikuwa mwana wa Ibrahimu na Sara.

Mungu alimwambia Ibrahimu amtoe Isaka kama sadaka. Ibrahimu alimpenda Isaka lakini alichagua kumtii Mungu. Muda mfupi kabla ya Ibrahimu kumtoa Isaka sadaka, malaika alimwambia Ibrahimu aache. Utayari wa Ibrahimu na Isaka wa kumtii Mungu ni ishara ya Upatanisho wa Mwana wa Pekee wa Mungu.

Isaka aliahidiwa baraka sawa na za Ibrahimu.

Yakobo

Picha
Yakobo

Kama vile baba yake na babu yake, Yakobo alikuwa mwaminifu kwa Mungu.

Kwa sababu ya uaminifu wake, Bwana alibadilisha jina la Yakobo kuwa Israeli, ambalo linamaanisha “mtu anayeshinda pamoja na Mungu” au “acha Mungu ashinde” (ona Bible Dictionary, “Israel”).

Yakobo alikuwa na wana 12. Wana hao na familia zao walijulikana kama makabila ya Israeli.

Agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu lilifanywa upya na Yakobo na watoto wake.

Mapatriaki na Wewe

Kama muumini wa Kanisa, wewe ni sehemu ya uzao wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Agano walilofanya na Mungu linakuhusu wewe!

Una baraka na wajibu wa kutoa ushuhuda wako wa Mwokozi na kushiriki injili.

Umeitwa pia kumualika kila mtu kufanya na kutunza maagano na kupokea ibada za ukuhani. Rais Russell M. Nelson amesema kwamba hii yote ni sehemu ya kukusanya Israeli, “kitu ambacho ni muhimu zaidi kinachofanyika duniani leo” (“Hope of Israel,” [worldwide youth devotional, June 3, 2018], 8, ChurchofJesusChrist.org).

Chapisha