Juu Yangu
Haya hapa ni mashairi ya wimbo huu kutoka katika albamu ya Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2024.
1. Ninapaswa kulipa stahili zangu;
Niko mbali na maisha kama Yako.
Najaribu lakini mimi ni mwanadamu tu,
Hali endelevu ya kujiboresha.
Lakini nausikia uzito
Ukiinuliwa toka sahani yangu.
Orodha ninayo ya mambo niliyokosea,
Maumivu yote niliyovumilia mpaka sasa
Haki ilishikilia karata,
Rehema ilionekana mbali sana
Kisha ukaingilia kati yangu na hatima yangu
Ukajitwalia hukumu niliyopaswa kulipa.
Sawa sawa na mistari ya nukta,
Ukaweka jina lako juu ya langu.
Langu. Langu. Langu.
2. Nawiwa nawe nafsi yangu yote; sasa
Nawiwa nawe kila dakika.
Lolote nifanyalo halitoshi.
Nawiwa nawe milele.
Lakini yote utakayo ni moyo wangu uliovunjika.
Orodha ninayo ya mambo niliyokosea,
Maumivu yote niliyovumilia mpaka sasa
Haki ilishikilia karata
Rehema ilionekana mbali sana
Kisha ukaingilia kati yangu na hatima yangu
Ukajitwalia hukumu niliyopaswa kulipa.
Sawa sawa na mistari ya nukta,
Ukaweka jina lako juu ya langu.
Langu. Langu. Langu.
Orodha ninayo ya mambo niliyokosea,
Maumivu yote niliyovumilia mpaka sasa
Haki ilishikilia karata
Rehema ilionekana mbali sana
Kisha ukaingilia kati yangu na hatima yangu
Ukajitwalia hukumu niliyopaswa kulipa.
Sawa sawa na mistari ya nukta,
Ukaweka jina lako juu ya langu.
Langu. Langu. Langu.
Nawiwa nawe nafsi yangu yote; sasa
Nawiwa nawe kila dakika.