Njoo, Unifuate
Kumbatia Siku Zako
Je, Unahaja ya kuishi katika yaliyopita? Basi, Usifanye hivyo
Je, umewahi kufikiria maisha yako yangekuwa rahisi zaidi au bora kama ungezaliwa katika nyakati za zamani? Wengine wamewahi kuhisi hivyo kabla—hata nabii, wakati mmoja.
Nabii Nefi (katika kitabu cha Helamani) aliona kiburi na uovu wa watu wake na kupuza sauti: “Ee, kwamba ningeliishi katika siku ambazo baba yangu Nefi alipotoka mara ya kwanza kutoka nchi ya Yerusalemu … — … ndipo roho yangu ingejawa na shangwe” (Helamani 7:7–8).
Alikuwa na wakati mgumu kuishi katika wakati wake. Mwishoni, ndiyo, alipaswa kuukabili uhalisia: “Lakini … hizi ndizo siku zangu” (Helamani 7:9).
Siku Zako
Hizi ni siku zako. Zinaweza kuleta changamoto, lakini pia zinatoa fursa. Kwa mfano, katika siku zako unaweza:
-
Kukusanya Israeli kutoka pande zote mbili za pazia. Hiki “ni kitu muhimu zaidi kinachofanyika duniani leo.” Unazo njia nyingi za kushiriki injili na kuwaalika wengine kujongea karibu zaidi na Yesu Kristo na Kanisa Lake. Unaweza kusaidia kugundua mababu katika njia za kushangaza na kuwasaidia wale waliofariki dunia kupokea ibada za hekaluni.
-
Tumia teknolojia katika njia chanya. Una vifaa maalumu vya kuonyesha ulimwengu jinsi teknolojia ya kisasa inavyoweza kutumika kwa manufaa.
-
Pinga chuki, dharau na migawangiko. Huku mabaa haya maovu yanapoenea katika ulimwengu wetu, wewe unaweza kuonyesha njia bora zaidi-njia ya Mwokozi ya ukarimu, huruma, upatanishi, na upendo.
-
Kuwa thabiti katika ulimwengu unaobadilika. Unapokuwa mwenye shukrani kwa Yesu Kristo, injili Yake, na Kanisa Lake, Bwana atakubariki, na wengine wataona mfano wako katika dhoruba za maisha.
Miujiza Yako
Haikuwa daima rahisi kwa Nefi, lakini alikuwa mahali (na wakati) Bwana alipohitaji yeye awepo. Yeye alikuwa mwaminifu. Kama matokeo, aliona miujiza na maajabu katika siku zake na aliungwa mkono na Bwana. (Ona Helamani 7–16.)
Unaweza kuona miujiza na maajabu yako mwenyewe wakati unapokuwa mwaminifu katika siku zako.