Yesu Kristo ni Nguvu Yako.
Ni nini “Mtazamo Wako”?
Mtazamo wako kwa kanuni zilizoko katika mwongozo wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana unaweza kukusaidia wewe kupaa hadi anga za juu.
Marubani wanaelezea ndege inapokuwa mahali pake angani kama mkao. Je, pua la ndege iko juu au chini? Inageuka au inaenda moja kwa moja na usawa? Katika Kiingereza, mtazamo inaweza pia kumaanisha msimamo kwa ajili ya kushughulika na milima na mabonde ya maisha. Msemo wa zamani unaosema kuhusu vyote kuruka na maisha ni huu: “Mtazamo wetu huamua mkao wetu.
Je, mtazamo wetu utakuwa nini tunaposoma Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi? Mtazamo wetu kuhusu kanuni zilizoko katika mwongozo unaweza kuwa wenye kubadilisha maisha na kuweza kuleta athari kama tutapaa hadi upeo wa juu au tutazama chini zaidi.
Mwokozi ametupa mahali pazuri pa kuanzia. Yeye alisema, “Heri wenye upole” (Mathayo5:5). Tunaweza kufanyia mazoezi kuwa na mtazamo wa upole kwa kuwa wenye kutenda haki, wanyenyekevu, na walio tayari kufuata mafundisho ya injili. Hapa kuna maswali matatu ambayo yanaelezea mtazamo tofauti tunaoweza kuwa nao kuhusu kanuni ambazo tumepewa.
Mtazamo wa 1: Ninaweza Kuwa Mbaya Jinsi Gani?
Wale walio na mtazamo huu wanasema, “Mstari uko wapi? Ninataka kuishi karibu nao kadiri iwezekanavyo pasipo kuuvuka.” Ni hatari kama ilivyo kwa mruka angani aulizaye, “Ninaweza kuwa karibu ya ardhi kwa kiasi gani kabla ya kufungua parachuti langu?”
Mtazamo wa 2: Napaswa Kuwa Mwema Jinsi Gani?
Mtazamo huu unatafuta juhudi ndogo inayowezekana. Hii ni kama kumuuliza mwalimu, “Ninaweza kufanya nini kidogo na bado nikafaulu darasani?” Ni kama mzamia angani akisema, “ninataka kufanya kazi nzuri ya kupakia parachuti langu, lakini siyo ile nzuri sana.”
Mtazamo wa 3: Naweza Kuwa Shujaa Jinsi Gani?
Mvulana mmoja wakati mmoja aliniambia alikwenda seminari saa 11:00 alfajiri. Nilimwambia, “Hiyo ilikuwa mapema sana. Kwa nini unaenda? Kwa urahisi tu alinijibu, “Kwa sababu ninataka kwenda. Ninapenda Seminari ni sehemu bora ya siku yangu. Mtazamo wake ulikuwa “ninataka kuwa shujaa!” Kwake yeye, utii ulikuwa kitu cha kutafuta, siyo usumbufu.
Hiyo ni kama mpiga mbiziangani akisema, “ninapakia parachuti langu kwa uangalifu na kulifungua mapema kabla ya kutua ardhini kwa sababu ninapenda kupiga mbizi angani na nataka kuendelea kufanya hivyo.” Mtazamo kama huo utatusaidia kupaa.
Katika Kitabu cha Mormoni, Baba wa Mfalme Lamoni alitoa sala nzuri sana ambayo kwa ukamilifu ilielezea ule mtazamo wa tatu:
“Ee Mungu … unaweza kujitambulisha kwangu, na nitaacha dhambi zangu zote ili nikujue wewe” (Alma 22:18).
Mfalme hakusema, “Jinsi gani ninaweza kuwa mbaya na kukujua wewe?” au “Hasa niwe mwema kiasi gani ili nikujue wewe?” Hapana, mtazamo wake ulikuwa “Nitaacha dhambi zangu zote ili nikujue wewe.”
Tabia za Juu na Takatifu Zaidi.
Bwana anatumaini sisi tusitafute mianya lakini badala yake tutafute tabia za juu na takatifu zaidi. Kama kitu hakijatamkwa kwa uwazi katika mwongozo kama ambavyo tungetarajia, basi tusiulize, “Je, Bwana ataruhusu nini?” bali “Je, Mungu angependelea nini?” Swali la pili linafunua moyo ulio tayari ambao Bwana anataka kila mmoja wetu kukuza kama anavyotufundisha kuwa wenye upole.
Kama ninaingia ndani ya ndege, sitaki rubani aulize “Naweza kuwa mbaya jinsi gani?” au hata “Ninaweza kuwa mzuri jinsi gani?” Ninamtaka kuuliza, “Ninaweza kuwa shujaa jinsi gani?” Katika kuruka na katika maisha, mtazamo utaamua mwinuko wetu. Mwongozo wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana haukuandikwa ili kuelezea viwango vya chini vya tabia bali ni mafundisho kwa ajili ya uanafunzi. Kwa kweli ni kiwango cha juu.