Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Jinsi ya Kufanya Mkutano Mkuu Kuwa na Maana Zaidi Kwako
Septemba 2024


Jinsi ya Kufanya Mkutano Mkuu Kuwa na Maana Zaidi Kwako

Jaribu mawazo haya matatu kwa ajili ya kufanya mkutano mkuu kuwa tukio muhimu.

mimbari

Vielelezo na Jarom Vogel

Mkutano mkuu unakuja, na unakusudiwa kuwa na matokeo ambayo yatadumu kupita siku za mkutano mkuu huo! Vidokezo hivyo vitatu vinaweza kuufanya mkutano mkuu kuwa wa maana zaidi kwako wewe.

msichana na maandiko

1. Jiandae Mwenye Kiroho

Kabla ya mkutano mkuu, unaweza kuiandaa roho yako kupitia mambo rahisi kama kujifunza maandiko na sala ya dhati. Unaweza hata kufanya mfungo wa mitandao ya kijamii au kufanya safari maalumu ya hekaluni. Kujiandaa kiroho kutakusaidia wewe kuhisi nguvu ya mwongozo wa Roho Mtakatifu.

mvulana akiwa na swali

2. Kuwa na Swali Akilini

Ni kitu gani kimekuwa akilini mwako hivi karibuni? Yawezekana ukawa na uamuzi muhimu wa kufanya, tatizo la kifamilia, au swali la injili. Omba kwa Baba wa Mbinguni kuhusu hilo, sikiliza mwongozo wakati wa mkutano mkuu.

Tazama uzoefu ambao James alikuwa nao mwaka uliopita!

Mkutano mkuu ulipokuja, nilitaka kujua jinsi gani ningeweza kutumia vyema nguvu ya Upatanisho wa Kristo katika maisha yangu. Kwa sala nilimwomba Baba wa Mbinguni anisaidie ili nimsikilize Roho, nijue jinsi ya kufanya chaguzi bora, na nisamehewe juu ya chaguzi zangu mbaya.

Wakati Mzee Dieter F. Uchtdorf alisema, hili lilikaa kwangu:

“Dakika ile unapoamua kurudi na kutembea katika njia ya Mwokozi na Mkombozi wetu, nguvu Zake zitaingia ndani ya maisha yako na kuyabadilisha.

Nilijua hili ndilo ambalo Bwana alitaka nisikie, na niliweza kuhisi Roho akishuhudia kwangu juu ya ukweli wake. Kwa kujiandaa nikiwa na swali akilini, niliweza kupokea jibu binafsi la sala zangu.

James M., 16, North Dakota, Marekani

msichana akiwa na shajara

3. Tumia Kanuni au Mwaliko

Sikiliza kwa ajili ya mafundisho au kanuni ambayo itakuwa ya kipekee kwako. Kisha fanya lengo la kuvitumia katika maisha yako. Unaweza pia kusikiliza kwa makini kwa ajili ya mialiko ya moja kwa moja kutoka kwa manabii na mitume. Andika chini na ufanyie kazi angalau moja ya mialiko hiyo. Kutenda kwa imani kutakusaidia kuhisi ukweli na nguvu za mafundisho ya kinabii.