Vidokezo 5 kwa ajili ya afya bora ya Kihisia
Tunasimama imara tukiwa pamoja.
Mume wangu, Scott, na mimi tulihudumu kama viongozi wa misheni katika Mishenii ya Australia Sydney kuanzia 2018 mpaka 2021. Wakati wowote rekodi za mmisionari zilipoonyesha walikuwa wakipambana na afya yao ya kihisia, niliwataka wajue moja kwa moja kwamba nimeishi kupitia nyakati hizo za msongo wa mawazo maisha yangu yote ya utu uzima. Niliwataka waelewe kwamba tulikuwa kwenye timu moja hivyo hawakutakiwa kukabiliana na hili peke yao.
Ningependa kushiriki ujumbe huo huo na ninyi! Hivyo watu wengi wanasumbuka na changamoto za afya ya kihisia, na wakati sisi sote tunaweza kusaidiana. Ili kuwa wazi: Mimi siyo mtaalamu wa afya ya kihisia. Lakini ningependa kushiriki vidokezo vichache vya kawaida na vya kiroho kwa ajili ya ubora wa afya ya kihisia ambavyo vimenisaidia mimi vile vile na wale ninaowajua na kuwapenda.
Kidokezo cha 1: Tumweke Kristo kama Kitovu
Nilikulia karibu na San Francisco, California, Marekani, na ninakumbuka kupenda kuendesha michezo ya burudani kwenye uwanja ulioko ufukweni! Ilikuwa na sahani kubwa la mbao ambalo ungekaa juu yake na kujaribu kubakia hapo wakati sahani hilo likizunguka kwa haraka zaidi. Wale ambao walikaa kuelekea upande wa nje kwa kawaida hurushwa nje kwanza. Wale ambao walielewa nguvu ya kani itokanayo na mzunguko, hata hivyo, walikaa karibu na katikati.
Nafikiri hiyo ni analojia kubwa ya kumweka Kristo kama kitovu wakati tunapopitia baadhi ya hali hizi ngumu—iwe ni wasiwasi, msongo wa mawazo, OCD, au kitu kama hicho. Tunahitaji Kristo kuwa kitovu cha maisha yetu.
Katika nyakati za changamo za kiafya, tunaweza kuwa muunganiko uliozimika na mbingu au kuwa na wakati mgumu wa kuhisi ukaribu wa Mwokozi. Hii haimaanishi tunakuwa tunaadhibiwa au kwamba hatustahili upendo wa Mungu. Kwangu mimi, kutumaini kuwa yupo pale wakati nikisubiria muunganiko kurejeshwa ni jambo la thamani. Endelea kusali, thamini maneno ya Mwokozi, amini ahadi Zake, pokea sakramenti, na ufanye yale yote yanayofanya Yeye kuwa kitovu.
Kidokezo cha 2: Acha Tumtegemee Bwana Kila Siku
Wana wa Israeli nyikani walimtegemea Bwana kwa mana kila siku. Nyakati tunaposhughulika na mambo mazito kama shambulio la hofu kubwa inayomwingia mtu ghafla au maumivu mengine ya kihisia, tunataka yaondoke yasirudi tena. Na labda yatarudi—lakini yawezekana siyo katika njia ile au katika ratiba ya wakati ambao tungependa. Hiyo haimaanishi kwamba matumaini yamepotea. Tunahitaji kumtegemea Mungu kila siku tunapofanya kazi na kutazamia nyakati angavu mbele yetu.
Njia mojawapo ni kutafuta usaidizi wa Baba wa Mbinguni na kujaribu maarifa tofauti ili kupata yanayofanya kazi vizuri kwako. Kisha Yeye anaweza kukusaidia kukumbuka, wakati wa nyakati nzito au shambulio la hofu kubwa ya ghafla, jinsi gani muziki wenye kupoza maumivu unavyoonekana kusaidia katika hali kama hiyo au jinsi gani kujiunganisha na mtu unayemwamini kulikufanya ujisikie salama wakati mmoja. Hii inakusaidia wewe kukusanye seti za zana zilizothibitishwa ili kujaribu wakati ujao wa changamoto. Chochote unachofanya, tafuta usaidizi wa Bwana kila siku.
Tunaweza hata kusema kwa sauti: Ninapomtegemea Bwana kila siku, nitainuka na kupata nguvu ambayo sikujua kuwa ninayo!”
Kidokezo cha 3: Unaweza Kushughulikia Mwili Wako
Ubongo ni sehemu ya mwili wetu na kwa hiyo ni wenye kuweza kuathiriwa kwa urahisi na aina nyingi ya hali zisizo timilifu za maisha ya kidunia. Lakini habari njema ni: kuna hatua zilizothibitishwa tunazoweza kuchukua ili kuimarisha ubongo wetu ambazo zinaweza pia kuboresha afya yetu ya kihisia. Hapa kuna hatua chache kama hizo:
-
Kuwa kwenye jua au mwangaza mng’avu wa bandia asubuhi
-
Toka nje katika mazingira asilia, jiunganishe na dunia
-
Fanya mazoezi mara kwa mara.
-
Kula chakula chenye afya
-
Kunywa maji mengi
-
Pata usingizi wa kutosha kila usiku
Mbinu za kupumua zinaweza kuwa na nguvu pia. Jaribu kuvuta pumzi moja ndefu kupitia pua yako, na fanya hivyo tena. Shikilia kwa dakika chache, mwishowe, lazimisha pumzi yako yote itoke kupitia mdomo wako.
Ninafanya hivi mara chache wakati ninapoamka, wakati wa nyakati za hisia ngumu (kama vile tu kabla ya kuzungumza kwenye mkutano mkuu!), na kabla tu ya kulala.
Kidokezo cha 4: Tunaweza Kuomba Usaidizi
Kama ulikuwa umepotea ukiwa katika matembezi ya umbali mrefuna ukakutana na mwongozaji, ungeona haya sana kuomba usaidizi ili kufikia usalama? Sidhani. Kuomba msaada siyo ishara ya udhaifu. Mara nyingi tunafanya hivyo katika maeneo mengine ya maisha yetu.
Saidia kuvunja unyanyapaa dhidi ya kuomba msaada wa changamoto za kihisia.
Iwe unataka usaidizi kutoka kwa Mungu, marafiki, familia au wataalamu wa tiba, wewe siyo mtu dhaifu kwa kuomba usaidizi wa ziada unaohitaji. Ukweli ni kwamba, wewe unapanda mbegu ya ujasiri!
Kidokezo cha 5: Acha Tubaki Tumeunganika
Kujiunganisha na Baba yako wa Mbinguni katika sala ya kila siku ni muhimu.
Pia nahisi ni muhimu sana kubakia wenye kuunganika na watu tunaoweza kuhisi tuko salama nao na tunawaamini. Mpigie simu mama yako. Ongea na rafiki yako uso kwa uso. Ongea na ndugu yako wa tumbo moja. Tunakuwa imara zaidi wakati tunaposaidiana sisi kwa sisi. Nguvu hiyo inaenda njia zote mbili. Kila mtu anamhitaji mtu. Kujitenga na msongo wa mawazo mara nyingi hutegemeana. Kujiunganisha na wale tunaowapenda na kuishi nao na tunaoweza kuwaona na kuwapa kumbatio ni dawa kubwa ya maumivu mengi tunayopitia.
Tunaweza Kustahimili Tanuru la Moto pamoja na Yeye!
Wakati mwingine tunahitaji tu kukumbushwa kwamba Mungu yu pamoja nasi.
Katika Agano la Kale, Mfalme Nebukadreza aliwatupa Shadraka, Meshaki, na Abednego kwenye tanuu ya moto mkali ambao hata walinzi waliokuwa nje hawakuweza kuvumilia joto lake.
Kwani hawa watatu walinusurika vipi?
Maandiko yanafundisha kwamba mtu wa nne aliweza kuonekana katika ndimi za moto pamoja nao ambaye alikuwa “kama Mwana wa Mungu” (Danieli 3:25).
Ninaamini hii inamaanisha Kristo yuko pamoja nasi katika joto la majaribu yetu, hususani tunapovumilia. Na changamoto za afya ya ubongo inaweza kwa uhakika kuwa kama tanuu ya joto kali. Kristo ndiye Imanueli, ambayo kwa uhalisia inamaana ya “Mungu pamoja nasi.”
Usisahau, Yesu Kristo ndiye nguvu yetu, siyo tu mwisho wa barabara, tunapokuwa huru kutokana na changamoto za hisia ambazo hatukuomba. Kwa hakika Yeye yu pamoja nasi katika safari yetu yote. Yeye ni nguvu yetu na msaada wetu sasa hivi.
Hebu tusimame imara pamoja!