“Je, ni kitu gani hasa ambacho tunaahidi wakati tunapobatizwa?,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Juni 2024.
Ujumbe wa kila mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Juni 2024
Je, ni kitu gani hasa ambacho tunaahidi wakati tunapobatizwa?
Maandiko yanatufundisha kwamba wakati tunapobatizwa, tunaweka agano (au tunaahidi) kuwa radhi kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo, kumtumikia Mungu, na kushika amri Zake (ona Mosia 18:10; Mafundisho na Maagano 20:37, 77).
Pia tunajifunza katika maandiko kwamba ubatizo unatusaidia kutimiza matamanio yetu ya “kuja katika zizi la Mungu, na kuitwa watu wake” (Mosia 18:8). Kwa maneno mengine, sababu mojawapo ya sisi kubatizwa ni kwamba tunataka kujiunga na Kanisa la Yesu Kristo na kufurahia upendo na mjumuisho ambavyo huja kutokana na kuwa wamoja katika Kristo.
Msimamo wa kumtumikia Bwana na kushika amri zake unaweza kujumuisha mambo mengi kote katika maisha yetu. Kwa mfano, hujumuisha “kuwa radhi kubebeana mizigo, … kuomboleza na wale wanaoomboleza; ndiyo, na kuwafariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa, na kusimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote, na katika mahali popote” (Mosia 18:8–9).
© 2024 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19 Tafsiri ya Monthly For the Strength of Youth Message, June 2024. Swahili. 19299 743