2010–2019
Je! Si Sisi Sote ni Waombaji?
Oktoba 2014


15:41

Je! Si Sisi Sote ni Waombaji?

Tajiri au maskini, sisi tunaweza “kutenda tunavyoweza” wakati wengine wana mahitaji.

Ni kitu cha kupendeza kipya jinsi gani kulichoanzishwa katika fomati ya mkutano wetu mkuu. Bien Hencho, Eduardo.

Katika kile ambacho kingekuwa ni wakati wa kushangaza wa huduma Yake ya awali, Yesu alisimama katika sinagogi la nyumbani Kwake Nazareti, na akasoma maneno haya yaliyotabiriwa na Nabii Isaya na kuandikwa katika Injili ya Luka: “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa.”1

Hivyo Mwokozi alifanya tangazo Lake la kwanza la wazi la huduma ya Kimasiya. Lakini mstari huu pia umeweka bayana kwamba akiwa njiani kuelekea kwenye upatanisho wa dhabihu Yake isiyo na mwisho na Ufufuko, kazi ya Kimasiya ya kwanza na ya msingi ya Yesu ingekuwa ni kuwabariki maskini, ikijumuisha maskini katika roho.

Kutoka mwanzo wa huduma Yake, Yesu aliwapenda walio na mahitaji na wenye mapungufu katika njia ya ajabu. Alizaliwa katika nyumba ya wawili wao na kukua miongoni mwa wengi sana wao. Hatujui utondoti wote wa maisha Yake ya hapa duniani, lakini wakati mmoja alisema, “Mbweha wana pango, na … ndege … wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.”2 Inavyoonekana Muumbaji wa mbingu na nchi, “na vitu vyote vilivyomo”3 alikuwa, angalau katika maisha Yake ya ukubwani, hakuwa na sehemu ya kulala.

Katika historia yote, umaskini umekuwa mojawapo wa changamoto kubwa sana na zilizoenea aa binadamu. Ni mateso yanayotokana na umaskini ambayo ni ya kimwili, lakini madhara ya kiroho na kifikra yanayoweza kutokea yanaweza kuwa ya madhara makubwa. Katika hali yoyote mwito wa kusisitiza ambao Mkombozi mkuu aliutoa kwa ajili yetu ni kujiunga Naye katika kuwasaidia watu kubeba mizigo. Kama Yehova alisema angehukumu nyumba ya Israeli kwa ukali sana kwa sababu “vitu mlivyowateka maskini vi ndani ya nyumbani zenu.

“Ni nini maana yake” Alisema kwa sauti, “ninyi kuwaonea watu wangu, na kuseta nyuso za maskini?”4

Mwandishi wa Mithali angefanya jambo hili kuwa la wazi kabisa. “Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake.” na “azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, … atalia [pia] lakini hatasikiwa.”5

Katika siku zetu kabla Kanisa la Yesu Kristo la urejesho lilikuwa bado halijamaliza mwaka wa kwanza Bwana aliwaamuru washiriki wake “na nitawaangalia maskini na …wenye shida na kuwapatia msaada ili kwamba wasiteseke.”6 Tazama sauti ya kuamuru katika kifungu cha maneno—“wasiteseke.” Hiyo ndio lugha ambayo Mungu anaitumia anapomaanisha ni kitu cha muhimu.

Ukizingatia changamoto nzito ya kusuluhisha usawa duniani, ni kitu gani mtu anaweza kukifanya? Bwana Mwenyewe alitoa jibu. Karibu na kusalitiwa kwake na mateso, Mariamu alimpaka mafuta Yesu kichwani kwa kutumia mafuta ya gharama ya kuzikia, Yuda Eskarioti alipinga upotevu na “kumnungunikia.”7

“Yesu alisema:

“Mbona mnamtaabisha mwanamke? Amenitendea kazi njema. …

“Ametenda alivyoweza.”8

“Ametenda alivyoweza”! Ni mpangilio wa nguvu jinsi gani! Mwandishi aliwahi kumuuliza Mother Teresa wa Calcutta kuhusu kazi yake isiyo na matumaini ya kuwaokoa maskini katika mji huo. Alisema kwamba, kutokana na takwimu, hakuwa anafanya chochote kile cha mafanikio. Mwanamke huyo wa kutambulika mdogo alijibu kwamba kazi yake ilikuwa ni kuhusu upendo, siyo takwimu. Mbali na idadi kubwa ya watu ambao hakuweza kuwasaidia, alisema kwamba aliweza kutii amri ya kumpenda Mungu na jirani zake kwa kuwasaidia wale ambao anaweza kuwafikia kwa rasilimali yoyote aliyokuwa nayo. “Tunachokifanya ni sawa na tone kwenye bahari,” angesema wakati mwingine. “Lakini kama tusingefanya hivyo, bahari ingepungukiwa na tone moja [kuliko ilivyo].”9 Kwa ujasiri mwandishi alihitimisha kwamba Ukristo si kwamba ni juhudi kuhusu juhudi za takwimu. Alitafakari kwamba kungekuwa na furaha zaidi mbinguni kwa mtenda dhambi mmoja anayetubu kuliko watu tisini na tisa ambao hawahitaji toba, hivyo basi inaonekana Mungu hajalishwi na asilimia.10

Je tunawezaje “kutenda tunavyoweza”?

Kwa kitu kimoja, tunaweza, kama Mfalme Benjamin alivyofundisha, tusizuie msaada kwa sababu tunaona kama maskini wamejisabishia matatizo. Labda baadhi yao wamejisababishia matatizo, lakini si kwamba wengine wetu tuliobaki hufanya hivyo hivyo? Je si ndio sababu huyu kiongozi mwenye huruma anauliza, “Si sisi sote ni waombaji?”11 Je hatuombi msaada tukiwa tayari kufanya chochote na tumaini na majibu ya maombi? Je hatuombi msamaha kwa ajili ya makosa tuliyoyafanya na shida tuliyoisababisha? Je sisi sote hatuombi ile rehema ili irekebishe udhaifu wetu. Kwamba rehema itaishinda haki angalau katika hali hii? Haistaabishi, hivyo kwamba Mfalme Benjamini anasema tunapokea ondoleo la dhambi kwa kuomba kwa Mungu, ambaye kwa huruma hujibu, lakini tunapata ondoleo la dhambi kwa kuwasaidia kwa huruma maskini wanaotuomba.12

Kwa kuongeza katika kuchukua hatua ya huruma kwa niaba yao, tunapaswa tuwaombee pia wale wenye mahitaji. Kundi la Wazoramu, walichukuliwa na washiriki wenzao kuwa “najisi” na “takataka,” hayo ni maneno ya kimaandiko---walitupwa nje ya nyumba za maombi “kwa sababu ya nguo zao hafifu.” Walikuwa, Mormoni anasema, “maskini katika mambo ya kidunia; na pia ….maskini katika roho”13 Hali mbili ambazo kila mara huenda pamoja. Wenza wa wamisionari Alma na Amuleki wanapinga dhidi ya kukataliwa kwa wale waliovyaa kihafifu kwa kuwaambia kwamba fursa yoyote watu wengine watawanyima, wanaweza kusali kila mara–katika sehemu zao na katika nyumba zao, katika familia zao na katika mioyo yao.14

Lakini sasa, kwa kundi hili hili ambalo lilikuwa limenyimwa kuingia, Amuleki anasema: “Baada ya kufanya [maombi] ikiwa [ninyi] mtawafukuza maskini, na walio uchi, na msiwatembelee wagonjwa na walioteseka na kuwagawia mali yenu, ikiwa [ninyi] [mnayo], wale ambao wanahitaji---Ninawaambia ninyi,…sala yenu ni ya bure kwani haitawapatia chochote, na [ninyi] ni kama wanafiki ambao wanakana imani.”15 Ni Ukumbusho wa namna gani kwamba tajiri au maskini, tutende tunavyoweza” wakati wengine wana mahitaji.

Sasa ili nisisingiziwe kushauri programu za viwango vya juu vya kote lakini zenye kuleta majibu mazuri katika kuwasaidia maskini ambazo zitatufanya tujisikie vizuri, ninakuhakikishia heshima katika kanuni za kiwanda, uangalifu katika kutumia pesa, kujitegemea, na malengo makuu ni imara kama ile ya mwanaume au mwanamke aliyehai. Mara zote tunategemewa kujisaidia kabla ya kutafuta msaada kutoka kwa wenzetu. Zaidi, sijui hasa hasa ni kwa vipi kila mmoja wenu atatimiza jukumu lake kwa wale ambao hawawezi au hawataweza kujisaidia. Lakini najua kwamba Mungu anajua, na Yeye atakusaidia na kukuongoza katika tendo la upendo la kiufuasi kama kwa uangalifu unataka na kuomba na kutafuta njia za kutii amri alizotupa mara kwa mara.

Utagundua kwamba ninaongea hapa juu ya mahitaji magumu ya jumuiya ambayo si ya washiriki wa Kanisa peke yao. Kwa bahati nzuri njia ya Bwana ya kusaidiana ni rahisi; wote wenye uwezo kimwili wanategemewa kutii sheria ya mfungo. Isaya aliandika:

“Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? …

Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo …[ili wewe] umsaidie mizigo mizito, na …waache wanaoteswa wawe huru… ?”16

Nashuhudia kuhusu miujiza, yote ya kiroho na kimwili, inayokuja kwa wale wanaoishi sheria ya mfungo. Ninashuhudia juu ya miujiza ambayo imenijia. Kweli, kama Isaya alivyosema, nimesali nilivyokuwa nafunga zaidi ya mara moja, na kweli Mungu amejibu, “Nipo hapa.”17 Furahieni fursa hii takatifu angalau kila mwezi, na muwe wakarimu jinsi mazingira yatakavyoruhusu katika matoleo ya mfungo na katika misaada mingine, elimu, na michango ya misionari. Ninahahidi kwamba Mungu atakuwa na hisani nanyi, wale wanaopata msaada kutokana na mkono wako wataliita jina lako mbarikiwa milele. Zaidi ya robo tatu ya washiriki milioni wa Kanisa wamesaidiwa mwaka jana kwa matoleo ya mfungo ambayo hutolewa kupitia maaskofu maalumu na marais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Hao ni watakatifu wengi wa siku za mwisho wenye shukrani.

Ndugu na kina dada, mahubiri kama haya yanahitaji kwamba kwa uwazi nitambue baraka ambazo sikuzifanyai kazi, nisizostahili, zisizo na mwisho katika maisha yangu, zote za kimwili na za kiroho. Kama ninyi nimekuwa na wasi wasi kuhusu uchumi mara kwa mara, lakini sijawahi kuwa maskini au sijui umaskini ukoje. Zaidi ya hapo sijui sababu zote za ni kwa nini mazingira ya uzazi, afya, elimu na fursa za kiuchumi zinapishana sana hapa katika maisha ya hapa duniani, lakini ninapoona mahitaji kati ya wengi ninajua kwamba “kama isingekuwa rehema ya Mungu na mimi ningekuwa katika hali hiyo hiyo.”18 Vile vile ninajua kwamba ingawa siwezi kuwa mlinzi wa ndugu yangu, mimi ni ndugu ya ndugu yangu, na “kwa sababu nimepewa mengi, na mimi pia nitoe.”19

Katika mwonekano huo mimi mwenyewe namheshimu Rais Thomas Spencer Monson. Nimebarikiwa kuwa uhusiano na mtu huyu kwa miaka 47 sasa, na taswira yake katika akili yangu ambayo nitaiheshimu kila mara ya wakati akirudi nyumbani kutoka nchi wakati huo iliyojulikana kama---Ujerumani ya Mashariki iliyoathirika sana kiuchumi akiwa amevalia makobanzi kwa sababu alikuwa ametoa si tu koti lake la pili na shati za ziada na hata vile viatu kutoka kwa miguu yake. “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima [na ikitembea katika uwanda wa ndege] miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani.”20 Zaidi ya mtu yeyote ninayemjua, Rais Monson “ametenda alivyoweza,” kutoka kwa wajane na wasio na baba, maskini na wanaodhulumiwa.

Mnamo mwaka 1831 ufunuo kwa Nabii Joseph Smith, Bwana alisema kwamba siku moja maskini angeuona ufalme wa Mungu ukija kuwaokoa katika nguvu na utukufu mkubwa.”21 Ninatumaini kwamba tutasaidia kutimiza unabii huo kwa kuja katika nguvu na utukufu wa ushiriki wetu katika Kanisa la Yesu Kristo la kweli kutenda tunachoweza kumwokoa yeyote tunayeweza kutoka katika umaskini na ufukara ambao unaowaweka utumwani na kuharibu ndoto zao zote, ninaomba katika jina lenye rehema la Yesu Kristo, amina.