Kwa Nini Ndoa, Kwa Nini Familia
Familia iliyojengwa kwenye ndoa ya mwanaume na mwanamke hupatiana mazingira bora ya mpango wa Mungu kushamiri.
Juu ya Lango Kuu maarufu la Magharibi la Westminster Abbey katika London, Uingereza, pamesimama sanamu za mashahidi 10 wakristo wa karne ya 20. Miongoni mwao ni Dietrich Bonhoeffer, mwanateolojia Mjerumani mwenye akili sana, aliyezaliwa mnamo mwaka wa 1906. 1 Bonheoffer alikuwa mkosoaji mkali wa utawala wa mabavu wa Nazi na walivyowatendea Wayahudi na wengine. Alitupwa gerezani kwa ajili ya shughuli za upinzani na mwishowe akauawa katika kambi ya wafungwa wa kisiasa. Bonheoffer alikuwa mwandishi mahiri, na baadhi ya kazi zake zinazojulikana sana ni barua ambazo walinzi waliomuunga mkono walisaidia kuficha na kuzitoa nje ya gereza, baadaye zilichapishwa kama Letters and Papers from Prison.
Mojawapo wa barua hizo ilikuwa ni kwa mpwa wake wa kike kabla ya harusi yake. Ilikuwa na huu umaizi muhimu: “Ndoa ni zaidi ya upendo wa mmoja kwa mwingine. … Katika penzi lenu mnaona tu ninyi wawili katika ulimwengu, bali katika ndoa ninyi mnaunganishwa na msururu wa vizazi, ambavyo Mungu amesababisha iwe na kupita kwa utukufu wake, na anaowaita katika ufalme wake. Katika penzi lenu mnaona tu mbingu ya furaha yenu wenyewe, bali katika ndoa mmewekwa katika nafasi ya majukumu kwa ulimwengu na binadamu. Penzi lenu ni mali yenu ya kibinafsi, lakini ndoa ni zaidi ya kitu cha kibinafsi---ni hadhi, ofisi. Kama vile ilivyo na taji, na siyo tu kuwa radhi kutawala, ambalo humfanya mfalme, vivyo ndivyo ilivyo na ndoa, siyo tu penzi lenu mmoja kwa mwingine, ambalo huwaunganisha pamoja katika macho ya Mungu na binadamu. … Hivyo basi penzi hutoka kwenu, lakini nayo ndoa hutoka juu, kutoka kwa Mungu.” 2
Ni kwa njia gani ndoa kati ya mwanamume na mwanamke inapita penzi lao mmoja na mwingine na furaha yao kuwa “nafasi ya majukumu kwa ulimwengu na binadamu”? Ni kwa hali gani inatoka “hutoka juu, kutoka kwa Mungu”? Ili kuelewa, tunahitaji kurudi nyuma huko mwanzoni.
Manabii wamefunua kwamba sisi kwanza tulikuwepo kwa viumbe akili, na kwamba tulipewa umbo, au miili ya kiroho, na Mungu, basi kuwa watoto Wake wa kiroho---wana na mabinti wa wazazi wa mbinguni.3 Kukaja wakati katika hali hii ya kuwepo kiroho kabla ya miasha ya mauti ambapo, katika kuendeleza hamu Yake kwamba “tungeweza kuwa na fursa ya kuwa kama yeye mwenyewe,” 4 Baba yetu wa Mbinguni alitayarisha mpango wa kuwezesha. Katika maandiko umepatiwa majina tofauti, ikijumuisha “mpango wa wokovu,”5 “mpango mkuu wa furaha,” 6 na “mpango wa ukombozi.” 7 Makusudi mawili muhimu ya mpango huu yaliezewa kwa Ibrahimu katika maneno haya:
“Na hapo akasimama mmoja miongoni mwao ambaye alifanana na Mungu, naye akasema kwa wale waliokuwa pamoja naye: Sisi tutakwenda chini, kwani kuna nafasi huko, nasi tutachukua vifaa hivi, nasi tutaifanya dunia mahali ambapo hawa [roho] watapata kukaa;
“Nasi tutawajaribu kwa njia hii, ili kuona kama wao watafanya mambo yote yale ambayo Bwana Mungu wao atawaamuru;
“Na wao ambao watatunza hali yao ya kwanza wataongezewa; … nao wale watakaoitunza hali yao ya pili watapata kuongezewa utukufu juu ya vichwa vyao kwa milele na milele.” 8
Kwa sababu ya Baba yetu wa Mbinguni, tulikuwa tayari tumekuwa viumbe wa kiroho. Sasa Yeye alikuwa anatupatia njia ya kutimiza au kukamilisha hicho kiumbe. Nyongeza ya kimwili ni muhimu kwa ujalivu wa kuwa na utukufu ambao Mungu Mwenyewe anao. Kama, tukiwa pamoja na Mungu katika dunia ya kiroho kabla kuzaliwa, tungekubali kushiriki katika mpango Wake---au kwa maneno mengine “kuitunza hali ya kwanza”---tungeweza “kuongezewa,” mwili tunapokuja kuishi hapa ulimwenguni ambao Yeye aliumba kwa ajili yetu.
Kama basi, katika hali ya duniani, tulichagua “kufanya mambo yote ambayo Bwana Mungu [wetu] [ange]tuamuru [sisi],” tungeweza kuitunza ‘hali yetu ya pili.” Hii inamaanisha kwamba kwa chaguo zetu tungemwonyesha Mungu (na kwetu mwenyewe) kujitolea kwetu na uwezo wetu wa kuishi sheria Yake ya selestia wakati tukiwa nje ya uwepo Wake na katika miili na nguvu zake zote, tamaa, na hamu. Je! Tungeweza kuthibiti nyama ili kwamba iwe chombo badala ya bwana wa roho? Je! Tungeaminiwa na yote katika muda milele na nguvu za kiungu, ikijumuisha nguvu ya kuumba uhai? Je! Tungeweza kushinda uovu peke yetu? Wale walioweza wangeweza “kupata utukufu kuongezewa juu ya vichwa vyetu milele na milele”---hali muhimu sana ya utukufu huo kuweza kufufuliwa, kutokufa, na kutukuka kimwili. 9 Si ajabu sisi “tulishangilia kwa furaha” kwa ajili ya uwezekano huu wa ajabu na ahadi. 10
Angalau vitu vinne vinahitajika kwa ufanisi wa huu mpango wa kiungu:
Kwanza ilikuwa ni Uumbaji wa nchi kama mahali pa makao yetu. Utondoti wowote wa mfanyiko wa uumbaji, tunajua kwamba haukuwa kwa bahati na sibu bali kwamba ulielekezwa na Mungu Baba na ukatekelezwa na Yesu Kristo---“vitu vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.”11
Pili ni hali maisha ya duniani. Adamu na Hawa walitenda kwa wote ambao walichagua kushiriki katika mpango mkuu wa furaha wa Baba.12 Kuanguka kwao kulizaa hali zilizohitajika kuzaliwa kimwili na uzoefu wa maisha ya duniani na kujifunza nje ya uwepo wa Mungu. Kwa Kuanguka ukaja ufahamu wa mema na maovu na uwezo wa uliotolewa na Mungu wa kuchagua.13 Hatimaye, Kuanguka kulileta kifo cha mwili kilichohitajika ili kufanya wakati wetu wa duniani kuwa wa muda, kwa hivyo tusipate kuishi milele katika dhambi.14
Tatu ni ukombozi kutoka kwa Kuanguka. Tunaona nafasi ya kifo katika mpango wa Baba yetu wa Mbinguni, lakini huo mpango unaweza kuwa bure bila kuwa na njia fulani za kushinda kifo hapo mwishowe, yote kimwili na kiroho. Basi, Mkombozi, Mwana wa Pekee wa Mungu, Yesu Kristo, aliteseka na kufa ili kulipia uvunjaji wa sheria wa Adamu na Hawa, kwa hivyo kuleta ufufuo na kutokakufa kwa wote. Na kwa vile hakuna yeyote kati yetu ambaye angekuwa anaweza kuwa mtiifu kamili na kila mara kwa sheria ya injili, Upatanisho pia hutukomboa kutoka na dhambi zetu wenyewe kwa sharti la toba. Kwa neema ya upatanisho ya Mwokozi ikitoa msamaha wa dhambi na kutakasa nafsi, tunaweza kuzaliwa tena kiroho na kupatanishwa na Mungu. Kifo chetu cha kiroho---utenganisho wetu kutoka kwa Mungu---utakoma.15
Nne, na mwisho, ni mazingira ya kuzaliwa kwetu na kufuatiwa na kuzaliwa tena kiroho katika ufalme wa Mungu. Ili kazi Yake kufaulu “[kutuinua sisi] naye mwenyewe,”16 Mungu ameteua kwamba wanaume na wanawake wanapaswa kuoana na kuzaa watoto, kwa hivyo kuumba, katika wenzi na Mungu, miili ambayo ni muhimu katika mtihani wa duniani na muhimu kwa utukufu wa milele Naye. Yeye pia ameteua kwamba wazazi wanapaswa kuanzisha familia na kulea watoto wao katika nuru na ukweli,17 unaowaelekeza wao kwenye tumaini katika Kristo. Baba alituamuru sisi:
“Wafundisheni watoto wetu kwa uwazi, akisema:
Kwamba ... kadiri ninyi mlivyozaliwa katika ulimwengu kwa maji, na damu, na roho, ambavyo nilivifanya, na hivyo kuwa vumbi la nafsi iliyo hai, hata hivyo lazima mzaliwe tena katika ufalme wa mbinguni, kwa maji, na kwa Roho [Mtakatifu], na kuoshwa kwa damu, hata damu ya Mwanangu wa Pekee; ili mpate kutakaswa kutokana na dhambi zote, na kufurahia maneno ya uzima wa milele katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao, hata utukufu katika mwili usiokufa.”18
Kujua kwa nini tuliondoka kutoka kwa uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni na kile kinachohitajika ili kurudi na kuinuliwa pamoja Naye, inakuwa wazi sana kwamba hakuna chochote kinacholingana na wakati wetu hapa duniani ambacho kinaweza kuwa muhimu kuliko kuzaliwa kimwili na kuzaliwa tena kiroho, kuna mahitaji mawili ya uzima wa milele. Nayo ni, nikitumia maneno ya Dietrich Bonheoffer, “ofisi” ya ndoa, “nafasi ya majukumu kwa … binadamu,” kile hiki kitengo cha kiungu “kutoka juu, kutoka kwa Mungu” hufanyiza. Ni “kiungo katika msururu wa vizazi” kote hapa na baada ya hapa---mpangilio wa mbinguni.
Familia iliyojengwa juu ya ndoa ya mwanaume na mwanamke hutoa mazingira bora kwa mpango wa Mungu kushamiri---mazingira kuzaliwa kwa watoto ambao huja katika uhalisi na umaasumu kutoka kwa Mungu na mazingira ya kujifunza na kujitayarisha watakayohitaji kwa ufanisi wa miasha ya duniani na uzima wa milele katika ulimwengu ujao. Kiasi fulani cha familia zilizojengwa katika ndoa kama hizo ni muhimu sana kwa jamii kustahimili na kunawiri. Hii ndiyo kwa nini jamii na mataifa kwa kawaida huhimiza na kulinda ndoa na familia kama kitengo chenye nafasi ya upendeleo. Haijapata kamwe kuwa ni kuhusu penzi na furaha ya watu wazima.
Mjadala wa sayansi ya kijamii wa ndoa na familia inayoongzwa na mwanamume na mwanamke waliooana ni wa kuvutia sana.19 Na hivyo, “tunaonya kwamba kusambaratika kwa familia kutaletea watu binafsi, jamii na mataifa majanga yaliyotabiriwa na manabii wa zamani na wa kisasa.”20 Lakini madai yetu ya nafasi ya ndoa na familia msingi wake si sayansi ya kijamii bali ni juu ya ukweli kuwa ni uumbaji wa Mungu. Ni Yeye hapo mwanzoni alimuumba Adamu na Hawa katika mfano wake, kiume na kike, na akawaunganisha wao kama mume na mke kuwa “mwili mmoja” na wazae na kuijaza nchi.21 Kila mtu anabeba mfano wa kiungu, lakini ni katika muungano wa ndoa ya kiume na kike ambapo kama kitu kimoja tunaweza kupata labda maana kamili kabisa ya sisi kuwa tuliumbwa katika mfano wa Mungu---kiume na kike. Wala sisi ama mtu mwingine yule anaweza kubadili huu mpangilio wa kiungu wa ndoa. Huu si ubunifu wa binadamu. Ndoa kama hiyo “inatoka juu, kutoka kwa Mungu” na vivyo hivyo kuwa sehemu ya mpango wa furaha kama vile Kuanguka na Upatanisho.
Katika ulimwengu wa kabla kuzaliwa, Shetani aliasi dhidi ya Mungu na mpango Wake, upinzani wake unaendelea kukua tu katika ukali. Anapiga vita kuzuia ndoa na kuundwa kwa familia, na pale ndoa na familia zimeundwa, anafanya awezavyo kuzivuruga. Anashambulia kila kitu ambacho ni kitakatifu kuhusu ujinsia wa binadamu, akiurarua kutoka kwa muktadha wa ndoa kwa mfufulizo usio na mwisho wa mawazo na vitendo vichafu. Hutafuta kuwashawishi wanaume na wanawake kwamba vipaumbele vya ndoa na familia vinaweza kupuuzwa au kutelekezwa, au kuwa kipaumbele cha chini ya kazi, mafanikio mengine, na utafutaji wa “kujiridhisha mwenyewe” na uhuru wa mtu binafsi. Kwa hakika adui anapendezwa wakati wazazi wanapopuuza kuwafundisha na kuwafunza watoto wao kuwa na imani katika Kristo, kupata uongofu, na kuzaliwa tena kiroho. Ndugu na kina dada, mambo mengi ni mazuri, mengi ni muhimu, lakini ni machache tu yaliyo muhimu.
Kutangaza kweli za kimsingi zinazohusiana na ndoa na familia si kupuuza au kudhoofisha dhabihu na ufanisi wa wale ambao ndoa na familia si uhalisi wa sasa. Wengine wenu mnakana baraka ya ndoa kwa sababu zinazojumuisha kukosa wenzi wastahiki, mvuto wa jinsia moja, mapungufu ya kimwili au kiakili, au kwa kawaida hofu ya kushindwa kwamba, kwa wakati huu, hukinzana na imani. Au huenda kuwa ulifunga ndoa, lakini ndoa ikavunjika, na ukaachwa peke yako kusimamia kile wawili wakiwa pamoja hawawezi kukistahimili. Wengine wenu ambao mmeoana na hamwezi kupata watoto licha ya hamu na maombi ya kusihi.
Hata hivyo, kila mmoja ana vipawa; kila mmoja ana talanta; kila mmoja anaweza kuchangia katika kufungua mpango wa kiungu katika kika kizazi. Mengi ambayo ni mazuri, mengi ambayo ni muhimu---hata wakati mwingine yote yaliyo muhimu kwa sasa---yanaweza kupatikana ni chini ya kiwango cha hali maridhawa. Wengi wenu mnafanya vyema mwezavyo. Na wakati ninyi mnaobeba mizigo mizito ya maisha ya duniani mnasimama kwa utetezi wa Mpango wa Mungu wa kuinua watoto Wake, sisi sote tu tayari kuwahimili. Kwa imani tunashuhudia kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo umeshatangulia na, hatimaye, utafidia mafadhaiko na hasara kwa wale ambao wanamgeukia Yeye. Hakuna aliyepangiwa mapema kupokea kidogo kuliko kile chote Baba alichonacho kwa ajili ya watoto Wake.
Mama mmoja kijana majuzi alinidokezea kuhusu hofu yake kuhusu mapungufu katika huu wito muhimu. Nilihisi kwamba mambo yaliyokuwa yanamsumbua yalikuwa madogo na hakuwa na haja kuwa na wasiwasi; alikuwa anaendelea vyema. Lakini mimi nilijua kwamba alikuwa anataka kumfurahisha Mungu na kuheshimu uthamini Wake. Nilimpatia maneno ya kutia moyo, na katika moyo wangu nilimsihi Mungu, Baba yake wa Mbinguni, aweze kumwinua kwa upendo Wake na ushahidi wa kibali Chake anapotekeleza kazi Yake.
Haya ndiyo maombi yangu kwetu sote hivi leo. Na tuweze kila mmoja kupata idhinisho machoni Yake. Na ndoa zishamiri na familia zifanikiwe, na hata kama kudra yetu ni ujalivu wa baraka hizi katika maisha ya dunia, au la, na neema za Bwana zilete furaha sasa na imani katika ahadi za hakika zipatikane. Katika jina la Yesu Kristo, amina.