2010–2019
Nyimbo Zinazoimbwa na Zisizoimbwa
Aprili 2017


14:34

Nyimbo Zinazoimbwa na Zisizoimbwa

Lakini ninamwomba kila mmoja wetu kubaki na kudumu kwa dhati katika kwaya.

“Kuna mwanga wa jua katika nafsi yangu leo ” Eliza Hewitt aliandika, “mtukufu na angavu kuliko mianga kwenya anga yoyote duniani, kwani Yesu ni nuru yangu.”1 Kwa furaha katika kila noti, wimbo huu wa zamani wa Kikristo ni vigumu kuuimba bila kutabasamu. Lakini leo ningependa kutoa kutoka kwenye muktadha mstari mmoja kutoka humo ambao unaweza kusaidia katika siku ambazo tunaona vigumu kuimba au kutabasamu na “nyakati za furaha ya amani” hazionekani “kuendelea.” Kama kwa wakati fulani unashindwa kuimba nyimbo mpya za furaha unazozisikia kutoka kwa wengine, ninawaomba kushikamana kwenye mstari katika wimbo huu ambao unatuhakikishia, “Yesu anayesikiliza anaweza kusikia nyimbo ambazo [ninyi] hamuwezi kuimba.”2

Miongoni mwa kweli tunazokumbana nazo kama watoto wa Mungu tuishio katika ulimwengu ulioanguka ni kwamba baadhi ya siku ni ngumu, siku ambazo imani yetu na ustahilimilivu wetu unajaribiwa. Changamoto hizi zaweza kuja kwa ukosefu wetu, ukosefu wa wengine, au ukosefu katika maisha, lakini kwa sababu yoyote ile, tunaona inaweza kutuibia nyimbo tunazotaka kuimba na kutia giza ahadi ya “majira ya kuchipua [katika] nafsi”3 ambayo Eliza Hewitt anafurahia katika mojawapo ya mistari yake.

Hivyo tunafanyaje katika nyakati kama hizo? Jambo moja ni, tunafuata ushauri wa Mtume Paulo na “kama tunatumaini kile [ambacho] hatujakiona … [na] tunakingojea kwa uvumilivu.”4 Katika nyakati hizo wakati tuni ya furaha inagugumia chini ya uwezo wetu wa kunena, tunaweza kusimama kimya kwa muda na kuwasikiliza wengine, tukipata nguvu kutoka kwa utukufu wa muziki unaotuzunguka. Wengi wetu ambao “tuna changamoto kimuziki” kujiamini kwetu kumeimarishwa na uimbaji wetu ukaboreka kwa kujiweka wenyewe karibu na mtu ambaye ana sauti nzuri. Hakika inafuata kwamba katika kuimba nyimbo za milele, tunatakiwa kusimama kama iwezekanavyo kwa binadamu karibu Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu—ambaye ana sauti nzuri. Kisha tunajipa moyo kutoka kwa uwezo Wake wa kusikia ukimya wetu na tunakuwa na matumaini kutokana na maombezi Yake ya kimasihi kwa ajili yetu. Ukweli ni “wakati Bwana yu karibu” kwamba “yule njiwa wa amani anaimba katika moyo wangu [na] maua ya neema ya kuonekana.”5

Katika siku zile ambazo tunahisi kupotoka kidogo kwa tuni, kuliko vile tuvyofikiria tunaona au kusikia wengine, ningetaka kuwaomba, hususani vijana wa Kanisa, kukumbuka ni kwa mpango mtakatifu ambao siyo sauti zote katika kwaya ya Mungu ni sawa. Inachukua mchanganyiko—sauti ya kwanza na ya pili, ya tatu na besi—kuufanya muziki kuwa mzuri. Kuazima mstari kutoka mawasiliano ya furaha ya wanawake wawili wa ajabu wa Siku za Mwisho, “Viumbe wote wa Mungu wana nafasi ndani ya kwaya.”6 Wakati tunaposhusha hadhi yetu ya upekee wetu au kujaribu kukubali uainishaji wa uongo—uainishaji unaotokana na utamaduni wa uteja usiyotosheka na kufanya udhanifu kuliko inavyowezekana na mitandao ya kijamii—tunapoteza utajiri wa sauti na sifa ya sauti ambayo Mungu ameiweka wakati aliumba ulimwengu wa anuwai.

Hii siyo kusema kwamba kila mtu katika kibwagizo hiki anaweza kuanza kupaza sauti yake ya ufasaha! Utofauti wa sauti siyo kelele, na kwaya zinahitaji nidhamu—kwa ajili ya malengo yetu leo, naomba niseme ufuasi—lakini baada ya kukubali mashairi matakatifu yaliyofunuliwa na okestra tamu iliyotungwa kabla kuumbwa kwa ulimwengu, Baba yetu wa Mbinguni anafurahi kutuona sisi tunaimba kwa sauti zetu wenyewe, siyo sauti ya mtu mwingine. Jiamini mwenyewe, na mwamini Yeye. Usidharau thamani yako au kukebehi mchango wako. Juu ya yote, usiache jukumu lako katika kibwagizo. Kwa Nini? Kwa sababu wewe ni wa kipekee na usiyo na kifani. Kuipoteza hata sauti moja kunapunguza uwezo wa waimbaji wengine katika kwaya yetu ya dunia, pamoja na kuwapoteza wale ambao wanajiona wapo pembeni mwa jamii au pembeni mwa Kanisa.

Japo ninawahimiza ninyi nyote kuwa na imani kuhusu nyimbo ambazo zinaweza kuwa ngumu kuimba, ninatambua kwamba kwa sababu tofauti mimi ninasumbuka na aina nyingine za nyimbo ambazo zilitakiwa kuimbwa—lakini—hazijaimbwa

Wakati ninapoona kutokuwa na usawa kwa kiasi kikubwa katika uchumi ulimwenguni, ninahisi kuwa na hatia kuimba pamoja na Bi. Hewitt wimbo “kwa baraka ambazo [Mungu] hunipa sasa na shangwe zilizowekwa huko juu.”7 Kibwagizo hicho hakiwezi kuimbwa kwa ukamilifu hadi tuwe tumewajali maskini kwa heshima. Mdororo wa kiuchumi ni laana ambayo inaendelea, mwaka hadi mwaka na kizazi hadi kizazi. Huharibu mwili, hulemaza roho, huumiza familia, na kuangamiza ndoto. Kama tungeweza kufanya zaidi ili kupunguza makali wa umaskini, kama Yesu alivyorudia kutuamuru sisi kutenda, huenda baadhi ya wasiojiweza kiuchumi katika ulimwengu waweze kugumia wimbo wa “Kuna Mwanga wa Jua katika Nafsi Yangu Leo,” labda kwa mara ya kwanza katika maisha yao.

Pia ninaona vigumu kuimba maneno ya uchangamfu, wimbo wa mdundo, wakati wengi miongoni mwetu wana matatizo ya kiakili na kimawazo au matatizo mengine ya kiafya. Kwa bahati mbaya, mizigo hii wakati mwingine inaendelea licha ya juhudi nyingi nzuri za wasaidizi, ikijumuisha wanafamilia. Ninaomba tusiwaache watoto hawa wa Mungu wateseke kimya kimya na kwamba tutajaliwa na uwezo Wake wa kusikia nyimbo ambazo hawawezi kuziimba sasa.

Na siku moja ninatumaini kibwagizo kizuri cha ulimwengu wote kitaimbwa katika jamii na makabila yote, kikitangaza kwamba bunduki, kashfa, na kejeli siyo njia ya kupambana na matatizo ya mwanadamu. Matangazo ya mbinguni yanapaza sauti kwetu kwamba njia pekee ambayo matatizo tata ya kijamii yanaweza kutatuliwa kamwe ni kwa kumpenda Mungu na kutii amri Zake, hivyo kufungua mlango ule wa milele, njia ya wokovu ya kupendana sisi kwa sisi kama majirani. Nabii Etheri alifundisha kwamba lazima “tutumainia ulimwengu bora.” Tukisoma wazo hilo miaka elfu baadaye, Moroni aliyechoshwa na vita na vurugu alitangaza kwamba “njia mzuri zaidi” kwa ulimwengu huo mara zote itakuwa injili ya Yesu Kristo.8

Tunashukuru kiasi gani kwamba miongoni mwa changamoto hizi unakuja, muda hadi muda, aina nyingine ya wimbo ambao tunashindwa kuuimba, lakini kwa sababu tofauti. Hii ni wakati hisia hizi ni za kina sana na binafsi, na hata takatifu sana, kwamba haziwezi au hazipaswi kuonyeshwa—kama upendo wa Cordelia kwa baba yake, ambaye alisema, “Upendo wangu … ni mkubwa kuliko ulimi wangu. … siwezi kuinua moyo wangu kwenda mdomoni kwangu.”9 Unakuja kwetu kama kitu kitakatifu, hisia hizi hazielezeki—hazisimuliki kiroho—kama maombi yaliyotolewa na Yesu kwa ajili ya watoto Wanefi. Wale waliokuwa mashahidi kwa tukio walisema:

“Jicho halijaona, wala sikio kusikia, … vitu vikubwa na vya ajabu vile tulivyoona na kusikia Yesu akisema kwa Baba; 

Hakuna ulimi unaoweza kusema, wala haiwezi kuandikwa na mtu yeyote, wala mioyo ya watu haiwezi kufikiria vitu vikubwa na vya ajabu kama tulivyoona na kusikia Yesu akisema.10

Nyakati za utakaso kama hizi zitabaki hazionekani kwa sababu uonyesho, hata ingewezekana, ingeonekana kama kufuru.

Akina kaka na dada, tunaishi katika ulimwengu wa mauti tukiwa na nyimbo nyingi tusizoweza au ambazo bado hatujaimba. Lakini nawaombeni kila mmoja wetu kudumu na kuwa mwaminifu kwenye kwaya, ambapo tutaweza kuonja milele ule wimbo mzuri kati ya zote—“wimbo wa ukombozi wa upendo.”11 Kwa bahati nzuri, viti kwa ajili ya wimbo huu havina hesabu. Kuna nafasi kwa wale wanaoongea lugha tofauti, wanaosherehekea utamadumu tofauti, na kuishi katika maeneo yao. Kuna nafasi kwa waseja, kwa waliooa au kuolewa, familia kubwa, na wasiokuwa na watoto. Kuna nafasi kwa wale ambao zamani walikuwa na maswali juu ya imani yao na nafasi kwa wale ambao bado wanayo. Kuna nafasi kwa wale wenye kuvutiwa tofauti kijinsia. Kwa kifupi , kuna nafasi kwa kila mtu anayempenda Mungu na kuheshimu amri Zake kama kipimo cha fimbo kisichokiukwa kwa ajili ya tabia binafsi, kwani kama upendo wa Mungu ni tuni ya wimbo wetu, hakika jitihada zetu za kumtii Yeye sharti ziwe za amani. Pamoja na masharti ya Mungu ya upendo na amani, toba na huruma, uaminifu na msamaha, kuna nafasi katika kwaya hii kwa wote ambao wanatamani kujiunga12 “Njooni kama mlivyo,” Baba mwenye upendo anasema kwa kila mmoja wetu, Yeye anaongezea, “Lakini usipange kubakia vile ulivyo.” Tunatabasamu na kukumbuka kwamba Mungu ana nia ya kutufanya tuwe zaidi ya tunavyofikiria tungekuwa.

Katika huu mpangilio wa muziki ambao ni mpango Wake kwa wokovu wetu, naomba kwa unyenyekevu tufuate kifimbo Chake na kuendelea kuimba nyimbo tusizoweza kuimba, hadi tuweze kuimba kwa Mfalme [wetu].”13 Kisha siku moja, kama wimbo tuupendao unavyosema:

“Tutaimba na kupaza sauti na majeshi ya mbinguni,

Hosanna, hosanna kwa Mungu na kwa mwana Kondoo! …

… Na Yesu akishuka na gari la moto!”14

Ninashuhudia siku hiyo itakuja, kwamba Mungu Baba wa Milele kwa mara nyingine atamtuma Mwana Wake wa Pekee, wakati huu kutawala kama Mfalme wa Wafalme milele. Ninashuhudia kwamba hili ni Kanisa Lake la urejesho na ni gari la kuleta mafundisho na ibada za kuokoa za injili Yake kwa kila mwanadamu. Wakati ujumbe Wake “utakuwa umepenya kila bara [na] kutembelea kila kijiji,”15 Yesu hakika “[ataonyesha] uso wake wa tabasamu,”16 Patakuwa na mwanga jua wa milele kwenye nafsi siku hiyo. Kwa ajili ya siku hiyo iliyoahidiwa, ninaomba kwa hamu, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. “There Is Sunshine in My Soul Today,” Hymns, no. 227.

  2. Hymns, no. 227.

  3. Hymns, no. 227.

  4. Warumi 8:25.

  5. Hymns, no. 227.

  6. Bill Staines, “All God’s Critters Got a Place in the Choir,” in Laurel Thatcher Ulrich and Emma Lou Thayne, All God’s Critters Got a Place in the Choir (1995), 4.

  7. Hymns, no. 227.

  8. Ona Ether 12:4, 11.

  9. William Shakespeare, King Lear, act 1, scene 1, lines 79–80, 93–94.

  10. 3 Nefi 5:16–17; mkazo umeongezewa.

  11. Alma 5:26; see also Alma 26:13.

  12. Ona 2 Nefi 2633.

  13. Hymns, no. 227.

  14. “The Spirit of God,” Hymns, no. 2.

  15. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 142.

  16. Hymns, no. 227.