Ukweli Halisi, Mafundisho Halisi na Ufunuo Halisi
Tafadhali fanyeni mkutano huu kuwa muda wa kusherehekea katika jumbe kutoka kwa Bwana kupitia watumishi Wake.
Akina kaka na dada zangu wapendwa, karibuni kwenye mkutano mkuu! Ni shangwe iliyoje kuwa pamoja nanyi! Mmekuwa kwenye mawazo yangu takribani muda wote katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Nimesali kuhusu ninyi na kwa ajili yenu. Katika wiki za karibuni nimesali kwa dhati kwamba mkutano huu utakuwa ni muda wa ufunuo na kutafakari kwa ajili ya wote watafutao baraka hizo.
Tunafurahi kuongea nanyi kutoka katika Kituo cha Mikutano kwa mara nyingine. Nafasi nyingi ziko wazi, lakini uwepo wa baadhi ya washiriki wa Kwaya ya Tabernacle ni hatua muhimu ya kusonga mbele. Tunawakaribisheni nyote katika mkutano huu kwa njia ya mtandao, popote mlipo.
Bado tunakabiliana na makali ya UVIKO-19 na mabadiliko yake. Tunawashukuru kwa kufuata ushauri wetu na ushauri wa wataalamu wa afya na viongozi wa serikali katika jamii zenu wenyewe.
Kila mkutano mkuu tunaouitisha unaongozwa na Bwana.1 Mfumo umebadilika kwa miaka mingi sasa. Nilipokuwa mdogo sana, mkutano ulichukua siku tatu au nne. Baadaye, siku zilipunguzwa mpaka siku mbili. Kila ujumbe—kipindi hicho na sasa—ni matokeo ya maombi ya dhati na maadalizi mengi ya kiroho.
Wakuu wenye Mamlaka na Maofisa Wakuu wa Kanisa watakaoongea watafokasi jumbe zao kwa Mwokozi wetu, Yesu Kristo, rehema Yake na nguvu Yake isiyo na mwisho ya kuokoa. Hakujawahi kuwepo na kipindi kama cha sasa katika historia ya ulimwengu ambapo maarifa ya Mwokozi wetu ni ya msingi na muhimu sana kibinafsi kwa kila nafsi ya mwanadamu. Fikiria jinsi mapigano ya uharibifu ulimwenguni kote—na yale katika maisha yetu binafsi—yatatatuliwa kwa haraka kama sisi sote tukichagua kumfuata Yesu Kristo na kusikiliza mafundisho Yake.
Katika roho hiyo, ninawaalikeni kusikiliza vitu vitatu wakati wa mkutano huu: ukweli halisi, injili halisi ya Kristo na ufunuo halisi. Kinyume na mashaka ya baadhi yenu kuna kitu kama hicho cha ukweli na uongo. Kweli kuna ukweli halisi—ukweli wa milele. Mojawapo wa majanga ya siku yetu ni kwamba watu wachache wanajua wapi pa kugeukia kwa ajili ya ukweli.2 Nawahakikishieni kwamba mtakachokisia leo na kesho kinabeba ukweli halisi.
Injili halisi ya Kristo ina nguvu. Inabadilisha maisha ya kila mtu ambaye anaielewa na kutafuta kuitenda katika maisha yake. Injili ya Kristo hutusaidia kupata na kubakia kwenye njia ya agano. Kubakia kwenye njia hiyo nyembamba lakini iliyo na mpangilio hatimaye kutatuwezesha kupokea vitu vyote alivyonayo Mungu.3 Hakuna chenye thamani zaidi ya vyote alivyonavyo Baba yetu!
Hatimaye, ufunuo halisi kwa ajili ya maswali ndani ya moyo wako utafanya mkutano huu kuwa wenye thawabu na usiosahaulika. Kama bado hujatafuta kuhudumiwa na Roho Mtakatifu ili akusaidie kusikia kile Bwana angetaka ninyi msikie katika siku hizi mbili, nawaalika kufanya hivyo sasa. Tafadhali fanyeni mkutano huu kuwa muda wa kusherehekea katika jumbe kutoka kwa Bwana kupitia watumishi Wake. Jifunzeni jinsi ya kutumia jumbe hizo maishani mwenu.
Hili ni Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Sisi ni watoto Wake wa agano. Bwana alitangaza kwamba ataharakisha kazi Yake katika muda wake,4 na Anafanya hivyo katika hatua kubwa zaidi. Tunayo fursa ya kushiriki katika kazi Yake Takatifu.
Natamka baraka juu ya wale watafutao nuru, maarifa na ukweli zaidi. Ninatoa upendo wangu kwa kila mmoja wenu, katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.