Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu
Akina kaka na dada, sasa itakuwa ni heshima kwangu kuwawasilisha kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu wa Kanisa kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.
Tunawaomba kwamba tafadhali muoneshe kukubali kwenu katika njia ya kawaida, popote mlipo. Kama kuna wale wanaopinga mapendekezo yoyote, tunaomba kwamba muwasiliane na rais wenu wa kigingi.
Inapendekezwa kwamba tumkubali Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Dallin Harris Oaks kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.
Wale wanaounga mkono, waoneshe.
Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonesha.
Inapendekezwa kwamba tumkubali Dallin H. Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na Jeffrey R. Holland kama Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.
Wale wanaounga mkono, tafadhali onesheni.
Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.
Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: Jeffrey R. Holland, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, Dale G. Renlund, Gerrit W. Gong, Ulisses Soares na Patrick Kearon.
Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.
Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.
Inapendekezwa kwamba tuwakubali washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji na wafunuzi.
Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.
Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.
Tunawapeni taarifa kwamba Sabini wa Maeneo wapya sita walikubaliwa wakati wa mikutano mikuu ya uongozi iliyofanyika Alhamisi, Oktoba 4, na baadaye walitangazwa kwenye tovuti ya Kanisa. Tunawaalikeni muwakubali ndugu hawa katika majukumu yao mapya.
Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.
Yeyote anayepinga, kwa ishara hiyo hiyo.
Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi wengine Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa wakuu kama ilivyo sasa.
Wanaounga mkono, tafadhali onesheni kwa kuinua mkono.
Wale wanaopinga, ikiwa kuna yeyote.
Tunawashukuru, akina kaka na dada kwa imani na sala zenu endelevu kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.
Mabadiliko kwa Sabini wa Eneo
Sabini wa Eneo wafuatao waliidhinishwa wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika kama sehemu ya mkutano mkuu:
Miguel A. Avila, Jean Pierre A. L. Haboko, Ramiro Ibarra Sanchez, George Katembo Njogu Munene, A. Enrique Texeira, Francisco Villanueva Rojas.