Mkutano Mkuu
Ishi Kulingana na Haki Zako
Mkutano mkuu wa Oktoba 2024


11:46

Ishi Kulingana na Haki Zako

Jifunze jinsi ibada za ukuhani na ahadi za maagano, zitakavyoruhusu nguvu za Mungu kutiririkia katika maisha yako.

Hivi karibuni mume wangu, Greg, alipokea majibu ya uchunguzi kwamba atahitaji upasuaji mkubwa na miezi mingi ya tibakemikali. Kama wengi wenu ambao mmekabiliwa na hali kama hiyo, mara moja tulianza kusali kuomba msaada wa mbinguni na nguvu za Mungu. Jumapili iliyofuatia upasuaji wa Greg, sakramenti ililetwa kwenye chumba chetu cha hospitali.

Kwenye tukio hili, mimi nilikuwa mtu pekee niliyepokea sakramenti. Kipande kimoja cha mkate. Kikombe kimoja cha maji. Kanisani, akili yangu hufokasi kwenye mfumo wa kutoa sakramenti—kujiandaa, kubariki, na kupitisha. Lakini mchana huo, nilitafakari kipawa cha nguvu za Mungu kikipatikana kwangu kupitia ibada takatifu zenyewe na ahadi ya agano niliyokuwa nikifanya nikitwaa kipande cha mkate na kile kikombe cha maji. Huu ulikuwa wakati nilihitaji nguvu kutoka mbinguni. Katikati ya mvunjiko mkubwa wa moyo, uchovu, na kukosa uhakika, nilishangaa kuhusu kipawa hiki ambacho kingeniruhusu kuvuta nguvu kutoka Kwake ambazo nilizihitaji sana. Kushiriki sakramenti kungeongeza wenza wangu na Roho wa Bwana, akiniruhusu kuvuta kutoka kwenye kipawa cha nguvu za Mungu, ikijumuisha kuhudumiwa na malaika na nguvu ya Mwokozi iwezeshayo kushinda.

Sidhani kama hapo kabla niliwahi kuwa na utambuzi huu wa wazi kwamba kitu muhimu si tu kuhusu mtu anayehudumu kwenye sakramenti—ni ibada gani na ahadi yetu ya agano huleta pia hustahili fokasi ya usikivu wangu. Ibada za ukuhani na ahadi za maagano humruhusu Mungu kututakasa sisi na kisha kufanya maajabu katika maisha yetu. Lakini hii inatokeaje?

Kwanza, ili ibada idhihirishe nguvu ya Mungu katika maisha yetu, lazima ifanyike kwa mamlaka kutoka kwa Mwana wa Mungu. Mfumo wa utolewaji ni muhimu. Baba alimkabidhi Yesu Kristo funguo na mamlaka ili kusimamia utolewaji wa ibada za ukuhani Wake. Chini ya maelekezo Yake, ndani ya utaratibu wa ukuhani Wake, wana wa Mungu wametawazwa ili kusimama mahali pa Mwana wa Mungu.

Pili, sisi hatuweki tu ahadi za kimaagano—ni lazima tuyashike. Katika ibada nyingi za injili, sisi tunafanya maagano matakatifu na Mungu; Yeye anaahidi kutubariki tunaposhika maagano hayo. Je, tunatambua ni muunganiko wa ibada za ukuhani pamoja na kushika ahadi za maagano ndicho huturuhusu kufikia nguvu za Mungu?

Mchana ule nilijiuliza kama mimi, binti wa agano wa Mungu, nilielewa kwa ukamilifu jinsi ya kufikia kipawa cha nguvu ya Mungu kupitia ibada za ukuhani na ikiwa kweli ninatambua jinsi nguvu za Mungu hufanya kazi ndani yangu.

Mnamo 2019 mwaliko wa kinabii ulitolewa kwa wanawake wa Kanisa, ukitufundisha jinsi gani ya kuvuta nguvu za Mwokozi katika maisha yetu. Rais Russell M. Nelson alitualika tujifunze Mafundisho na Maagano 25, ufunuo uliotolewa kwa Emma Smith huko Harmony, Pennsylvania. Kukubali mwaliko huo kumebadilisha maisha yangu.

Mwezi uliopita nilipata fursa nisiyoitarajia ya kutembelea Harmony. Huko, chini ya miti ya maple, ukuhani ulirejeshwa kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery. Karibu na miti hiyo ni mlango wa mbele wa nyumba ya Joseph na Emma. Upande wa pili kutoka mahali pa tanuru ya kupasha nyumba joto kuna dirisha. Nilisimama kwenye dirisha lile na kujiuliza jinsi Emma angehisi wakati akiangalia nje kwenye miti.

Mnamo Julai ya mwaka 1830, Emma alikuwa na umri wa miaka 26; alikuwa bado mdogo sana. Alikuwa na miaka mitatu na nusu ndani ya ndoa yake. Alikuwa amepoteza mtoto mchanga wa kiume—wa kwanza. Kaburi lake dogo liko karibu na barabara ya kutoka nyumbani kwake. Nikiwa nimesimama katika dirisha lile, haikuwa vigumu kwangu kufikiria nini kilijaza mawazo yake. Hakika alikuwa na wasiwasi kuhusu kipato chao, kuhusu ongezeko la mateso ambayo yalitishia usalama wao, kuhusu siku zao za baadaye. Na bado kazi ya Mungu ilikuwa kila mahali kumzunguka. je, alijiuliza pia kuhusu nafasi yake katika mpango, dhumuni lake katika ufalme wa Mungu, na uwezekano wake katika macho ya Mungu?

Nadhani aliwaza hayo.

Upande wa pili tu wa barabara, kipawa cha Mungu cha mamlaka na funguo za ukuhani zilikuwa zimerejeshwa duniani. Huu ulikuwa wakati ambapo Emma kwa kweli alihitaji nguvu kutoka mbinguni. Katikati ya mvunjiko mkubwa wa moyo, uchovu, na kukosa uhakika, ninavuta taswira ya Emma akijiuliza kuhusu kipawa hiki cha ukuhani wa Mungu ambacho kingeweza kufungua nguvu kutoka kwa Mungu ambazo alizihitaji sana.

Lakini Emma hakuwa tu amesimama kwenye dirisha lile akijiuliza.

Wakati Nabii Joseph alipokuwa akifunzwa juu ya funguo, ofisi, ibada na jinsi ya kusaidia katika huduma za ukuhani, Bwana Mwenyewe, kupitia nabii Wake, alimpatia Emma ufunuo. Si ufunuo kwa rais-Emma wa Muungano wa Usaidizi wa Nauvoo—ufunuo huu ulitolewa kwa Emma akiwa umri wa miaka 26 huko Harmony. Kupitia ufunuo huo, Emma angejifunza kuhusu utakaso wa ndani kwa ndani na muunganiko kupitia agano ambao ungeongeza ufanyaji kazi wa ibada hizo za kikuhani maishani mwake.

Kwanza, Bwana alimkumbusha Emma juu ya mahali pake katika mpango Wake, ikijumuisha yeye alikuwa nani na alikuwa wa nani—binti katika ufalme Wake. Alialikwa “kutembea katika njia za wema,” njia ambayo ilijumuisha ibada ambazo zingefungua nguvu za Mungu kama Emma angeshikilia kwenye maagano yake.

Pili, katika majira Yake ya kuomboleza kwa kina, Bwana alimpa dhumuni lake. Emma siyo tu alikuwa na kiti cha mstari wa mbele katika Urejesho, yeye alikuwa mshiriki muhimu katika kazi iliyokuwa ikifanyika. Angesimikwa “ili kuelezea maandiko, na kushawishi Kanisa.” Muda wake “ungetolewa ili kuandika na kujifunza mengi.” Emma alipewa kazi takatifu ili kusaidia kuwaandaa Watakatifu katika kuabudu; nyimbo zao kwa Bwana zingepokelewa kama sala na “zilijibiwa kwa baraka juu ya vichwa vyao.”

Mwisho, Bwana alitoa muhtasari wa mchakato wa utakaso wa ndani kwa ndani ambao ungemwandaa Emma kwa ajili ya kuinuliwa. “Isipokuwa umefanya hili,” Bwana alimweleza, “mahali nilipo wewe huwezi kuja.”

Kama tutaisoma sehemu ya 25 kwa uangalifu, tunagundua upigaji hatua muhimu ukifanyika. Emma angepiga hatua kutoka kuwa binti katika ufalme hadi “mwanamke mteule” hadi malkia. Ibada za Ukuhani wa Haruni na Melkizedeki zikiunganika na ushikaji ahadi zake za maagano, zingeongeza kwake ushirika wa Roho na malaika, zikimpa nguvu kuongoza maisha yake kwa mwongozo wa kiungu. Kupitia nguvu za kiungu, Mungu angeuponya moyo wake, kuongeza uwezo wake, na kumbadilisha kuwa toleo lake bora ambalo Yeye alijua angeweza kuwa. Na kupitia ibada za Ukuhani wa Melkizedeki, “nguvu za uchamungu [zingedhihirika] ” katika maisha yake, na Bwana angefungua pazia ili aweze kupokea uelewa kutoka Kwake. Hiki ndicho kinachoonekana kama nguvu za Bwana kufanya kazi ndani yetu.

Rais Russell M. Nelson alifundisha:

Kila kitu ambacho kilitokea katika [Harmony] kina uhusiano mkubwa kwenye maisha yenu. Urejesho wa ukuhani, pamoja na ushauri wa Bwana kwa Emma, vinaweza kumuongoza na kumbariki kila mmoja wenu. …

“… Kufikia nguvu za Bwana katika maisha yako kunahitaji vitu sawa na hivyo ambavyo Bwana alimwelekeza Emma na kila mmoja wetu kuvifanya.”

Kulikuwa na mambo muhimu yaliyokuwa yakitokea katika pande zote mbili za dirisha lile huko Harmony, ikijumuisha ufunuo uliotolewa kwa mwanamke mteule ambaye Bwana alimuita—ufunuo ambao ungeimarisha, kutia moyo, na kumwelekeza Emma Smith, binti wa Mungu.

Wakati Isabelle mjukuu wetu wa kike alipopewa jina na kubarikiwa, baba yake alimbariki kuwa na uelewa juu ya ukuhani; kwamba angeendelea kukua na kujifunza kuhusu baraka ambazo zingeletwa nao katika maisha yake; na kwamba imani yake katika ukuhani ingekua kadiri alivyoendelea kukua katika uelewa.

Si kawaida kwa msichana mdogo kupewa baraka ya kuelewa ukuhani na kujifunza jinsi gani ibada hizo za ukuhani na ahadi za maagano zitamsaidia yeye kufikia nguvu za Mungu. Lakini nilimkumbuka Emma na kuwaza, Kwa nini isiwe hivyo? Binti huyu mdogo kabisa ana uwezekano wa kuwa mwanamke mteule katika ufalme Wake na hatimaye kuwa malkia. Kupitia ibada za ukuhani Zake na utiifu wa ahadi za ukuhani, nguvu za Mungu zitafanya kazi katika yeye na kupitia yeye ili kushinda chochote kiletwacho na maisha na kuwa mwanamke Mungu ajuaye anaweza kuwa. Hiki ndicho kitu ninachotaka kila msichana katika ufalme aelewe.

“Ishi kulingana na haki zako.”

Jifunze jinsi ibada za ukuhani na ahadi za maagano, vitakavyoruhusu nguvu za Mungu kutiririkia katika maisha yako kwa ufanisi mkubwa, zikifanya kazi ndani yako na kupitia wewe, zikikuwezesha na kukuandaa kufikia dhumuni na uwezekano wako mkamilifu.

Kwa uangalifu jifunze na utafakari juu ya ibada za Ukuhani wa Haruni na Mekizedeki, ahadi za maagano tunayoweka na kila ukuhani na nguvu za Mungu tunazozifikia kupitia ibada hizo.

Kumbuka si muhimu tu kuhusu mtu anayehudumu kwenye ibada; lakini pia kitu ambacho ibada na ahadi ya maagano kinaungua pia kinastahili fokasi ya usikivu wako.

Kula mkate na kunywa maji ni ukumbusho wa kila wiki juu ya nguvu Zake zikifanya kazi ndani yako ili kukusaidia kushinda. Uvaaji wa gamenti ya ukuhani mtakatifu ni ukumbusho wa kila siku juu ya nguvu Zake kufanya kazi ndani yako ili kukusaidia uwe na nguvu.

Sisi sote tunayo njia ya kufikia kipawa cha nguvu za Mungu.

Kila wakati tunaposhiriki sakramenti.

Kila wakati tunapoingia hekaluni.

Hili ni angazio la Sabato yangu. Hii ndiyo kwa nini ninapenda kibali changu cha hekaluni.

“Katika ibada zake, nguvu za uchamungu hudhihirika.”

Juu ya kipawa hiki, ninatoa ushahidi katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Mafundisho na Maagano 107:20.

  2. Mzee D. Todd Christofferson alifundisha: “Katika ibada zote, hususani zile za hekaluni, tunapata endaumenti kwa nguvu kutoka juu. Nguvu ‘hii ya uchamungu’ huja ndani ya mtu na kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu. … Ninashuhudia kwamba Mungu atatimiza ahadi Zake kwako kadiri unavyoheshimu maagano yako na Yeye. … Yeye, kupitia Roho Mtakatifu, atakujaza nguvu za kiungu” (”Nguvu za Maagano,” Liahona, Mei 2009).

  3. Dallin H. Oaks, “Ukuhani wa Haruni na Sakramenti,” Liahona, Nov. 1999, 45

  4. “Kila mwanamume na kila mwanamke ambaye anashiriki katika ibada za ukuhani na ambaye anafanya na kushika maagano na Mungu anao ufikiaji wa moja kwa moja kwenye nguvu za Mungu” (Russell M. Nelson, “Agano Lisilo na Mwisho,” Liahona, Nov. 2022, 10).

  5. Ona Yoshua 3:5, tanbihi a. Mzee Dale G. Renlund alielezea: Kupitia maagano haya, tuna ufikiaji mkubwa wa nguvu ya Bwana. Ili kuwa wazi, maagano ya ubatizo na ya hekaluni, siyo ndani yake au kwa yenyewe, chanzo cha nguvu. Chanzo cha nguvu ni Bwana Yesu Kristo na Baba yetu wa Mbinguni. Kufanya na kushika maagano hujenga njia kwa ajili ya nguvu Zao katika maisha yetu.” (“(Muunganiko Wenye Nguvu, Mtakatifu wa Mafundisho ya Kristo,” Liahona, Mei 2024, 82.)

  6. Ona Mafundisho na Maagano 107:1–3; Tafsiri ya Joseph Smith, Waebrania 7:3; katika kiambatisho cha BibliaAlma 13:2. Rais Dallin H. Oaks alifundisha: “Kutoka kwenye maandiko sisi pia tunajua kwamba wale wanaohudumu katika tendo la ukuhani wanatenda kwa niaba ya Bwana (ona Mafundisho na Maagano 1:38; 36:2). Sasa nitapendekeza jinsi walimu na makuhani na mashemasi wanavyopaswa kutimiza majukumu yao ya kutenda kwa niaba ya Bwana katika kuandaa, kuhudumia na kupitisha sakramenti” (“The Aaronic Priesthood and the Sacrament,” Ensign, Nov. 1999, 45).

  7. Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 3.5. 1–2, Maktaba ya Injili.

  8. Ona Mafundisho na Maagano 107:18–20; Wafilipi 1:6.

  9. Ona Russell M. Nelson, “Hazina za Kiroho,” Liahona, Nov. 2019, 77.

  10. Ona “Joseph and Emma Smith’s Home” (ChurchofJesusChrist.org) kwa maelezo zaidi kuhusu utengenezaji mpya wa nyumba ya Smith kwenye eneo la Kanisa la kihistoria huko Harmony, Pennsylvania.

  11. Mamlaka na funguo za ukuhani zinaruhusu nguvu za Mungu kutiririka katika maisha ya wale wanaopokea ibada za ukuhani na kufanya na kutii maagano yaliyohusiana na mamlaka na funguo hizo” (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 3.5, Maktaba ya Injili).

  12. Ona Joseph Smith—Historia 1:71, muhtasari.

  13. Ona Mafundisho na Maagano 25.

  14. Ona Mafundisho na Maagano 25:1.

  15. Mafundisho na Maagano 25:2.

  16. Ona Mafundisho na Maagano 25:13. “Neno agano ni la asili ya Kilatini, con venire, na linamaanisha ‘kuja pamoja.’ Katika muktadha wa ukuhani, ‘agano ni kuja pamoja au makubaliano baina ya Mugu na Mwanadamu. Inadhaniwa kwamba Mungu na mwanadamu wanakuja pmoja ili kufanya mkataba, ili kukubaliana juu ya ahadi, masharti, haki, na wajibu. …

    “Agano lililofanywa katika njia hii haliondolewi na halibadiliki. Iinaitegemeza nafsi; linatengeneza msingi imara na usiotingishika kwa matarajio ya siku za baadaye” (Dale G. Renlund na Ruth Lybbert Renlund, Ukuhani wa Melkizedeki: Kuelewa Mafundisho, Kuishi Kanuni [2018], 60).

  17. Mafundisho na Maagano 25:7.

  18. Mafundisho na Maagano 25:8.

  19. Mafundisho na Maagano 25:12.

  20. Ona Mafundisho na Maagano 25:15.

  21. Mafundisho na Maagano 25:15. Rais Dallini H. Oaks alifundisha: “Ibada ya ubatizo na maagano yake husika ni vigezo vinavyohitajika ili kuingia katika ufalme wa selestia. Ibada na maagano yanayohusika ya hekaluni ni vigezo vinavyohitajika kwa ajili ya kuinuliwa katika ufalme wa selestia, ambao ni uzima wa milele, ‘Zawadi ya Mungu iliyo kuu kuliko zote’ [Mafundisho na Maagano 14:7]” (“Maagano na Wajibu,” Liahona, Mei 2024, 96).

  22. Ona Mafundisho na Maagano 25:1.

  23. Mafundisho na Maagano 25:3.

  24. Ona Mafundisho na Maagano 25:15.

  25. Ona Dallin H. Oaks, “Ukuhani wa Haruni na Sakramenti,” Ensign, Nov. 1999, 44 Rais Nelson alifundisha:

    “Katika njia inayohusiana kwa karibu, ibada hizi za Ukuhani wa Haruni pia ni muhimu kwa kuhudumiwa na malaika. …

    “… Jumbe za malaika zinaweza kutolewa kwa sauti ama tu kwa mawazo ama hisia zikiwasilishwa akilini” (“The Aaronic Priesthood and the Sacrament,” Liahona, Jan. 1999, 44, 45)

    Kwa kuongezea, Nabii Joseph Smith alitoa ahadi hii wakati akizungumza na kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama: “Kama mtaishi kulingana na haki zenu, malaika hawawezi kuzuiwa kuwa washirika wenu”(Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith [2011], 454).

  26. Ona Mafundisho na Maagano 84:19–20.

  27. Ona Mafundisho na Maagano 107:18–19.

  28. Russell M. Nelson, “Hazina za Kiroho,” 77. “Willard Richards alisema: Rais Joseph Smith alisoma ufunuo [uliotolewa] kwa Emma Smith … na kusema kwamba … si yeye pekee, bali wengine pia, wanaweza kupata baraka sawa na hizo” (Mafundisho: Joseph Smith, 453–54). Ona pia Nauvoo Relief Society Minute Book, March 17, 1842, in Jill Mulvay Derr and others, eds., katika The First Fifty Years of Relief Society: Key Documents in Latter-day Saint Women’s History (2016), 1.2.1, churchhistorianspress.org.

  29. Ona Mafundisho na Maagano 24, kichwa cha habari cha sehemu. Hii inasema kwamba “mafunuo matatu yanayofuta yalitolewa wakati huu ili kuimarisha, kutia moyo, na kuelekeza.

  30. Mafundisho: Joseph Smith, 454.

  31. Ona Russell M. Nelson, “Hazina za Kiroho,” 77. Ninawasihi mjifunze kwa sala kweli zote mnazoweza kupata kuhusu nguvu ya ukuhani. Unaweza kuanza na Mafundisho na Maagano 84 na 107. Sehemu hizo zitawaongoza kwenye vifungu vingine. Maandiko na mafundisho ya manabii, waonaji, na wafunuzi wa siku hizi yamejaa kweli hizi. Pale ufahamu wenu unapoongezeka na pale mnapofanyia kazi imani katika Bwana na nguvu Yake ya ukuhani, uwezo wenu wa kuleta hazina hii ya kiroho ambayo Bwana amefanya ipatikane utaongezeka (Russell M. Nelson, “Hazina Kiroho,” 79).

  32. Ona Mafundisho na Maagano 109:22.

  33. Mafundisho na Maagano 84:20.