Mkutano Mkuu
Wapendwa wa Mungu
Mkutano mkuu wa Oktoba 2024


10:31

Wapendwa wa Mungu

Kujazwa na upendo wa Mungu hutukinga dhidi ya dhoruba za maisha lakini pia hufanya nyakati za furaha kuwa za furaha zaidi.

Kabla sijaanza, ninapaswa niwaambie kwamba watoto wangu wawili walizimia wakati wakizungumza kwenye mimbari, na sijawahi kuhisi kuunganika na wao zaidi kuliko wakati huu. Nina mengi mawazoni mwangu zaidi ya mlango mdogo wa kutorokea.

Familia yetu ina watoto sita ambao wakati mwingine hutaniana kwamba wao ni mtoto mpendwa. Kila mmoja ana sababu tofauti za kupendelewa. Upendo wetu kwa kila mmoja kwa watoto wetu ni safi na unaridhisha na kamili. Hatukuweza kumpenda yeyote kati yao zaidi ya mwingine—kwa kuzaliwa kwa kila mtoto kulileta upanuzi mzuri zaidi wa upendo wetu. Ninahisi zaidi upendo wa Baba yangu wa Mbinguni kwangu kupitia upendo ambao ninauhisi kwa watoto wangu.

Kila mmoja anaporuduia rudia madai ya kuwa mtoto anayependwa zaidi, unaweza kuwa umefikiria kwamba familia yetu haijawahi kuwa na chumba cha kulala ambacho hakijapangika. Hisia ya dosari kwenye uhusiano kati ya mzazi na mtoto hupungua ukifokasi kwenye upendo.

Wakati fulani, labda kwa sababu ninaweza kuona kwamba tunaelekea kwenye vurugu za familia zisizoepukika, nitasema kitu kama “SAWA, mmenichosha, lakini sitatangaza; mnajua ni nani ni kipenzi changu.” Lengo langu ni kwamba kila mmojawapo wa hawa sita anahisi mshindi na vita vyote kuepukwa—angalau mpaka wakati mwingine!

Katika Injili yake, Yohana alijielezea kama mwanafunzi “ambaye Yesu alimpenda,” kana kwamba hicho kilikuwa kitu cha kipekee. Napenda kufikiri kwamba ilikuwa hivyo kwa sababu Yohana alihisi kupendwa kikamilifu na Yesu. Nefi alinipa maana kama hiyo alipoandika, “Ninamfurahia Yesu wangu”. Bila shaka, Mwokozi sio wa Nefi zaidi kuliko wa Yohana, hatahivyo uhusiano binafsi wa Nefi na Yesu “wake” ulimsababisha kuelezea hivyo.

Je, haishangazi kwamba kuna nyakati tunaweza kuhisi binafsi kutambulika na kupendwa kikamilifu? Nefi anaweza kumwita Yeye Yesu “wake” nasi pia tunaweza. Upendo wa Mwokozi wetu ni “upendo wa hali ya juu, wenye hadhi, wenye nguvu,” na Yeye huutoa mpaka “tujazwe.” Upendo wa kitukufu kamwe haukauki, na kila mmoja wetu anapendwa na kufurahiwa. Upendo wa Mungu, ni kama maduara yanayoshabihiana, sisi sote tunashabihiana. Sehemu yetu yoyote inayoonekana tofauti, kwenye upendo Wake ndipo tunapopata umoja.

Je, ni ya kushangaza kwamba amri kuu ni kumpenda Mungu na kuwapenda wale wanaotuzunguka? Ninapoona watu wakionyesha upendo kama wa Kristo wao kwa wao, huonekana kwangu kana kwamba upendo huo si tu hubeba upendo wao ni upendo ambao pia una uungu ndani yake. Tunapopendana kwa njia hii, kwa yote na kikamilifu kadiri tuwezavyo, mbingu huhusika pia.

Kwa hivyo ikiwa mtu tunayemjali anaonekana kuwa mbali na hisia ya upendo wa kiungu, tunaweza kufuata mfano huu—kwa kufanya mambo ambayo yanatuleta karibu na Mungu sisi wenyewe na kisha kufanya mambo ambayo yanatuleta karibu nao—ishara ya kimya kimya ya kusogea kwa Kristo.

Natamani ningeweza kukaa chini na wewe na kukuuliza ni hali gani zinazokufanya uhisi upendo wa Mungu. Ni mistari gani ya maandiko, ambayo ni vitendo dhahiri vya huduma? Je, Ungekuwa wapi? Ni, muziki gani? Ni katika uwepo wa nani? Mkutano Mkuu ni mahali pazuri pa kujifunza kuhusu kuungana na upendo wa kimbingu.

Lakini pengine unahisi kuwa mbali na upendo wa Mungu. pengine kuna sauti za kukukatisha tamaa na kutia kiza ambazo zinajaza mawazo yako, jumbe zikikuambia kwamba umejeruhiwa na kukanganywa sana, mdhaifu sana na asiyejaliwa, wa utofauti sana au asiye na mpangilio ili kupata upendo wa kimbingu katika njia yoyote dhahiri. Ikiwa unasikia mawazo hayo, basi tafadhali sikia hili: sauti hizo ni za uongo. Kiujasiri tunaweza kutojali uvunjikaji wa aina yoyote ile ambao hutufanya kutostahili upendo wa kimbingu—kila mara tunapoimba wimbo ambao unatukumbusha kwamba Mwokozi wetu mpendwa na asiye na dosari alichagua “kuchubuliwa, kuvunjwa, [na] kuchanwa kwa ajili yetu,” kila mara tunaposhiriki mkate uliomegwa. Hakika Yesu hoondoa aibu yote kutoka waliovunjwa. Kupitia kuvunjika Kwake, Yeye akawa mkamilifu, na Yeye anaweza kutufanya tuwe wakamilifu licha ya kuvunjika kwetu. Akiwa amevunjika, mpweke, aliyechanwa, na kuchubuliwa—nasi tunaweza kuhisi hivyo—lakini kutengwa na upendo wa Mungu, haitokuwa hivyo kwetu. “Watu waliovunjika, upendo kamili,” kama wimbo unavyoimba.

Unaweza kujua kitu cha siri kuhusu wewe mwenyewe ambacho kinakufanya uhisi kuwa haupendeki. Vyovyote vile unavyoweza kuwa sahihi kuhusu kile unachojua kukuhusu wewe mwenyewe, unakosea kufikiri kwamba umejiweka mbali na upendo wa Mungu. Wakati mwingine sisi ni wakatili na tusio na subira kwetu wenyewe kwa njia ambazo hatungeweza kamwe kufikiria tumekuwa kwa mtu mwingine yeyote. Kuna mengi ya kufanya katika maisha haya, lakini kujilaumu na aibu ya kujihukumu hayapo kwenye orodha hii. Iwe kwa chochote sisi tunaweza kuhisi kwamba tuko hivyo, mikono Yake haijafupishwa. Hapana. Daima ni mirefu vya kutosha “[kufikia] pale tulipo” na kumkumbatia kila mmoja wetu.

Wakati hatuhisi joto la upendo wa kiungu, upendo huo haujaondoka. Maneno ya Mungu mwenyewe ni kwamba “milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; lakini wema wake hautaondoka kwetu.” Kwa hiyo, ili kufafanua vyema, wazo kwamba Mungu ameacha kupenda linapaswa kuwa chini sana kwenye orodha ya maelezo yanayoweza kutolewa kwenye maisha ambayo hatuwezi kuyafikia mpaka milima ikiondoka na vilima kutokweka!

Ninafurahia sana ishara hii ya milima kuwa ushahidi wa uhakika wa upendo wa Mungu. Ishara hiyo yenye nguvu inaingia katika simulizi za wale wanaoenda milimani kupokea ufunuo na maelezo ya Isaya ya “mlima wa nyumba ya Bwana” “kuwekwa juu ya milima.” Nyumba ya Bwana ni nyumba ya maagano yetu ya thamani sana na mahali pa sisi sote kukimbilia na kuzama kwa kina katika ushahidi wa upendo wa Baba yetu kwetu. Pia nimefurahia faraja inayokuja kwenye nafsi yangu wakati ninapojifunga kwa nguvu zaidi katika agano langu la ubatizo na kumpata mtu ambaye anaomboleza au anayehuzunishwa kwa kukatishwa tamaa na kujaribu kuwasaidia wao kushikilia na kuchakata hisia zao. Je, hizi ni njia ambazo tunaweza kujikita zaidi katika upendo wa thamani wa agano uitwao hesed?

Basi ikiwa upendo wa Mungu hautuachi, kwa nini tusiuhisi wakati wote? Ili kukidhi tu matarajio yako: Mimi sijui. Lakini kuwa mwenye kupendwa kwa hakika siyo sawa na kuhisi kupendwa, na nina mawazo machache ambayo yanaweza kukusaidia unapofuatilia majibu yako ya swali hilo.

Labda unapambana na huzuni, mfadhaiko, usaliti, upweke, kukata tamaa au mambo mengine yenye nguvu kwenye uwezo wako wa kuhisi upendo wa Mungu kwako. Ikiwa ndivyo, mambo haya yanaweza kufifisha au kusimamisha uwezo wetu wa kuhisi upendo huo hali ya kuwa tungetakiwa kuuhisi. Angalau kwa kipindi kifupi, pengine hutaweza kuhisi upendo Wake, na uelewa unapaswa kutosha. Lakini najiuliza kama ungeweza kupata uzoefu—kwa uvumilivu—kupitia njia tofauti tofauti za kuonyesha na kupokea upendo wa kiungu. Je, unaweza kupiga hatua kurudi nyuma kutoka kwenye chochote kilicho mbele yako na labda hatua nyingine na nyingine, mpaka uone uwanda mpana, mpana na mpana zaidi kama itahitajika, mpaka uweze “kufikiria selestia” kwa sababu unaangalia nyota na kukumbuka dunia zisizo na idadi na kupitia kwazo Muumba wao?

Sauti za ndege, kuhisi joto au upepo au mvua kwenye ngozi yangu, na nyakati ambapo asili huweka hisia zangu kwenye mshangao juu ya Mungu—kila kimoja kimekuwa na sehemu katika kunipa uhusiano wa kimbingu. Pengine faraja ya marafiki waaminifu itasaidia. Pengine muziki? Au kuhudumu? Je, umeweka kumbukumbu au kuandika shajara wakati uhusiano wako na Mungu ulikuwa dhahiri zaidi kwako? Labda ungeweza kuwaalika wale unaowaamini kushiriki na wewe vyanzo vyao vya uhusiano wa kiungu unapotafuta msaada na uelewa.

Ninajiuliza, ikiwa Yesu angechagua mahali ambapo wewe na Yeye mngeweza kukutana, mahali pa faragha ambapo mngeweza kuwa na mtazamo wa umoja juu Yake, je, angeweza kuchagua mahali pako pa kipekee pa mateso binafsi, mahali pa hitaji lako la kina, ambapo hakuna mtu mwingine anayeweza kwenda? Mahali fulani unapohisi upweke sana kwamba lazima uwe peke yako lakini si hivyo, mahali ambapo labda tu Yeye amepitia lakini tayari amejiandaa kukutana nawe unapowasili? Kama unamsubiri Yeye aje, pengine tayari yupo huko na anaweza kufikiwa?

Ikiwa unahisi kujazwa na upendo katika kipindi hiki cha maisha yako, tafadhali jaribu na shikilia hilo kwa ufanisi kama chujio lishikiliavyo maji. Sambaza kila mahali unapoenda. Mojawapo ya miujiza ya mambo ya kiungu ni kwamba tunapojaribu kushiriki upendo wa Yesu, tunajikuta tukijazwa katika aina mbali mbali za kanuni kwamba “yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata.”

Kujazwa na upendo wa Mungu hutukinga dhidi ya dhoruba za maisha lakini pia hufanya nyakati za furaha kuwa na furaha zaidi—siku zetu za shangwe, wakati kuna jua angani, zinafanywa kuwa angavu zaidi kupitia uchangamfu katika nafsi zetu.

Acha “tukite mizizi na kuwa imara” katika Yesu wetu na upendo Wake. Hebu tutafute na tuthamini uzoefu wa kuhisi upendo Wake na nguvu Zake katika maisha yetu. Shangwe ya injili inapatikana kwa wote: si tu kwa wenye furaha, si tu kwa walioanguka. Shangwe ni lengo letu, si matokeo ya hali zetu. Tuna kila sababu nzuri ya “kufurahi na kujazwa na upendo kwa Mungu na watu wote.” Acha tujazwe. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Yohana 21:20; ona pia Yohana 13:23; 19:26; 20:2; 21:7.

  2. 2 Nefi 33:6; msisitizo umeongezwa.

  3. Kamusi ya Biblia, “Hisani

  4. Kwenye Nchi Takatifu: Mathayo 14:15–20. Na katika bara za Amerika: 3 Nefi 27:16.

  5. Ona Mathayo 22:35–40.

  6. Ona 1 Yohana 4:12.

  7. Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi huanisha kwamba tunahitaji “kuwasaidia [wengine] kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni kupitia [sisi]” ([2022], 12).

  8. “Yesu, Mkombozi, Kristo, Bwana,” Nyimbo za Dini, na. 98; ona pia Isaya 53:5; Matthayo 26:26.

  9. Rais Russell M. Nelson alielezea: “Kabla ya kusulubiwa kwa [Mwokozi], Yeye alisema kwamba katika siku ya tatu nitakamilika’ [Luka 13:32; msisitizo umeongezwa]. Fikiria kuhusu hilo! Bwana asiye na dhambi, asiye na makosa—akiwa tayari amekamilika kulingana na viwango vyetu vya duniani—alitangaza hali Yake ya ukamilifu ambayo ingekuja baadae. Ukamilifu Wake wa milele ungefuatia baada ya ufufuko wake na upokeaji wa nguvu zote … mbinguni na duniani’ [Mathayo 28:18; ona pia Mafundisho na Maagano 93:2–23]” (“Perfection Pending,” Ensign, Nov. 1995, 87). Nabii Moroni aliwaalika wote “njoo kwa Kristo na mkamilishwe ndani yake, na mjinyime ubaya wote; na ikiwa mtajinyima ubaya wote, na kumpenda Mungu na mioyo yenu, akili na nguvu zenu zote, basi neema yake inawatosha, kwamba kwa neema yake mngekamilishwa katika Kristo” (Moroni 10:32).

  10. “Savior of My Soul,” 2024 Youth Album, ChurchofJesusChrist.org.

  11. Ona Isaya 59:1.

  12. “Iwapi Amani?” Nyimbo za Dini, no.62

  13. Isaya 54:10.

  14. Kwa mfano, Nefi (ona 1 Nefi 17:7), Musa (ona Kutoka 19:3), wanafunzi kumi na moja (ona Mathayo 28:16), na Mwokozi (ona Mathayo14:23)ona pia Zaburi 24:3.

  15. Isaya 2:2; ona pia mstari wa 3. Mfano huu wa lugha ya picha hunifanya kutafakari zaidi kuhusu malengo ya Bwana kwenye kuleta mamia ya mahekalu kwa ajili ya watoto Wake kote ulimwenguni.

  16. Uzoefu wangu unashuhudia ukweli wa ahadi ya Rais Nelson kwamba mahali salama zaidi pa kuishi ni ndani ya maagano yetu ya hekaluni (ona “Hekalu na Msingi Wako wa Kiroho,” Liahona, Nov. 2021, 96).

  17. Rais Nelson ametuhakikishia:

    “Muda hekaluni kutakusaidia ufikirie selestia na uelewe wewe ni nani hasa, unaweza kuwa nani na aina ya maisha ambayo unaweza kuwa nayo milele. Kuabudu hekaluni mara kwa mara kutadumisha jinsi unavyojiona na jinsi ulivyo sehemu ya mpango mtukufu wa Mungu. Ninakuahidi hilo. …

    “… Hakuna kitakachoipa faraja zaidi roho yako nyakati za maumivu. Hakuna kitakachofungua mbingu zaidi. Hakuna!” (“Furahia katika Zawadi ya Funguo za Ukuhani,” Liahona, Mei 2024, 121, 122).

  18. Ona Mosia 18:8–10, 13. “Agano la ubatizo ni ushuhuda wa wazi kwa Baba wa Mbinguni wa ahadi tatu maalum: kumtumikia Mungu, kushika amri zake, na kuwa tayari kuchukua juu yetu jina la Yesu Kristo. Vipengele vingine ambavyo mara nyingi vinahusishwa na agano la ubatizo—kwamba ‘tunabebeana mizigo ya kila mmoja,’ ‘kuomboleza pamoja na wale wanaoomboleza,’ na ‘kuwafariji wale wanaohitaji faraja’ (Mosia 18:8–9)—ni matunda ya kufanya agano badala ya sehemu ya agano lenyewe. Vipengele hivi ni muhimu kwa sababu ni kile ambacho nafsi iliyoongoka ingefanya kwa kawaida” (Dale G. Renlund, “Stronger and Closer Connection to God through Multiple Covenants” [Brigham Young University devotional, Mar. 5, 2024], speeches.byu.edu).

  19. Ona Russell M. Nelson, “Agano Lisilo na Mwisho,” Liahona, Okt. 2022, 4–11.

  20. Ona Russell M. Nelson, “Fikiria Selestia!,” Liahona, Nov. 2023, 117, 118.

  21. Mathayo 16:25.

  22. Waefeso 3:17

  23. Ona 2 Nefi 2:25; Russell M. Nelson, “Shangwe na Kunusurika Kiroho,” Liahona,, Nov. 2016, 81–84.

  24. Mosia 2:4.

  25. Ona Moroni 7:48.