Kutafuta Majibu ya Maswali ya Kiroho
Maswali yetu ya dhati ya injili yanaweza kutoa fursa kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kutusaidia tukue.
Najua hili linaweza kushangaza, lakini nimekua vya kutosha kukumbuka wakati tulipofunzwa shuleni kwamba kulikuwa na sayari tisa katika mfumo wa jua. Moja ya sayari hizo, Pluto, ilipewa jina lake na Vetenia Burney mwenye miaka 11 wa Oxford, Uingereza, baada ya ugunduzi wake mnamo 1930. Na hadi kufikia 1992, Pluto iliaminika kuwa sayari ya mbali zaidi katika mfumo wa jua. Katika kipindi hiki, ilikuwa kawaida kupata mifano ya maumbo ya karatasi ya umbali wa sayari katika madarasa na maonesho ya sayansi, kila moja ikionesha nafasi ya Pluto kwenye mpaka unaojulikana. Wanasayansi wengi waliamini kwamba zaidi ya ukingo huo mfumo wa nje wa jua ulikuwa na nafasi tupu.
Hata hivyo, swali la muda mrefu lilibaki katika jamii ya wanasayansi kuhusiana na chanzo cha aina fulani ya kimondo ambacho wanajimu walikifuatilia mara kwa mara. Na swali hilo liliendelea kwa miongo kabla ya ugunduzi wa eneo jingine la mbali la mfumo wetu wa jua. Kwa ufahamu wenye ukomo waliokuwa nao, wanasayansi walitumia miongo hiyo ya mwingiliano kuzalisha maendeleo muhimu ya kiteknolojia ambayo yaliruhusu mafunzo na utafiti zaidi. Hatma ya ugunduzi wao ilisanidi ukanda wetu wa kisayari na kuleta matokeo ya Pluto kuwekwa kwenye eneo hili jipya la anga na mfumo wetu wa jua ukijumuisha sayari nane.
Mwanasayansi mmoja maarufu na mchunguzi mkuu kwa ajili ya misheni ya Ukanda Mpya wa anga aliyepewa jukumu la kuitafiti Pluto kwa ukaribu alikuwa na hili la kusema kuhusu uzoefu huu: “Tulidhani tulielewa jiografia ya mfumo wetu wa jua. Hatukuelewa. Tulidhani tulielewa idadi ya sayari katika mfumo wetu wa jua. Na hatukuwa sahihi.”
Kinachovuta umakini wangu kuhusu kipindi hiki cha ugunduzi wa kihistoria wa anga ni baadhi ya mifanano na utofauti muhimu kati ya utafutaji wa kisitiari wa ukanda mpana wa kisayansi na safari ambayo sisi, kama watoto wa Mungu, tunaifanya ili kutafuta majibu ya maswali yetu ya kiroho. Kwa upekee, jinsi tunavyoweza kushughulikia vizuizi vya uelewa wetu wa kiroho na kujitayarisha kwa hatua inayofuata ya ukuaji binafsi—na wapi tunageukia kwa ajili ya msaada.
Mstari juu ya Mstari
Kuuliza maswali na kutafuta maana ni sehemu ya asili na ya kawaida ya uzoefu wetu wa maisha. Kuna nyakati, kutokuwa na majibu kamili kunaweza kutuleta kwenye ukingo wa uelewa wetu, na vikwazo hivyo vinaweza kuleta hisia za hasira au za kuchosha. Cha kushangaza, mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yetu sote umekusudiwa kutusaidia tupige hatua licha ya vikwazo na kufikia kile tusichoweza kufikia peke yetu, hata bila ufahamu kamili wa mambo yote. Mpango wa Mungu ni wa rehema kwa vizuizi vya ubinadamu wetu; unatupatia Mwokozi wetu, Yesu Kristo, kuwa Mchungaji wetu Mwema; na kutupatia msukumo wa kutumia haki yetu ya kujiamulia kumchagua Yeye.
Mzee Dieter F. Uchtdorf amefundisha kwamba “kuuliza maswali si ishara ya udhaifu,” badala yake “ni mwanzo wa ukuaji.” Akizungumza moja kwa moja kuhusu juhudi zetu binafsi kama watafutaji wa ukweli, nabii wetu, Rais Russell M. Nelson, amefundisha kwamba lazima tuwe na “nia ya dhati” na “tuombe kwa moyo wa kweli [na] kusudi halisi, tukiwa na imani katika [Yesu] Kristo.” Amefundisha zaidi kwamba “‘kusudi halisi’ humaanisha kwamba mtu anakusudia kwa dhati kufuata mwongozo wa kiungu unaotolewa.”
Juhudi zetu binafsi za kukua katika hekima zinaweza kutuongoza kwenye kutathmini maswali yetu, magumu au vinginevyo, kupitia lenzi ya chanzo na madhara, tukitafuta na kutambua mipangilio na kisha kuunda masimulizi ili kuupa umbo uelewa wetu na kujaza nafasi wazi katika maarifa. Tunapozingatia utafutaji wetu wa maarifa ya kiroho, hata hivyo, michakato hii muhimu inaweza kuwa wakati mwingine yenye msaada lakini ikiwa peke yake inaweza kuwa haijakamilika pale tunapotazama ili kujua vitu vinavyohusiana na Baba wa Mbinguni na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, injili Yao, Kanisa Lao, na mpango Wao kwetu sote.
Njia ya Mungu Baba na Mwanaye ya kutupatia hekima Yao huwekea kipaumbele kualika nguvu ya Roho Mtakatifu kuwa mwalimu wetu binafsi pale tunapomweka Yesu Kristo kuwa kiini katika maisha yetu na katika utafutaji wetu wa dhati wa majibu Yao na maana Yao. Wanatualika tuutambue ukweli kupitia muda uliotengwa kujifunza maandiko matakatifu na kutafuta ukweli wa siku za mwisho uliofunuliwa kwa ajili ya siku yetu na wakati wetu, uliotolewa na manabii na mitume wa siku za leo. Wanatusihi tutumie muda mwingi, wa kuabudu ndani ya nyumba ya Bwana na kupiga magoti katika sala “ili kufikia taarifa kutoka mbinguni.” Ahadi ya Yesu kwa wale waliokuwepo kusikia Mahubiri Yake Mlimani ni ya kweli katika siku yetu kama ilivyokuwa wakati wa huduma Yake duniani: “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtaona; bisheni nanyi mtafunguliwa.” Mwokozi wetu anahakikisha kwamba “Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao.”
Njia ya Bwana ya kufundisha ni “mstari juu ya mstari, kanuni juu ya kanuni.” Tunaweza kuhitajika “kumngojea Bwana” katika nafasi kati ya mstari wetu wa sasa wa uelewa na ujao ambao bado haujatolewa. Nafasi hii takatifu inaweza kuwa mahala ambapo hali yetu kubwa zaidi ya kiroho inaweza kutokea—mahala ambapo tunaweza “kuvumilia kwa subira” utafutaji wetu wa dhati na kufanya upya nguvu yetu ya kuendelea kutii ahadi takatifu tulizozifanya kwa Mungu kupitia agano.
Uhusiano wetu wa agano pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo unaashiria uraia wetu wa kudumu katika ufalme wa Mungu. Na ukaaji wetu huko huhitaji kuyaoanisha maisha yetu kwenye kanuni za kiungu na kuweka juhudi ya kukua kiroho.
Utiifu
Kanuni moja ya msingi inayofunzwa kote katika Kitabu cha Mormoni ni wakati watoto wa Mungu wanapochagua kuonesha utiifu na kushika maagano yao, wanapokea mwongozo na maelekezo endelevu ya kiroho. Bwana ametuambia kwamba kupitia utiifu wetu na bidii, tunaweza kupata maarifa na akili. Sheria na amri za Mungu hazijakusudiwa kuwa vikwazo katika maisha yetu bali njia yenye nguvu kuelekea ufunuo na elimu binafsi ya kiroho. Rais Nelson amefundisha ukweli muhimu kwamba “ufunuo kutoka kwa Mungu mara zote umeunganishwa kwenye sheria yake ya milele” na zaidi kwamba “kamwe haukinzani na mafundisho Yake.” Utiifu wako wa hiari kwa amri za Mungu, licha ya kutokuwa na maarifa kamili ya sababu Zake, unakuweka kwenye kombania ya manabii Wake. Musa 5 inatufunza kuhusu mchangamano fulani kati ya Adamu na malaika wa Bwana.
Baada ya Bwana kuwapa Adamu na Hawa “amri, kwamba wamwabudu Bwana Mungu wao, na wamtolee wazao wa kwanza wa mifugo yao, kwa ajili ya sadaka kwa Bwana,” maandiko yanasema kwamba “Adamu akawa mtiifu kwa amri za Bwana.” Tunaendelea kusoma kwamba “baada ya siku nyingi malaika wa Bwana akamtokea Adamu, akisema: Kwa nini wamtolea Bwana dhabihu? Na Adamu akasema: Mimi sijui, ila Bwana ameniamuru.”
Utiifu wa Adamu ulitangulia uelewa wake na ulimuandaa yeye kupokea maarifa matakatifu kwamba alikuwa akishiriki katika ishara takatifu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Utiifu wetu wa unyenyekevu, vile vile, utachonga njia kwa ajili ya uelewa wetu wa kiroho wa njia za Mungu na lengo Lake la kiungu kwa ajili ya kila mmoja wetu. Kupambana ili kuinua utiifu wetu hutuleta karibu na Mwokozi wetu Yesu Kristo, kwa sababu utiifu wa sheria na amri Zake ni matokeo ya kumfikia Yeye.
Kama nyongeza, uaminifu wetu kwenye maarifa na hekima tuliyorithi tayari kupitia utiifu wa kanuni za injili na maagano matakatifu ni maandalizi muhimu kwa ajili ya utayari wetu wa kupokea na kuwa mawakala wa mawasiliano kutoka kwa Roho Mtakatifu.
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ni chanzo cha ukweli wote na wanashiriki hekima Yao kwa ukarimu. Pia, kuelewa kwamba hatupati maarifa yoyote binafsi pasipo Mungu inaweza kutusaidia tujue nani wa kumgeukia na wapi pa kuweka msingi wa tumaini letu.
Tumaini Kuu
Hadithi ya Agano la Kale ya Naamani, kiongozi wa jeshi ambaye aliponywa ukoma na nabii Elisha, ndiyo hasa hadithi yangu pendwa. Hadithi inaelezea jinsi imani imara ya “mjakazi mdogo” ilivyogeuza hatma ya maisha ya mtu mmoja na, kwa waaminio wote, ilifunua mfiko wa rehema ya Mungu kwa wale wanaoweka tumaini Kwake na kwa nabii Wake. Japo hakutajwa jina, binti huyu mdogo pia alisaidia kusukuma uelewa wetu mbele. Na imani ya Naamani kwenye ushuhuda wa binti ilimsukuma kupeleka ombi lake kwa ajili ya uponyaji kwa mtumishi mteule wa Mungu.
Mwitikio wa Naamani kwa maelekezo ya nabii Elisha ya kuoga ndani ya mto Yordani mwanzo ulikuwa wa mashaka na wa kuudhi. Lakini mwaliko wa yeye kuwa mtiifu kwenye ushauri wa nabii ulifanya njia kwa ajili ya uponyaji na uelewa wake mkubwa kwamba Mungu ni halisi.
Tunaweza kukuta kwamba baadhi ya maombi yetu ya kiroho yana majibu ya sababu zinazojulikana na huenda yasilete usumbufu muhimu kwetu. Au, kama vile Naamani, tunaweza kukuta kwamba mahitaji mengine yana changamoto na yanaweza kuleta hisia ngumu na nzito ndani yetu. Au, sawa na maelezo ya hitimisho la mwanzo la wanajimu kuhusu mfumo wetu wa jua, katika kutafuta kwetu ukweli wa kiroho, tunaweza kufikia ufafanuzi usio sahihi sana ikiwa tutategemea uelewa wetu wenyewe wenye ukomo, matokeo ya huzuni na yasiyotarajiwa ambayo yanaweza kutuongoza mbali kutoka kwenye njia ya agano. Na zaidi, baadhi ya maswali yanaweza kuendelea hadi pale Mungu, mwenye “uwezo wote” na “hekima yote, na uelewa wote,” ambaye “anaelewa vitu vyote” katika rehema Yake, hutoa uelewa kupitia uaminifu wetu kwa jina Lake.
Onyo moja muhimu kutoka hadithi ya Naamani ni kwamba kutokuwa mtiifu kwenye sheria na amri za Mungu kunaweza kuchukua muda mrefu au kuchelewesha ukuaji wetu. Tumebarikiwa kuwa na Yesu Kristo kama Mponyaji wetu Mkuu. Utiifu wetu kwenye sheria na amri za Mungu unaweza kufungua njia kwa ajili ya Mwokozi wetu kutoa uelewa na uponyaji anaojua tunauhitaji, kulingana na mpango Wake wa tiba uliopendekezwa kwetu.
Mzee Richard G. Scott alifundisha kwamba “maisha haya ni uzoefu katika tumaini kubwa—tumaini katika Yesu Kristo, tumaini katika mafundisho Yake, tumaini katika uwezo wetu kama tunavyoongozwa na Roho Mtakatifu kutii mafundisho hayo kwa furaha sasa na kwa maisha yenye malengo, yenye furaha halisi ya kuwepo milele yote. Kutumaini kunamaanisha kutii kwa hiari bila kujua mwisho kutokea mwanzo (ona Mithali 3:5–7). Ili kuzaa matunda, tumaini lako kwa Bwana ni lazima liwe na nguvu na lenye kudumu kuliko ujasiri wako kwenye hisia na uzoefu wako binafsi.”
Mzee Scott anaendelea: “Kuonesha imani ni kutumaini kwamba Bwana anajua kile anachokifanya kwako na kwamba anaweza kukikamilisha kwa faida yako ya milele hata kama huwezi kuelewa jinsi Yeye anavyoweza kukikamilisha.”
Ushuhuda wa Hitimisho
Marafiki wapendwa, ninashuhudia kwamba maswali ya dhati ya injili yanaweza kutoa fursa kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kutusaidia tukue. Juhudi yangu binafsi ya kutafuta majibu kutoka kwa Bwana kwa maswali yangu binafsi ya kiroho—yaliyopita na ya sasa—imeniruhusu kutumia nafasi kati ya uelewa wangu na wa Mungu ili kufanyia kazi utiifu Kwake na uaminifu kwenye maarifa ya kiroho ambayo ninayo sasa.
Ninashuhudia kwamba kuweka tumaini lako kwa Baba wa Mbinguni na kwa manabii Wake, aliowatuma, kutakusaidia kuinuka kiroho na kukusukuma mbele kuelekea uwanda mpana wa Mungu. Mtazamo wako utabadilika kwa sababu wewe utabadilika. Mungu anajua kwamba kadiri unavyokuwa juu, ndivyo unavyoweza kuona mbali zaidi. Mwokozi wetu anakualika upande juu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.