Mkutano mkuu wa Oktoba 2024 Kikao cha Jumamosi Asubuhi Kikao cha Jumamosi AsubuhiKikao cha Jumamosi Asubuhi cha Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa 194 wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kinachofanyika Oktoba 5–6, 2024. Henry B. EyringKuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa WakuuRais Eyring anawasilisha Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu kwa ajili ya kura ya kuwakubali. Neil L. AndersenUshindi wa TumainiMzee Andersen anafundisha kwamba tunapokuwa na tumaini katika Kristo na na kumtumainia Yeye, tutaweza kuhisi amani Yake. Emily Belle FreemanIshi Kulingana na Haki ZakoRais Freeman anawahimiza wanawake na wasichana kujifunza jinsi ibada za ukuhani na ahadi za agano zinaruhusu nguvu za Mungu katika maisha yao, kuwasaidia wao kufikia uwezekano wao. Karl D. HirstWapendwa wa MunguMzee Hirst anafundisha namna ya kuhisi upendo mtakatifu wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Dale G. Renlund“Hii Ni Injili Yangu”—“Hili Ni Kanisa Langu”Mzee Renlund anafundisha kwamba muunganiko wa injili ya Mwokozi na Kanisa la Mwokozi unatupatia kufikia nguvu za Mungu na kutusaidia kuwa watakatifu. David P. HomerKumwamini Baba YetuMzee Homer anafundisha kwamba tunapokea baraka wakati tunapomwamini Mungu na kufuata amri Zake. Gregorio E. CasillasMungu Anawapenda Watoto Wake WoteMzee Casillas anafundisha kwamba tunaweza kubariki maisha ya watoto wa Mungu kupitia utumishi na uanafunzi. Dallin H. OaksKumfuata KristoRais Oaks anafundisha umuhimu wa kufuata amri za Yesu Kristo, akisisitiza amri Yake ya kuepukana na ubishi. Kikao cha Jumamosi Mchana Kikao cha Jumamosi MchanaKikao cha Jumamosi Mchana cha Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa 194 wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kinachofanyika Oktoba 5–6, 2024. D. Todd ChristoffersonKuzika Silaha Zetu za UasiMzee Christofferson anatuhimiza kuzika dalili yoyote ya uasi dhidi ya Mungu katika maisha yetu, iwe ni kutotii amri Zake kwa makusudi au kupuuza mapenzi Yake kimyakimya. José A. TeixeiraKuunganishwa kwa Yesu Kristo: Kuwa Chumvi ya DuniaMzee Teixeira anafundisha njia nne rahisi lakini zenye nguvu tunazoweza kubaki tukiwa tumeunganishwa kwa Yesu Kristo. Juan Pablo VillarMkono Wake Uko Tayari KutusaidiaMzee Villar anafundisha kwamba Mwokozi daima yupo pale kutusaidia kushinda changamoto yoyote ikiwa tuna imani katika Yeye. Patrick KearonKaribuni kwenye Kanisa lenye ShangweMzee Kearon anafundisha kuhusu shangwe ambayo inaweza kupatikana katika Kanisa la Yesu Kristo. David L. Buckner“Ninyi ni Marafiki Zangu”Mzee Buckner anafundisha kwamba tunapaswa kuacha kutafuta sababu za kugawanyika bali kutafuta fursa za “kuwa wamoja.” D. Martin GouryTakasikaMzee Goury anafundisha kwamba toba ya kila siku hutusaidia kuwa wasikivu na tayari kwa mwongozo wa Bwana na ushawishi wa Roho Mtakatifu. Aroldo B. CavalcanteUpepo Haukuacha Kamwe KuvumaMzee Cavalcante anafundisha kwamba Mungu anaweza kutuidhinisha katika majaribu yetu na kwamba tunaweza kusaidiana katika safari yetu ya kiroho pia. Ulisses SoaresKufungamanisha Mapenzi Yetu na YakeMzee Soares anafundisha kwamba mtihani mkuu kabisa wa uanafunzi wetu unapatikana katika utayari wetu wa kuachana na uzamani wetu wenyewe na kusalimisha roho yetu na nafsi yetu yote kwa Mungu ili kwamba mapenzi Yake yawe mapenzi yetu. Kikao cha Jumamosi Jioni Kikao cha Jumamosi JioniKikao cha Jumamosi Jioni cha Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa 194 wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kinachofanyika Oktoba 5–6, 2024. Gerrit W. GongUtakatifu kwa Bwana katika Maisha ya Kila SikuMzee Gong anatualika kufanya takatifu sehemu ya maisha yetu ya kila siku, ambayo itatusogeza karibu zaidi na Bwana na kila mmoja. Kristin M. YeeShangwe ya Ukombozi WetuDada Yee anafundisha kwamba kupitia uhusiano wetu wa agano na Mungu, tunaweza kufikia nguvu za utakaso, uponyaji, na za ukombozi za Yesu Kristo. Kyle S. McKayMwanamume Aliyenena na YehovaMzee McKay anatoa ushahidi wake juu ya maisha na urithi mkubwa wa Nabii Joseph Smith. Jorge M. AlvaradoKumbatia Zawadi ya Bwana ya TobaMzee Alvarado anafundisha kuhusu toba na anashuhudia juu ya uponyaji unaopatikana kwa wote kupitia nguvu zenye kukombozi za Yesu Kristo. David A. BednarKatika Kipindi Kisicho cha Miaka MingiMzee Bednar anatumia mifano ya Wanefi na Walamani katika Kitabu cha Mormoni kuonya dhidi ya kuruhusu kiburi kitugeuze kwenda mbali na Bwana. Kikao cha Jumapili Asubuhi Kikao cha Jumapili AsubuhiKikao cha Jumapili Asubuhi cha Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa 194 wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kinachofanyika Oktoba 5–6, 2024. Jeffrey R. Holland“Ni Mimi”Rais Holland anafundisha kuhusu utiifu kamili wa Kristo kwa Baba Yake na upendo Wake mkuu kwa kila mmoja wetu. Tracy Y. BrowningKutafuta Majibu ya Maswali ya KirohoDada Browning anafundisha kwamba Mungu anaweza kutusaidia tukue kiroho kadiri tunavyouliza maswali ya dhati, kutii amri Zake, na kuweka tumaini letu Kwake. Brook P. HalesMaisha ya Duniani Yanafanya Kazi!Mzee Hales anafundisha kwamba kwa sababu ya injili ya Yesu Kristo na mpango wa wokovu, maisha ya duniani yanafanya kazi! L. Todd BudgeMtafute kwa Moyo Wako WoteAskofu Budge anazungumza kuhusu umuhimu wa muda mtulivu wa kuabudu na kuwasiliana na Mungu. Gary E. StevensonSiku Ambazo Kamwe HazitasahaulikaMzee Stevenson anatazamia miaka 10 inayokuja kama fursa ambayo haijapata kuonekana ya kushiriki habari njema za injili ya Yesu Kristo kwa ulimwengu. Bradley R. WilcoxEe Vijana wa Haki Tukufu ya UzaliwaAkiongea na vijana, Kaka Wilcox anazungumzia swali, Kwa nini Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaishi tofauti sana na wengine? Henry B. EyringRahisi Ni Mafundisho ya Yesu KristoRais Eyring anatuhimiza kufundisha injili ya kweli ya Yesu Kristo kwa urahisi. Kisha wapendwa wetu watakumbuka majaribu yanapokuja, na sisi tutabarikiwa. Kikao cha Jumapili Mchana Kikao cha Jumapili MchanaKikao cha Jumapili Mchana cha Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa 194 wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kinachofanyika Oktoba 5–6, 2024. Dieter F. UchtdorfLisha Mizizi na Matawi YatakuaMzee Uchtdorf anafundisha kwamba matawi ya ushuhuda wetu yanakua tunaporutubisha mizizi: imani kwa Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo. Takashi WadaManeno ya Kristo na Roho Mtakatifu Vitatuongoza kwenye UkweliMzee Wada anafundisha jinsi kusherekea maneno ya Kristo na kumsikiliza Roho kutatuaongoza sisi hadi uzima wa milele. Ronald A. Rasband“Tazama Mimi ni Mwangaza Ambao Mtainua Juu”Mzee Rasband anafundisha kuhusu kumkubali nabii aliye hai kwa kufuata mafundisho yake na mfano wake. Quentin L. CookMaandiko Matakatifu—Msingi wa ImaniMzee Cook anafundisha kuhusu umuhimu wa maandiko, hususani Kitabu cha Mormoni, katika uongofu endelevu. Rubén V. AlliaudWana na Mabinti wa MunguMzee Alliaud anafundisha kwamba sisi sote tu watoto wa Mungu. I. Raymond EgboFokasi kwa Yesu Kristo na injili YakeMzee Egbo anafundisha kwamba tunapofokasi kwa Yesu Kristo na injili Yake, tunaweza kuhisi shangwe hata wakati wa majaribu na changamoto. Russell M. NelsonBwana Yesu Kristo Atakuja TenaRais Nelson anafundisha kwamba sasa ndiyo wakati wa kumfanya Yesu Kristo kuwa msingi wa maisha yetu na kujiandaa kwa ajili ya Ujio Wake wa Pili.