Kanuni za Kuhudumu, Februari 2019
Kukuza Huruma ili Kuhudumu
Kuhudumu ni kuinua. Tunaweza kuwainua wengine tunapojaribu kuelewa kile wanachopitia na kuonyesha kuwa tuna hiari kutembea nao kwa yale wanayoyapitia.
Kwa kuwa Baba Yetu wa Mbinguni anatutaka kuwa kama alivyo, changamoto tunazokumbana nazo katika maisha haya zinaweza kuwa nafasi za kujifunza tunapomwamini na kukaa kwenye mapito. Ijapokuwa, kukaa kwenye mapito kunaweza kuwa kugumu hasa tunapohisi kuwa tunakumbana na majaribu haya peke yetu.
Lakini kamwe hatukukusudiwa kutembea kwenye mapito peke yetu. Mwokozi alitimiza kwa ajili yetu huruma kamilifu akishuka chini ya vitu vyote ili aweze kutusaidia katika mateso na maradhi yetu (ona Alma 7:11–12; Mafundisho na Maagano 122:8). Anamtarajia kila mmoja wetu kufuata mfano wake na pia kuonyesha huruma. Kila mshiriki wa Kanisa ameweka agano “kuomboleza na wale wanaoomboleza na kuwafariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa” (Mosia 18:9). Licha ya changamoto zetu wenyewe tunafundishwa kote katika maandiko kugeuka nje na “kuinua mikono inayolegea na [kuimarisha] magoti yaliyo dhaifu” na “Kunyoosha mapito ya miguu yenu ili yule aliyelemaa asije akaondolewa mapitoni” Waebrania 12:12–13; ona pia Isaya 35:3–4; Mafundisho na Maagano 81:5–6).
Tunapowashika wengine mkono, acha watuegemee, na kutembea nao, tunawasaidia kukaa kwenye mapito kwa muda mrefu wa kutosha kwa Mwokozi sio tuu aweze kuwaongoa—mojawapo ya makusudi muhimu ya kuhudumu—bali pia kuwaponya (ona Mafundisho na Maagano 112:13).
Huruma ni nini?
Huruma ni kuelewa hisia, mawazo, na hali ya mtu mwingine kutoka kwenye mtazamo wao kuliko ule wa wetu1
Kuwa na huruma ni muhimu katika juhudi zetu za kuwahudumia wengine na kutimiza kusudi letu katika kuwahudumia akina kaka na akina dada. Hutuwezesha kujiweka wenyewe ndani ya viatu vya mtu mwingine.
Kutembea ndani ya Viatu Vya Mtu Mwingine
Hadithi inasimulia kuhusu mwanaume Mtakatifu wa Siku za Mwisho aliyekuwa na soni ambaye kila mara alikaa peke yake kwenye safu ya mwisho ya jumba la ibada. Wakati mshiriki wa akidi ya wazee alipofariki ghafla, Askofu aliwapa baraka za ukuhani kuwafariji wanafamilia wa mzee. Akina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama walileta chakula. Marafiki na majirani wa heri njema walitembelea familia na kusema “tujulishe kama kuna kitu chochote tunachoweza kufanya ili kusaidia”
Lakini huyu mtu aliyekuwa mwenye soni alipoitembelea familia baadaye siku hiyo, alipiga kengele mlangoni na wakati mjane alipojibu, alisema tu “nimekuja kusafisha viatu vyako.” Kwa masaa kadhaa, viatu vya familia vilikuwa safi na viling’aa kwa matayarisho ya mazishi. Jumapili iliyofuata familia ya mzee aliyefariki ilikaa karibu na yule mtu mwenye soni kwenye safu ya nyuma.
Hapa kulikuwa na mtu aliyeweza kutimiza haja iliyokuwa haijatimizwa Wao pamoja naye walibarikiwa na kuhudumu kwake kulikoongozwa na huruma.
“Nawezaje kuikuza Huruma?”
Wengine wanaonekana kuwa wamebarikiwa na karama ya kuweza kuwa na huruma. Lakini kwa wale wanaofanya juhudi, kuna habari njema. Kwa muda wa miaka 30 iliyopita, idadi kubwa ya watafiti wamechunguza huruma. Ingawa wengine wanakumbana na mada hii kwa njia tofauti, wengi wao wanakubaliana kwamba huruma ni kitu ambacho unaweza kujifunza.2
Tunaweza kuomba kwa ajili ya karama ya huruma. Ili kuiboresha, inasaidia pia kuwa na uelewa muafaka wa jinsi huruma inavyofanya kazi. Mapendekezo yafuatayo yamekubalika kwa jumla kama vipengele vya kimsingi vya huruma.3 Huku haya hufanyika kila mara bila sisi kufikiria kuwa yanafanyika, kuwa na ufahamu nayo kunatupa nafasi ya kuona fursa ya kuboresha.
1.Elewa
Huruma huhitaji uelewa wa hali ya mwingine. Tunapoelewa vizuri hali zao, ndivyo inavyokuwa rahisi kuelewa jinsi wanavyohisi na kile tunachoweza kufanya ili kusaidia.
Kusikiliza kwa uaminifu, kuuliza maswali, na kushauriana nao na wengine ni matendo muhimu ya kuelewa hali zao. Jifunze zaidi kuhusu dhana hizi kwenye makala yaliyopita ya Kanuni za Kuhudumu:
-
“Mambo Matano Wasikilizaji Wazuri Hufanya, ” Liahona, Juni 2018, 6.
-
“Shauriana kuhusu Mahitaji Yao,” Liahona, Sept. 2018, 6.
-
“Wahusishe Wengine katika Kuhudumu—Kama Inavyohitajika,” Liahona,Okt. 2018, 6.
Tunapotafuta kuelewa ni lazima tuchukue muda kuelewa hali zao maalum badala ya kudhania kwa mujibu wa mwingine ambaye aliyekuwa na hali kama hiyo. Vinginevyo, tunaweza kukosa alama na kuwaacha wakihisi kutoeleweka.
2.Fikiria
Katika juhudi zetu za kuweka maagano kuomboleza na wanaoomboleza na kuwafariji wale wanaohitaji faraja, tunaweza kuomba kwa Roho Mtakatifu kutusaidia tuelewe kile mwingine anaweza kuwa anahisi na jinsi tunavyoweza kusaidia.4
Mara tunapoelewa hali ya mtu, kila mmoja wetu—ikiwa inafanyika kimaumbile au la—tunaweza kupitia tendo la kufikiria kile tungefikiri au kuhisi katika hali hiyo. Kuelewa mawazo hayo na hisia kubwa, pamoja na uongozi wa Roho Mtakatifu kunaweza kusaidia kuongoza majibu yetu kwa hali yao.
Tunapokuja kuelewa hali na kufikiria jinsi wanavyoweza kuhisi, ni muhimu kuwa tusiwahukumu isivyopofaa (ona Mathayo 7:1). Kuwa wakosoaji ya jinsi mtu alivyoingia kwenye hali hiyo kunaweza kutuongoza kupuuza uchungu ambao hali hiyo inasababisha.
3.Mjibizo
Jinsi tunavyojibu ni muhimu kwa sababu hivyo ndivyo huruma wetu unavyoonekana. Kuna njia nyingi za kuwasiliana uelewa wetu kwa maneno au bila maneno. Ni muhimu kukumbuka kwamba kusudi letu si hasa kutatua tatizo. Mara nyingi kusudi ni kuinua na kuimarisha kwa kuwafanya wajue kuwa hawako peke yao. Hii inaweza kumaanisha kusema, “Nina furaha sana umeniambia” au “Pole. Hiyo lazima inaumiza.”
Kwa kila hali mjibizo wetu lazima uwe halisi. Na wakati unaofaa, kuwa katika hali isio ya usalama kuacha wengine kuona udhaifu wako na kutokuwa salama kunaweza kujenga hisia ya muungano.
Mwaliko wa Kutenda
Unapofikiria hali za wale unaowahudumia, fikiria kuwa katika hali zao na kile ambacho ungeona kuwa chenye msaada zaidi, kama ungekuwa kwenye viatu vyao. Omba ili kuelewa jinsi wanavyohisi na kufuatilia. Mjibizo wako unaweza kuwa rahisi, bali utakuwa wa maana.
© 2019 na Intellectual Reserve, Inc. All rights reserved. Imepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/18. Idhini ya kutafsiri: 6/18. Tafsiri ya Ministering Principles, February 2019. Swahili. 15763 743