2020
Kuhudumu kupitia Historia ya Familia
Februari 2020


Kanuni za Kuhudumu, Februari 2020

Kuhudumu kupitia Historia ya Familia

ministering

Mchoro na Joshua Dennis; picha ya nyuma na picha kutoka Getty Images

Kusaidia mtu kwa historia ya familia yao ni njia yenye nguvu katika kuhudumia. Unapowaunganisha wengine na babu zao kupitia hadithi za familia na maelezo, unaishia kujaza mapengo kwenye mioyo yao ambayo wakati mwingine hawakujua kuwa walikuwa nayo (Ona Malaki 4:5–6)

Iwe ni muumini wa Kanisa wa muda mrefu au mtu ambaye hajawahi kusikia juu ya injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo, watoto wote wa Mungu wana hamu ya kujua juu ya walikotokea.

Mara nyingi haichukui muda mrefu kuacha hisia za kina na za kudumu, kama inavyoonyeshwa kwenye hadithi zifuatazo.

Kuipata Familia umbali wa Futi 30,000

Hivi karibuni nikiwa kwenye ndege kurudi nyumbani, nilijikuta karibu na Steve, ambaye alishiriki nami sehemu binafsi za hadithi yake. Alikuwa amehitimu kutoka shule ya upili, akajiunga na Jeshi la Marekani kama mtaalamu wa mawasiliano akiwa na umri wa miaka 18, na punde alianza kufanya kazi katika White House, akitoa msaada wa mawasiliano kwa Rais wa Marekani. Kuanzia umri wa miaka 18 hadi 26, alihudumia Marais wawili wa Marekani. Hadithi zake zilikuwa za kusisimua!

“Steve,” nikasema, “lazima uandike hadithi hizi kwa ajili ya kizazi chako! Wanahitaji kuwa na hadithi hizi kwa mtazamo wako mwenyewe.” Alikubali.

Kisha Roho alinisukuma kumuuliza anajua nini juu ya mababu zake. Steve alijua mengi juu ya upande wa mama yake, pamoja na hadithi ya jinsi familia yake ilivyokula chakula cha jioni na Abraham Lincoln wakati alikuwa akifanya kampeni maeneo ya vijijini wakati wa uchaguzi wa rais wa mwaka 1860 wa Marekani.

Alijua kidogo sana kuhusu upande wa baba yake. Kwa kweli alitaka kujua zaidi. Nilitoa simu yangu na kufungua programu ya Familysearch “Steve, tunaweza kupata familia yako hivi sasa!”

Niliunganishwa na Wi-Fi ya ndani ya ndege. Niliweka simu yangu kwenye meza mbele yangu ili sote wawili tuone. Tulitafuta FamilyTree. Ndani ya dakika chache sote tulikuwa tukitazama cheti cha ndoa cha babu yake na bibi yake.

“Ndio hao!” Alisema. “Nakumbuka jina lake la mwisho sasa!”

Roho ya furaha ilimiminika kwetu sote. Tulifanya kazi ya kuunda maelezo mafupi kwa mababu zake wasiojulikana kwa dakika 45 zilizofuata. Aliniomba nimuahidi kwamba tutaendelea kutafuta pamoja huko Colorado. Tulibadilishana mawasiliano wakati ndege ilipokuwa inatua.

Hapa tulikuwa, tukiruka angani futi 30,000, (mita 9,145) na kifaa kidogo kama mkono wangu, tukitafuta mwanamume na mwanamke waliofunga ndoa miaka 100 iliyopita ambao walikuwa wamepotea kwake na kwa familia yake. Ajabu! Lakini tuliwapata. Familia ziliunganishwa. Hadithi zilikumbukwa. Hisia za shukrani zilihisiwa kwa ajili ya teknolojia na vifaa. Haikuwa chochote ila muujiza.

Jonathan Petty, Colorado, USA

Kuzungukwa na Familia Mpya

Maria alikuwa hashiriki kikamilifu kwa zaidi ya miaka 20. Miezi michache iliyopita, tulitumia nae masaa kadhaa nyumbani kwetu, tukitafiti familia yake kupitia sensa na rekodi zingine. Wakati mmoja alitokwa na machozi akisema, “Nimejifunza mengi juu ya familia yangu katika masaa mawili kuliko nilivyojua katika maisha yangu yote!”

Mwisho wa wakati wetu pamoja, tulimtambulisha kwenye makala ya Jamaa Wanaonizunguka kutoka sehemu ya programu ya FamilyTree. Ilibainika kuwa mimi na mume wangu tuna uhusiano wa karibu sana na Maria. Alitokwa na machozi tena, akisema alikuwa anafikiria yuko peke yake. Hakuwahi kujua kuwa alikuwa na familia katika eneo hilo. Wiki chache baadae Maria alikutana na Askofu wetu. Kwa sasa anafanya kazi ya kujiandaa kwa ajili ya kwenda hekaluni, na amekutana na binamu zake “wapya” kwenye kata yetu!

Carol Riner Everett, North Carolina, USA

Kiambata cha Kuhudumia

Mimi na Ashley, dada ambaye ninamhudumia, tuna vitabu vya upishi kutoka kwa bibi zetu. Chake ni kutoka kwa bibi yake mkuu, na changu ni kitabu nilichokiweka pamoja wakati niliporithi sanduku la mapishi la bibi yangu Greenwood baada ya kufariki kwake.

Mimi na Ashley tulichagua kiambata upishi kutoka kwenye vitabu vya mapishi, na tukakutana baada ya kufanya kazi usiku mmoja ili kuvijaribu. Alichagua mapishi ya kitindamlo, kwa hivyo tulitengeneza kwanza na kuweka katika oveni. Nilichagua viazi vya kukaanga vikavu—chakula kikuu katika kila sherehe ya familia ya Greenwood. Binti wa Ashley Alice alitusaidia kuonja na kutathmini chakula. Kisha, kwa sababu Ashley hakutaka watoto wake kula kitindamlo chote, aligawa sehemu yake kwa akina dada ambao anawahudumia.

Jambo ambalo nilipenda zaidi juu ya usiku wa mapishi yetu ni kwamba wakati tunapika na kuoka, tulizungumza juu ya mada zote za kawaida za kuhudumia—changamoto zake na za kwangu. Lakini pia tulizungumza juu ya bibi zetu na mama zetu, ambayo ilikuwa ya kulainisha moyo kwetu sote.

Jenifer Greenwood, Utah, USA

Njia Maalum za Kusaidia

Historia ya familia inaweza kufungua milango ya fursa za kuhudumia wakati inapoonekana kama hakuna kitu kingine cha kuweza kufanya hivyo. Hapa kuna maoni machache ambayo unaweza kujaribu.

  • Wasaidie kurekodi na kupakia rekodi za sauti za hadithi za historia ya familia, hasa zile zinazofanana na picha.

  • Unda chati ya duara au nyaraka zingine za historia ya familia ambazo unaweza kutoa kama zawadi.

  • Fundisha njia za kupata historia yao wenyewe kupitia kuandika shajara kwa njia wanayoifurahia. Shajara ya sauti? Shajara ya picha? Faili za video? Kuna chaguzi nyingi kwa wale ambao hawapendelei mfumo wa kawaida wa shajara.

  • Nendeni hekaluni pamoja kufanya ibada kwa ajili ya mababu. Au jitolee kufanya ibada kwa niaba ya majina ya familia zao ikiwa wana zaidi ya wanavyoweza kushughulikia.

  • Kutaneni pamoja kushiriki tamaduni za familia.

  • Hudhurieni darasa la historia ya familia pamoja.