“Kupata Faraja katika Yesu Kristo,” Liahona, Septemba 2024.
Karibu kwenye Toleo Hili
Kupata Faraja katika Yesu Kristo
Mwezi huu katika kujifunza kwetu Njoo, Unifuate , tunasoma kuhusu tukio maalum na la kipekee: Kristo mfufuka akitembelea mabara ya Amerika na kuwaalika Wanefi “inukeni na mje kwangu, ili msukume mikono yenu na muitie kwenye ubavu wangu, na pia kwamba mguse alama za misumari katika mikono yangu na katika miguu yangu, ili mjue mimi ni Mungu wa Israeli, na Mungu wa ulimwengu wote, na nimeuawa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu” (3 Nefi 11:14).
Kama Yeye alivyowafanyia Wanefi, Yesu Kristo anatualika kila mmoja wetu kuja na kuwa na uzoefu binafsi na Yeye na kukuza uhusiano wa agano na Yeye. Ni shukrani iliyoje kwangu kwamba Yeye anatupenda sisi katika njia hii na anatamani kuwa pamoja nasi. Kwa sababu yake Yeye, kamwe hatupo peke yetu. Katika makala yangu, ninaeleza kwamba “tulikusudiwa kuwa na ubia na Bwana katika njia yenye nguvu zaidi kupitia maagano yetu” (ukurasa wa 44). Tunapokuja Kwake kupitia chaguzi zetu za kila siku za kushika maagano matakatifu, tunajenga uhusiano na Yesu Kristo ambao utaleta upendo Wake na faraja katika maisha yetu na maisha ya familia zetu.
Tunakumbushwa juu ya Yesu Kristo kwa kuvaa gamenti ya hekaluni baada ya kuwa tumepokea endaumenti, anaeleza Rais Jeffrey R. Holland katika makala yake “Gamenti ya Ukuhani Mtakatifu” (ukurasa wa 4). Anashiriki ahadi ya Urais wa Kwanza kwamba kushika maagano yetu na kuvaa gamenti kutatupatia ufikiaji mkubwa zaidi kwenye ulinzi na nguvu ya Mwokozi.
Ninashuhudia kwamba Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wanakupenda wewe na kwamba Yesu Kristo alikuja kwa kusudi hili hasa: kutuletea sisi faraja ambayo tunaitafuta. Yesu Kristo ni faraja!
Kwa moyo wa dhati,
Kristin M. Yee
Mshauri wa Pili katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi