“Reykjavík, Islandi,” Liahona, Sept. 2024.
Kanisa Liko Hapa
Reykjavík, Islandi
Wamisionari wa kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho walifika Islandi katika mwaka 1851. Katika karne ya 20, waumini wengi walihamia nchi zingine. Leo, hata hivyo, waumini wa Kanisa katika Islandi wamekuja kutoka nchi mbalimbali, na wengi wa Waislandi wenyeji walirudi kuhubiri injili ya Yesu Kristo na kuwasaidia waongofu wapya kuongoza Kanisa. Ingawa ni wachache kwa idadi, wao ni jamii iliyotangamana sana. Kanisa huko Islandi lina:
-
Waumini 380 (kwa makadirio)
-
Matawi 4 (ikijumuisha moja la Kihispania)
-
Kituo kimoja cha FamilySearch
Jumuiya ya Watakatifu
Waumini katika Islandi wanategemeana. Wakati mume wa Bettina Gudnason alipofariki, yeye alipata faraja katika familia ya Watakatifu waliomzunguka: “Waumini wa Kanisa daima walikuwa karibu nami na pamoja nami. Ninajua katika moyo wangu kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanajua kila kitu ambacho kinatendeka karibu nasi. Wao wanatujua kwa majina.”