Liahona
Miongo ya Huduma ya Kujitolea kwa Dhati: Mafundisho Yaliyochaguliwa kutoka kwa Rais Russell M. Nelson
Septemba 2024


Miongo ya Huduma ya Kujitolea kwa Dhati: Mafundisho Yaliyochaguliwa kutoka kwa Rais Russell M. Nelson, Liahona, Septemba 2024.

Miongo ya Huduma ya Kujitolea kwa Dhati: Mafundisho Yaliyochaguliwa kutoka kwa Rais Russell M. Nelson

Sasa ana umri wa miaka 100, Rais Nelson amehudumu kwa miaka 40 kama Mtume. Yafuatayo ni baadhi ya mafundisho yake tangu wakati wake kama Rais wa Kanisa.

mandhari tofauti kutoka kwenye maisha ya Rais Russell M. Nelson.

Anza Ukiwa na Mwisho Akilini

“Mwisho ambao kila mmoja wetu hujitahidi kuufikia ni kupata endaumenti ya nguvu katika Nyumba ya Bwana, kuunganishwa kama familia, uaminifu katika maagano yaliyofanywa hekaluni ambayo hutufanya tustahili baraka kubwa zaidi ya Mungu—ile ya uzima wa milele. Ibada za hekaluni na maagano unayofanya huko ni muhimu katika kuimarisha maisha yako, ndoa yako na familia yako, na uwezo wako wa kupinga mashambulizi ya adui. Kuabudu kwako hekaluni na huduma yako kule kwa niaba ya mababu zako vitakubariki kwa ongezeko la ufunuo binafsi na amani na vitaimarisha ahadi yako ya kubaki katika njia ya agano.”

Tunaposonga Mbele Pamoja,” Liahona,, Apr. 2018, 7.

Tubu Kila Siku

“Hakuna kinachotoa uhuru zaidi, cha kiungwana zaidi, au cha muhimu zaidi kwa maendeleo yetu binafsi kuliko ilivyo fokasi ya mazoea ya kila siku kwenye toba. Toba siyo tukio; ni mchakato. Ni ufunguo kwenye furaha na amani ya akili. Inapoambatana na imani, toba hufungua ufikiaji wetu kwenye nguvu za Upatanisho za Yesu Kristo.”

Tunaweza Kufanya Vizuri Zaidi na Kuwa Bora Zaidi,” Liahona, Mei 2019, 67.

Fanya na Shika Maagano

“Kila mwanamke na kila mwanamume anayefanya maagano na Mungu na kuyashika maagano hayo, na anayeshiriki kwa kustahili katika ibada za ukuhani, ana ufikiaji wa moja kwa moja kwenye nguvu ya Mungu. Wale ambao wamepokea endaumenti katika nyumba ya Bwana wanapokea kipawa cha nguvu ya ukuhani wa Mungu kwa njia ya agano lao, pamoja na kipawa cha ufahamu wa kujua jinsi ya kuvuta nguvu hiyo.”

Hazina za Kiroho,” Liahona, Nov. 2019, 77.

Msikilize Bwana

“Baba Yetu anajua kwamba pale tunapozingirwa na sintofahamu na woga, kitakachotusaidia hasa ni kumsikiliza Mwana Wake.

“Kwa sababu tunapotafuta kumsikiliza—kumsikiliza kwa dhati—Mwana Wake, tutaongozwa kujua nini cha kufanya katika hali yoyote.”

Msikilize Yeye,” Liahona, Mei 2020, 89.

Chagua Kumwacha Mungu Ashinde

“Pamoja na maana ya Kiebrania ya neno Israeli akilini, tunagundua kwamba kukusanywa kwa Israeli kunachukua maana iliyoongezeka. Bwana anawakusanya wale ambao wako radhi kuacha Mungu ashinde katika maisha yao. Mungu anawakusanya wale ambao watachagua kuacha Mungu awe nguvu ya ushawishi muhimu katika maisha yao.”

Acha Mungu Ashinde,” Liahona, Nov. 2020, 92–95

Ushinde Ulimwengu

“Kuushinda ulimwengu siyo tukio ambalo hutokea katika siku moja au mbili. Inatokea katika maisha yote tunaporudia rudia kuyakumbatia mafundisho ya Kristo. Tunapanda imani katika Yesu Kristo kwa kutubu kila siku na kushika maagano ambayo hutuvisha nguvu. Tunabaki kwenye njia ya agano na tunabarikiwa kwa kuwa na nguvu ya kiroho, ufunuo binafsi, ongezeko la imani, na kuhudumiwa na malaika. Kuishi mafundisho ya Kristo kunaweza kuzalisha mzunguko imara zaidi, ukitengeneza kasi ya kiroho katika maisha yetu.”

Ushinde Ulimwengu na Upate Pumziko,” Liahona, Nov. 2022, 97.

Chagua Kuwa Mpatanishi

“Ubishi humfukuza Roho—kila mara. Ubishi hukuza dhana potofu kwamba mifarakano ni njia ya kutatua tofauti, lakini kamwe siyo. Ubishi ni uchaguzi. Upatanishi ni uchaguzi. Unayo haki ya kujiamulia ya kuchagua ubishi au mapatano. Ninawasihi mchague kuwa wapatanishi, sasa na daima.

Wapatanishi Wanahitajika,” Liahona, Mei 2023, 100).

Fikiria Selestia

“Wakati mnapofanya chaguzi, ninawaalika kuwa na mtazamo mrefu—mtazamo wa umilele. Mwekeni Yesu Kristo kwanza kwa sababu maisha yenu ya milele yanategemea imani yenu Kwake na Upatanisho Wake. Maisha yenu pia yanategemea juu ya utiifu wenu wa sheria Zake. Utiifu huandaa njia kwa ajili ya maisha ya shangwe kwenu leo hii na thawabu kuu ya uzima wa milele kesho.”

Fikiria Selestia!,” Liahona, Nov. 2023, 118.