“Picha ya Kiroho ya Uumbaji,” Liahona, Septemba 2024.
Taswira za Imani
Picha ya Kiroho ya Uumbaji
Upatanisho wa Yesu Kristo ulipata maana ya kina kwangu nilipochonga hadithi ya Ibrahimu na Isaka.
Kuchora na kuchonga ni njia mojawapo ya kuonyesha shukrani zangu kwa uzuri wa hii dunia. Kwangu mimi, sanaa huanza na picha ya kiroho ya uumbaji.
“Mtoto wa Agano”
Wakati rafiki yangu aliposataafu kazi na kujiandaa kuhamia mbali, nilitengeneza sanamu kwa ajili yake iliyoitwa Mtoto wa Agano. Ilikuwa sanamu ya kuchonga ya Ibrahimu amembeba mtoto Isaka. Tangu hapo, nimetengeneza msururu wa sanamu zingine zikimwonyesha Ibrahimu na Isaka. Ni sanamu zangu pendwa na baadhi ya sanamu zangu muhimu sana.
Yenye nguvu zaidi kwangu ni ile ya Ibrahimu akimfundisha mwanawe kutoka kwenye maandiko ya kukunjwa. Ibrahimu anashikilia paja lake na kuangalia juu kwa muonekano wa maumivu kwenye uso wake kwa kupata picha kutoka kwa Bwana kwamba lazima amtoe dhabihu mwanawe wa pekee. Isaka anamkumbatia Ibrahimu lakini hawezi kuelewa kwa nini baba yake hakutaka kumjibu.
Sanamu nyingine iliyo kwenye mchakato inaonyesha wawili hao wakijenga madhabahu. Isaka anauliza dhabihu iko wapi, na Ibrahimu anajibu kwamba Bwana atatoa. Katika sanamu ya awali, Ibrahimu anapatiwa kondoo dume kwenye kichaka na kuambiwa kwamba hahitaji kumtoa dhabihu mwanawe. Ibrahimu anamkumbatia Isaka, akimshikilia kwa nguvu. (Ona Mwanzo 22:1–13.)
Kilicho cha thamani sana kuhusu hadithi hii ni kwamba ni aina, au ishara, ya dhabihu ya Mwana wa Mungu. Baba yetu aliye Mbinguni, ambaye anampenda Mwana Mzaliwa Pekee, pia alichagua kumtoa Yeye dhabihu bali hakumnusuru Yeye dakika ya mwisho. Katika maneno ya Mzee Neal A. Maxwell (1928–2004) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, “Hakukuwa na kondoo dume katika kichaka huko Kalvari wa kumnusuru Yeye, Rafiki huyu wa Ibrahimu na Isaka” (“O, Divine Redeemer,” Ensign, Nov. 1981, 8).
Badala yake, Baba aliruhusu Mwanawe mteule (ona Musa 4:2) kufanya Upatanisho kwa niaba yetu ili kwamba sote tuweze kurudi nyumbani kuishi pamoja Nao tena kama sisi tunatamani na kuishi kwa kustahili baraka hiyo (ona Yohana 3:16–17).
Uzoefu wangu unaniambia kwamba Mungu anahusika katika maisha yetu. Tupo ili kwamba sisi “tupate shangwe” (2 Nefi 2:25), lakini tunapata uzoefu kwa mambo tunayopitia. Hakika kadiri ambavyo mambo mazuri hutokea, kuna, hata hivyo, “upinzani katika vitu vyote” (2 Nefi 2:11). Mungu, hata hivyo, yupo kwa ajili yetu, na tunaweza kushinda chochote tunachopaswa kushinda, bila kujali kile kinachokuja kwetu. Tutaona kwamba sisi tunaweza kushinda majaribio yetu tunapoendelea kujaribu kupenda, kuhudumu, na kuwa wenye hisani zaidi—kama Mwokozi wetu.
Nina shukrani kwa ajili ya injili, familia yangu, na watu wote wazuri katika Kanisa. Popote pale mimi na mke wangu, Kathleen, tulipoenda kwenye misioni kote ulimwenguni, tuliwakuta Watakatifu wanaopendana na kutumikiana, na kutoa dhabihu kwa ajili ya kila mmoja. Baba wa Mbinguni anatupenda, na sisi ni watoto Wake. Hakuna kilicho cha muhimu zaidi kuliko kuwa mwaminifu Kwake na kwa Mwanawe, ambao ni waaminifu sana kwetu sisi.