Liahona
Shukrani kwa ajili ya Nabii
Septemba 2024


“Shukrani kwa ajili ya Nabii,” Liahona, Septemba 2024.

Kwa ajili ya Wazazi

Shukrani kwa ajili ya Nabii

Rais Russell M. Nelson anapeana mkono na mwanamke huko Hawaii

Rais Russell M. Nelson anasalimiana na Watakatifu wa Siku za Mwisho huko Kona, Hawaii, mnamo Mei 16, 2019, wakati wa ziara yake ya huduma huko Pasifiki.

Wapendwa Wazazi,

Mwezi huu Rais Russell M. Nelson anaadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwake Makala katika toleo hili inasisitizia jinsi gani yeye na manabii wengine wanatuelekeza kwa Yesu Kristo.

Njia mojawapo ambayo kupitia hiyo vijana wanaweza kumfuata nabii ni kwa kujibu mwaliko wake wa kuhudhuria seminari kila mara na kusoma maandiko kila siku. Ameahidi baraka za kupendeza kwa wale ambao watafanya hivyo, ikijumuisha kujifunza kupokea ufunuo binafsi, kupata majibu ya maswali magumu ya maisha, na kuja kumjua Mwokozi. Je, watoto wenu vijana wameshasikia mwaliko huu wa kinabii? Tembelea seminary.ChurchofJesusChrist.org ili kupata taarifa zaidi.

Mijadala ya Injili

Kumbuka Maagano Yako

Katika makala ya Rais Jeffrey R. Holland kwenye ukurasa wa 4, tunajifunza jinsi kushika maagano yetu na kuvaa gamenti ya ukuhani mtakatifu baada ya kuwa tumepokea endaumenti kutatupatia ulinzi na kutuweka karibu na Roho. Ungeweza kushiriki na familia yako nukuu kutoka kwenye makala na kuzungumza kuhusu jinsi kuvaa gamenti hii “ni dhihirisho la nje la msimamo wa ndani” Ni madhihirisho gani mengine ya nje tunayofanya ili kuonyesha msimamo wetu wa kuwa wafuasi?

Zishike Amri

Mzee Isaac K. Morrison alimwomba Rais Nelson ujumbe binafsi kwa ajili ya mke wake na watoto wake. Jibu la nabii lilikuwa “Zishikeni Amri.” (Ona ukurasa wa 20.) Ungeweza kuwauliza watoto wako: Ni kwa jinsi gani chaguzi zenu zingekuwa tofauti kama nabii angeketi mezani pamoja nanyi na kuwaombeni mzishike amri?

Mfuate Nabii

Rais Nelson anafikisha umri wa miaka 100 mwezi huu! Rais Dallin H. Oaks anashiriki baadhi ya masomo aliyojifunza kutoka kwa nabii huyu (ona ukurasa wa 12). Je, watoto wako wamejifunza nini kutoka kwa nabii? Je, kumekuwa na mahubiri mahususi au ibada mahususi ambayo imekuwa na maana zaidi kwao? Shirikini mawazo yenu. Mngeweza kutazama ujumbe wa video kutoka kwake.