Liahona
Si Mpweke Tena: Njia 7 za Kuunganika
Septemba 2024


“Si Mpweke Tena: Njia 7 za Kuunganika, Liahona, Septemba 2024.

Kuzeeka kwa Uaminifu

Si Mpweke Tena: Njia 7 za Kuunganika

Upweke ni changamoto ambayo inaweza kushindwa kwa baadhi ya juhudi, nguvu za hisia, na msaada kutoka kwa Mwokozi.

watu wawili wakitembea kwa kukaribiana

Sisi sote tuna uwezekano wa kupatwa na upweke nyakati zingine. Hisia za upweke za mara moja moja zinaweza kuwa ni afya na zenye manufaa, ni ishara ya kibaiolojia kwamba tunahitaji kujenga uhusiano imara. Lakini upweke endelevu mara nyingi ni kikwazo kikubwa kwa furaha.

Mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni hujumuisha kutukusanya katika familia na mikusanyiko. Hii hutusaidia sisi siyo tu katika maendeleo yetu ya milele bali pia katika hitaji letu la ubinadamu la kuwa miongoni mwa wengine, kuhisi kuwa tumejumuishwa, kupokea na kutoa usaidizi wa kihisia. Sayansi inaanza kutambua kuwa muunganiko wa kijamii ni hitaji la kibaiolojia lililounganika na afya yetu na kuendelea kwetu kuishi .

Pia ni hitaji la kiroho. Tunahitajiana kwa ajili ya ustawi wetu wa kiroho na ukuaji wetu. Na mbingu iliyojaa uhusiano wa milele ni wazo la shangwe haswa (ona Mafundisho na Maagano 130:2).

Fikiria mawazo yafuatayo ya kukabiliana na upweke katika maisha yako.

  1. Mtegemee Mwokozi. Baba yako wa Mbinguni na Yesu Kristo wanajua upweke wako na wanataka kukusaidia. Kujua kwamba Mwokozi anafahamu uchungu wa upweke kunaweza kukusaidia kujua kwamba Yeye anaelewa kile unachohisi. Kusogea karibu na Baba wa Mbinguni na Mwokozi kupitia sala, kujifunza maandiko, na kuabudu siku ya Sabato na katika hekalu kutakusaidia wewe kujua hauko peke yako. Kama vile Rais Russell M. Nelson alivyofundisha, “Fokasi ya maisha yetu inapokuwa juu ya … Yesu Kristo na injili Yake, tunaweza kuhisi shangwe bila kujali nini kinatokea—au hakitokei—katika maisha yetu.”

  2. Kuwa rafiki. Upweke unaweza wakati mwingine kutusababishia kutilia shaka kwamba kufanya juhudi kutapunguza maumivu yetu. Fanya tathmini binafsi ili kuona kama unakuwa mwenye kukata tamaa. Wakati ukitafuta urafiki, kumbuka kwamba kuwa rafiki kila mra kunahitajika. Kusema jambo rahisi tu kwa jirani kunaweza kuleta tofauti. Na kutafuta fursa za kubariki maisha ya wengine ambao nao pia wanahangaika kwa upweke kunaweza kuwa msaada wenye nguvu sana kuliko yote.

  3. Jenga kwenye mambo mnayoyapenda nyote. Tafuta watu na makundi ambayo mapendeleo, mitazamo, na viwango vyao ni sawa na vyako. Ungeweza kutafuta (au hata kufikiria kuanzisha) klabu ya vitabu, klabu ya huduma, klabu ya matembezi ya masafa, kundi la kuimba, kundi la jioni ya nyumbani, au kundi la wazazi ambao watoto wao wameshaondoka nyumbani.

  4. Imarisha uhusiano uliyopo. Watu wengi tayari wana uhusiano wa kifamilia, marafiki, majirani, na washiriki wa kata. Kukuza uhusiano uliyopo ni sehemu nzuri ya kuanzia wakati unapokabiliana na upweke. Urafiki huchukua muda kujengwa kiuhalisia, kwa hiyo kuwa na subira unapokuza uhusiano. Kumbuka kwamba ubora wa uhusiano wako ni muhimu sana kuliko idadi ya uhusiano ulio nao.

  5. Tafuta fursa za kuhudumu na kushiriki vipaji vyako na karama za kiroho. Kuna fursa nyingi zisizo na ukomo za kutumikia na kuhudumu Kanisani, katika familia zetu, na katika jumuiya. Wakati tunapohisi juhudi zetu zinakuwa na matokeo chanya kwa wengine, inaweza kuleta hisia ya maana na yenye lengo kwenye maisha yetu. Kuhisi kwamba maisha yetu yana maana kwa wengine ni kizuizi imara kwa upweke.

  6. Panga kwa ajili ya nyakati za changamoto. Sikukuu na tarehe zingine muhimu, kama vile siku ya kumbukizi ya kifo cha mpendwa, inaweza kuwa ngumu. Jaribu kupanga shughuli na marafiki au familia juu ya siku kama hizo ili kuondokana na mawazo ya kutamani miunganiko ambayo ungetaka kuwa nayo.

  7. Shiriki katika kazi ya hekaluni na historia ya familia. Hii ni njia yenye nguvu ya kuhisi faraja na mjumuisho. Mzee Dale G. Renlund wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili aliahidi baraka zisizo na idadi tunazoweza kupokea, ikijumuisha “ongezeko la upendo na shukrani kwa mababu zetu na ndugu walio hai, ili kwamba hatuhisi tena tuko peke yetu.”

Kwa watu wengi, upweke ni changamoto ambayo inaweza kushindwa kwa baadhi ya juhudi, nguvu za hisia, na msaada kutoka kwa Mwokozi.