Liahona
Kujenga Kujitegemea: Mradi wa Moroni wa Kigingi cha Kinshasa
Septemba 2024


Makala

Kujenga Kujitegemea: Mradi wa Moroni wa Kigingi cha Kinshasa

Kigingi cha Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kilianzisha mradi wa Moroni ili kuwasaidia waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kuwa wenye kujitegemea. Programu hii ya majaribio imefokasi kwenye kilimo cha mazao na ufugaji mifugo kisasa kwenye shamba la hekta 10 huko Maluku, kaskazini mashariki mwa Kinshasa.

Waumini wa Kanisa wanashiriki kikamilifu katika mradi kwa kulima mazao kama mananasi, viazi vitamu, pilipili za kawaida, pilipili kali na kufuga mifugo. Mradi pia unatoa ajira kwa wakazi wa eneo husika, hata kama si waumini wa Kanisa.

Baadaye, lengo la mradi huu ni kukuza kujitegemea kifedha kwa kuwafanya waumini kuuza na kununua mazao katika bei nzuri. Sehemu ya faida inagawiwa kwa waumini wenye mahitaji.

Mnamo Aprili 2024, mradi ulifikia kiwango cha juu. Kaka Sylvain Tshibaka, akijulikana kwa mipango yake ya kujitegemea ndani ya Kigingi cha Kinshasa, alianzisha ukaguzi wa uzinduzi wa mavuno pamoja na kaka Jean-Claude Buzangu, Tshimanga Pisthou na Charles Kayembe, ambao ni Meneja Ustawi na Kujitegemea wa eneo la Kinshasa.

Baada ya miezi mingi ya mipango madhubuti, kulima kwa juhudi na kujitoa kwa dhati, mashamba yanaanza kuonyesha ahadi ya kile kijulikanacho kama kesho yenye neema. Kwa ufahari na kujiamini, akina kaka hawa walivuna mavuno ya kwanza ya shamba ya mahindi na pilipili. Wakifanya kazi kwa pamoja, walionyesha mfano wa roho ya umoja na ushirikiano ambayo ndiyo maana ya Mradi wa Moroni na kuonyesha nguvu ya juhudi za pamoja katika kufikia malengo ya pamoja.

Mradi wa Moroni unagharamiwa kifedha na Kitengo cha Kanisa cha Huduma za Ustawi na Kujitegemea. Mradi hutoa mfano wa kushikika wa maono ya kujitegemea yanayohamasishwa na urais wa Eneo la Kati la Afrika.

Mradi wa Moroni unanuia kuifanya jamii kuwa imara na yenye kuungana zaidi. Kwa kufanya kazi kwa pamoja kwenye mradi huu, waumini wa kigingi huimarisha umoja wao na kukuza mshikamano. Pia hutoa fursa kwa waumini kushiriki maarifa na ujuzi, kukuza mazingira ya kujifunza pamoja na kukua kwa pamoja.

Kwa kusisitiza kwenye maendeleo ya rasilimali za ndani na maendeleo endelevu ya kiuchumi, Mradi wa Moroni huchangia kwenye kujitegemea kwa muda mrefu katika eneo la Kinshasa. Kwa kuhimiza kilimo ambacho ni rafiki kwa mazingira na kuwekeza katika elimu ya kifedha na ujasiriamali, kigingi kimedhamiria kujenga kesho ambayo kila mtu atastawi na kuchangia katika ustawi wa jamii zao.