Liahona
Darasa la Kujitegemea na Uwekezaji wa Kanisa Kuonyesha Matokeo ya Haraka
Septemba 2024


Makala

Darasa la Kujitegemea na Uwekezaji wa Kanisa Kuonyesha Matokeo ya Haraka

Mary Deng, mkimbizi kutokea Sudani ya Kusini na mama wa watoto wanne, karibuni watakuwa watano, alijifunza ushonaji kupitia madarasa ya kujitegemea yaliyofanywa mwishoni mwa 2023 na Wilaya ya Eldoret ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Katika kuhitimisha mafunzo, yeye pamoja na washiriki washonaji wengine walipatiwa mashine ya kushona ya kukanyaga kwa mguu ya Butterfly, kitambaa cha kuanzia na nyuzi. Washiriki walihimizwa kuanza na miradi midogo, kama vile mito ya kulalia, ili kujipatia kipato kwa haraka.

Mwanzoni mwa 2024, kupitia jitihada zake za masoko, Mary alialikwa kuwasilisha sare za shule za mfano kwa shule moja huko Sudani Kusini. Aliwasajili washiriki wengine watatu wa darasa la kujitegemea kusaidia katika kazi hiyo. Sare za mfano zilisanifiwa, kushonwa na kusafirishwa mwanzoni mwa Februari.

Takribani siku kumi baada ya kuwasilisha sare za mfano, Mary alijulishwa kwamba ameshinda zabuni. Muda wa kukamilisha sare zote ulikuwa ni wiki mbili tu. Akiwa pamoja na washirika wake watatu, Mary alianza kushona kwa dhati ili akidhi vigezo vya zabuni.

Mary alielezea umuhimu wa changamoto hiyo. “Kuanzisha biashara ni mchakato mgumu sana, lakini kwa subira na uthabiti, inawezekana. Kutangaza kupata wateja imekuwa vigumu sana. Najua Mungu anajibu kila ombi. Bila msaada wa Baba Muweza Yote, nisingeshinda zabuni hii. Imenipatia uzoefu mkubwa sana katika kuwa na subira na tumaini kwa ajili ya kitu kizuri zaidi. Nimefanya majaribio yasiyo na mafanikio ya kupata zabuni kwa ajili ya kushona sare za shule, lakini sikukata tamaa.”

Zabuni niliyoshinda inatosha kugharamia gharama na kulipa washiriki, na pesa inabakia kwa ajili ya kununua vifaa vya ziada. Siyo kiasi kikubwa sana kama ambavyo ingetarajiwa, lakini Mary alituma maombi ya zabuni ili aipate.

Mary ana wasiwasi mwingine katikati ya mradi huu. Mtoto wao wa tano atazaliwa mwanzoni mwa mwezi Aprili na yeye pamoja na familia yake wamekuwa wakisubiri kwa subira kutoka kwenye Mfuko wa Ufadhili wa Kanisa wa Hekaluni ili kusafiri kwenda Accra Ghana kwa ajili ya Kuunganishwa. Wanatarajia kukamilisha kazi yao ya hekaluni kabla ndege hazijazuia kusafiri kwake. Pamoja na kuahirisha mara nyingi hapo kabla, familia ya Deng iliunganishwa mnamo 1Machi 2024. Timu yake ya ushonaji inasaidia wakati yeye hayupo.

Kutokana na hekaheka ya zabuni ya sare za shule na changamoto za safari, Mary alijifungua mtoto wao wa tano, Blessing, majira ya asubuhi sana ya Machi 12, wiki tatu nyuma kabla ya muda halisi wa kujifungua na siku nane tu baada ya kurejea kutoka Accra na Hekaluni. Jina la Blessing ni kwa ajili ya kumkumbuka bibi wa Mary, ambaye alifariki kabla Mary hajagundua kwamba alikuwa na ujauzito wa mtoto wa tano.

Mary anasema alikuwa na furaha sana kuwa sehemu ya programu inayolenga kwa muumini ya kujitegemea. Alisema, “Kujitegemea kumenibariki mimi na familia yangu kwa fursa nyingi na uzoefu ambao umeruhusu tufokasi kwenye injili ya Yesu Kristo. Najua kwamba kipaji hiki, ujuzi na maarifa nilivyopokea kutoka kwenye madarasa ya ushonaji vitabariki maisha ya ndugu zangu, marafiki na wanafamilia mbeleni. Nina shukrani kwa baraka zote ninazopokea kutoka programu ya kujitegemea.”