Liahona
Muhtasari wa Kitabu cha Jumla
Septemba 2024


Muhtasari wa Kitabu cha Jumla

Lengo la Muziki ndani ya Kanisa

Katika ufunuo kwa Nabii Joseph Smith, Bwana alisema, “Nafsi yangu hufurahia katika nyimbo za moyoni; ndiyo, wimbo wa mwenye haki ni sala kwangu Mimi, nayo itajibiwa kwa baraka juu ya vichwa vyao” (Mafundisho na Maagano 25:12). Pia alisema, “Wenye haki … watakuja Sayuni, wakiimba nyimbo za shangwe isiyo na mwisho” (Mafundisho na Maagano 45:71).

Muziki mtakatifu huongeza imani katika Yesu Kristo. Humwalika Roho na hufundisha mafundisho. Pia huleta hisia ya unyenyekevu, huunganisha waumini na hutoa njia ya kumwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Muziki Nyumbani

Kupitia manabii Wake, Bwana amewahimiza watu binafsi na familia kutumia muziki wa kuinua katika maisha yao ya kila siku. Kuimba na kusikiliza muziki mtakatifu kunaweza kumwalika roho wa uzuri na amani. Pia huweza kuongeza upendo na umoja miongoni mwa wanafamilia. Nyimbo za Dini zinaweza kuwasaidia watu wapate ujasiri na wastahimili majaribu.

Rekodi za nyimbo za Kanisa zinapatikana kwenye vyanzo vifuatavyo:

Kanisa hutoa nyenzo kuwawezesha watu binafsi na familia wajifunze ujuzi wa msingi wa muziki. Nyenzo zinapatikana kwenye music.ChurchofJesusChrist.org (ona pia 19.6). Kukuza ujuzi wa muziki huongeza fursa kwa waumini za kutumikia nyumbani na Kanisani.

(Kitabu cha Maelezo ya Jumla 19.1-2)