Liahona
Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kujiandaa Kumpokea Mwokozi?
Septemba 2024


“Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kujiandaa Kumpokea Mwokozi?” Liahona, Septemba 2024.

Njoo, Unifuate

Helamani 10; 3 Nefi

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kujiandaa Kumpokea Mwokozi?

Hapa kuna njia nne ambazo unaweza kumpokea Mwokozi katika maisha yako.

Wanefi walihitaji kujiandaa wenyewe ili kumpokea Mwokozi kimwili katika uwepo wao. Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wao ili kutusaidia sisi tumpokee Mwokozi kiroho katika maisha yetu?

watu wakisoma maandiko

Tafakari Mambo ya Mungu

Wakati huo: Nabii Nefi alipokuwa anahisi “kutupwa chini,” yeye alitafakari “juu ya vitu ambavyo Bwana alikuwa amemwonesha.” (Helamani 10:2–3).

Sasa: Kukumbuka kile ambacho Mungu ametufanyia sisi, katika nyakati zote nzuri na mbaya, kutatupatia nguvu na ujasiri wa kubaki karibu na Yeye na kukabiliana na siku za usoni kwa imani.

Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alipendekeza tutafakari kila siku na kuandika misukumo yetu. Alisema: “Unaweza kusali na kutafakari, ukiuliza maswali: Je, Mungu alituma ujumbe ambao ulikuwa mahususi kwa ajili yangu? Je, niliuona mkono Wake katika maisha yangu au maisha ya watoto wangu?”

Ni kwa jinsi gani umeona upendo, mwongozo wa kiungu, au baraka za Mungu katika maisha yako?

Kujichukulia juu Yako Jina la Kristo

Wakati huo: Mormoni alikuwa jasiri katika kutamka kwamba yeye alikuwa “mwanafunzi wa Yesu Kristo” (3 Nefi 5:13).

Sasa: Mzee Jonathan S. Schmitt wa Sabini amependekeza kwamba tunaweza kufokasi juu ya Yesu Kristo kwa kujichukulia juu yetu majina yake tofauti. Kwa mfano, Yesu ni “yule yule jana, leo, na milele” (1 Nefi 10:18). Mzee Schmitt anapendekeza kwamba tunaweza kujichukulia juu yetu jina hili kwa kuwa thabiti katika kuishi injili.

Ni majina gani mengine au vyeo vya Yesu Kristo unavyoweza kuvifikiria na kuvitumia kwako mwenyewe?

picha ya video ya Biblia ya Mwokozi

Mruhusu Mwokozi Akukusanye Kwake

Wakati huo: Katika 3 Nefi 10:4–6, Yesu Kristo anajifananisha na kuku akiwakusanya vifaranga vyake. Huu ni mfano mzuri kwa sababu Yeye daima anatuita sisi tuje Kwake ili Yeye aweze kutulinda na kutulisha. Lakini sisi lazima tuchague kuja Kwake. Alisema, “Ni mara ngapi ningewakusanya kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake na hamnikubali” (mstari wa 5).

Sasa: Yesu anaendelea kutukusanya sisi leo, lakini inabidi tujiachilie tukusanywe Kwake. Je, wewe unajiruhusu mwenyewe ukusanywe kwa Mwokozi na kupata ulinzi Kwake, au unakataa na kubaki umejihatarisha?

Ni mwaliko gani Mwokozi anautoa kwako, na ni nini unahitaji kufanya ili kukubali?

Tazama kuelekea Mbinguni

Wakati huo: Iliwachukua Wanefi majaribio matatu kuisikia sauti ya Mungu. “Na tena mara ya tatu wakasikia hiyo sauti, na wakafungua masikio yao kuisikiliza; na macho yao yakaelekea kule kulikotokea sauti; na walitazama kwa uthabiti kuelekea mbinguni” (3 Nefi 11:5).

Sasa: Njia mojawapo tunayoweza “kutazama kwa uthabiti kuelekea mbinguni” ni kwa, katika kirai cha Rais Russell M. Nelson, “kufikiria selestia.” Alielezea kwamba kipengele kimoja cha kufikiria selestia ni “kwa kufikiri kiroho.”

Je, unaweza kufanya nini ili kufikiri zaidi kirohoi na “kutazama kwa uthabiti kuelekea mbinguni”?