“Roho Alikamilisha Tofauti,” Liahona, Septemba 2024.
Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho
Roho Alikamilisha Tofauti Ile
Ningeweza kuhisi upendo wa washiriki wa kata walipokuwa wakiimba bila usaidizi wangu.
Tulikuwa tunaishi katika mji mdogo katika Georgia, Marekani, wakati baba yangu alipofariki akiwa tu na umri wa miaka 55. Wengi wa wanafamilia yetu waliishi katika jimbo lingine. Maili 2,000 (kilomita 3200) kati yetu hazijawahi kuonekana kuwa mbali sana kuliko wakati huu.
Mume wangu alikuwa askofu na mimi nilikuwa mpiga kinanda wa kata yetu ndogo. Kwa hisia na msongo wote wa mawazo ya kusaidia katika mipango ya mazishi, nilikuwa ninahisi kuchoka sana Jumapili hiyo wakati ilipofika muda wa wimbo wetu wa kufunga mkutano wa sakramenti: “Mungu Awe Nanyi Daima” (Nyimbo za Dini, na. 82).
Kufikia nusu ya ubeti wa pili, huzuni yangu ilinizidia. Kwa namna fulani nilipiga mpaka mwisho wa ubeti ule, lakini mikono yangu ilikuwa inatetemeka na macho yangu kujawa na machozi kabisa kiasi kwamba ilibidi niache ubeti mzima ukiwa umebakia. Sikuweza kuacha kulia.
Kutulia kidogo kulifuatia wakati mkusanyiko ulipogudua kinanda kimenyamaza. Lakini kisha washiriki wa kata walianza kuimba bila muziki. Uimbaji haukuwa kamili. Tulikuwa wachache, hata hivyo. Lakini Roho alikamilisha tofauti. Kupitia majonzi yangu na aibu, nilihisi upendo wa wengi walipokuwa wanaimba.
Mungu awe nanyi daima; hadi tuonane tena
Nguvu ya upendo Wake;
Imeshinda mambo yote.
Mungu awe nanyi daima; hadi tuonane tena.
Wakati wimbo ulipoisha, kiongozi wa muziki alinishikilia nilipokuwa nikilia wakati wote wa sala ya kufunga. Watu kadhaa kisha walikuja kwenye kinanda na machozi machoni mwao ili kusema jinsi walivyohuzunika kuhusu baba yangu.
Baadaye, nilimwambia kiongozi wa muziki ningependa kupiga kinanda wakati wa mazishi. Ilionekana labda lilikuwa sio wazo zuri baada ya kile kilichokuwa kimetokea, lakini baba yangu angefurahia sana kunisikia nikipiga kinanda. Nilitaka kupiga kwa ajili yake. Nitambua wakati huo ni jinsi gani yeye alikuwa amejisikia kuwa karibu wakati wa wimbo wa kufunga.
Ninashukuru sana kwa ajili ya nyimbo za dini. Ninashuhudia kwamba muziki unaweza kutufundisha na kutufariji katika njia ambazo maneno kila mara hayawezi. Kama vile Urais wa Kwanza ulivyoandika katika dibaji ya kitabu cha nyimbo za dini, “Nyimbo … hufariji wachovu, huwaliwaza wenye kuomboleza, na hututia moyo kuvumilia mpaka mwisho.” Mimi pia nina shukrani kwa ajili upendo wa kata nzuri wakati nilipokuwa mbali sana na familia yangu. Ninajua kwamba mimi na baba yangu hakika tutakutana tena.