“Maswali ya Ziada Yanayoulizwa Mara kwa Mara,” Jan. 2021.
Maswali ya Ziada Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Je, ninaulizaje maswali kuhusu usajili wangu?
Kwa maswali kuhusu usajili wako, tembelea store.ChurchofJesusChrist.org na utafute nambari ya eneo lako chini ya “Wasiliana Nasi.”
Nani anaweza kupokea usajili wa kuchapisha bila malipo?
Urais wa Kwanza umewahimiza viongozi wa kata na matawi kuwasaidia waumini kupata maudhui ya magazeti ya kidijitali au ya kuchapisha kutoka Kanisani kwa njia zifuatazo:
Kutoa magazeti kwa waumini wapya waliobatizwa: Baada ya waumini wapya kubatizwa, wanapaswa kuonyeshwa jinsi ya kupata magazeti ya Kanisa katika programu ya Maktaba ya Injili au mtandaoni. Ikiwa wanapendelea gazeti lililochapishwa, waumini wapya wanaweza kupewa usajili wa mwaka mmoja bila malipo kwa kutumia fedha za tawi husika.
Kutoa magazeti kwa vijana na watoto: Kwa kutumia fedha za tawi husika, usajili unapaswa kupatikana kwa watoto na vijana wote wanaohudhuria kanisa bila mzazi au mlezi.
Je, ninawasilishaje makala, wazo au maoni kwa magazeti?
Ili kuwasilisha makala, wazo au maoni kwa magazeti, tumia viungo vilivyo hapa chini:
Liahona: Wasilisha makala, mawazo na maoni kwenye Liahona mtandaoni.
VW Kila Wiki: Wasilisha makala, mawazo na maoni kwenye VW Kila Wiki mtandaoni.
Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana: Wasilisha makala, mawazo na maoni kwenye Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana mtandaoni au tutumie barua pepe kwenda ftsoy@ChurchofJesusChrist.org.
Rafiki: Wasilisha makala, mawazo, na maoni kwenye Rafiki mtandaoni au tutumie barua pepe kwenda friend@ChurchofJesusChrist.org.
Kwa nini Ensign na New Era yalibadilishwa?
Kwa miaka mingi, Kanisa limechapisha magazeti matatu kwa Kiingereza (Rafiki, New Era, na Ensign), na pia gazeti moja lililotafsiriwa katika lugha zingine (Liahona).
Kuanzia Januari 2021, machapisho haya yalibadilishwa na kuwekwa magazeti matatu ambayo yanawahudumia waumini ulimwenguni kote katika lugha nyingi: Rafiki kwa watoto wenye umri wa miaka 3–11, Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana kwa vijana wenye umri wa miaka 11–18 na Liahona kwa watu wazima.
Magazeti haya ya ulimwengu yatasaidia kushiriki jumbe zenye umoja zaidi kwa makundi mbalimbali ya wasomaji. Kurahisishwa huku pia kutaruhusu Kanisa kutuma maudhui kwenda maeneo tofauti ya ulimwengu mara nyingi zaidi kuliko hapo mwanzo.
Ni kwa jinsi gani naweza kujisajili?
Unaweza kujisajili kwenye store.ChurchofJesusChrist.org, kupitia kituo chako cha usambazaji cha eneo au kwa kuwasiliana na Kitengo cha Huduma cha Ulimwengu. Walio nchini Marekani na Kanada wanaweza kupiga simu kwa 1-800-537-5971.
Ni mara ngapi nitaweza kupata gazeti?
Kuanzia mwezi Januari 2021, magazeti yaliyochapishwa na ya kidijitali yatapatikana kila mwezi katika lugha zifuatazo: Kisebuano, kichina, Kichina kilichorahisishwa, Kidanishi, Kidachi, Kiingereza, Kifinishi, Kifaransa, kijerumani, Kihangari, Kiitaliano, Kijapani, Kikorea, Kinorweyi, Kireno, Kirusi, Kisamoa, Kihispania, Kiswedish, Kitagalog, Kithai, Kitonga na Kiyukrain.
Katika lugha zifuatazo, magazeti ya chapa na magazeti ya dijitali yatapatikana kila miezi miwili (mara sita kwa mwaka): Kialbania, Kiarmenia, Kibislama, Kibulgaria, Kikambodia, Kikroeshia, Kicheki, Kiestonia, Kifiji, Kigiriki, Kiaislandi, Kiindonesia, Kiribati, Kilatvia, Kilithuania, Kimalagasi, Kimarshall, Kimongolia, Kipolandi, Kiromania, Kislovenia, Kiswahili, Kitahiti, na Kivietinamu. Zaidi ya hayo, maudhui yaliyochaguliwa ya gazeti yatapatikana katika lugha hizi kidijitali katika miezi ambayo gazeti la uchapishaji halipo.
Katika lugha zifuatazo, maudhui yaliyochaguliwa ya majarida yatapatikana kidijitali tu kila mwezi: Kiafrikaan, Kiamharic, Kiarabu, Kiburmese, Kichuukese, Kiefik, Kifante, Kigeorgia, Kihaiti, Kihiligaynon, Kihindi, Kihindi (Fiji), Kihmong, Kiigbo, Killokano, Kinyarwanda, Kikosraean, Kilaotia, Kilingala, Kimalay, Kimaltese, Kinepali, Kipalauan, Kipohnpeian, Ki S. Sotho, Kiserbia, Kishona, Kisinhala, Kislovak, Kitamil, Kitelugu, Kitshiluba, Kitswana, Kituruki, Kitwi Kiurdu, Kixhosa, Kiyapese, Kiyoruba, na Kizulu.