Hadithi za Maandiko
Wazoramu


“Wazoramu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Alma 31-35

3:26

Wazoramu

Kukuza imani yao katika Yesu Kristo

Amuleki, Alma, Koriantoni, na Wanefi wengine wanasafiri kwenda kwenye mji

Kundi la watu wa Wanefi walioitwa Wazoramu hawakuwa wakitii amri za Mungu. Hii ilimfanya nabii Alma ahuzunike. Alijua njia bora zaidi ya kuwasaidia ilikuwa ni kuwafundisha neno la Mungu. Alikwenda pamoja na Amuleki na wengine kuwafundisha.

Alma 31:2–11

Alma na Amuleki wanaonekana wenye huzuni, na watu waliovalia mavazi ya gharama kubwa wanawapuuza watu wenye shida

Wazoramu walijua kuhusu Mungu lakini walikuwa wamebadilisha mafundisho Yake. Waliabudu sanamu. Walifikiri kuwa walikuwa bora zaidi kuliko watu wengine. Pia walikuwa wachoyo kwa watu ambao hawakuwa na pesa.

Alma 31:1, 8–12, 24–25; 32:2–3

Wazoramu waliovalia mavazi ya gharama kubwa wanasimama kwenye jukwaa refu katikati ya umati wa watu na kuinua mikono yao kuelekea juu

Wazoramu walikuwa wamejenga mahali pa juu pa kusimama katikati ya makanisa yao. Mmoja baada ya mwingine walisimama juu yake na kuomba. Wangeomba wakitumia maneno yale yale kila mara. Katika sala, walisema Mungu hakuwa na mwili na Yesu Kristo hakuwa halisi. Walisema walikuwa watu pekee ambao Mungu angewaokoa.

Alma 31:12–23

Alma na Amuleki wanazungumza na Wazoramu masikini

Alma aliwapenda Wazoramu na aliwataka wamfuate Mungu na Yesu. Alisali na kumwomba Mungu amsaidie yeye na wengine waliokuja pamoja naye kuwafundisha Wazoramu. Alma na wale waliokuwa naye wote walijazwa na Roho Mtakatifu. Walienda na kufundisha kwa nguvu za Mungu.

Alma 31:24–38; 32:1

Wazoramu wengi masikini wanamsikiliza Alma, Amuleki, na Zeezromu wakifundisha

Baadhi ya Wazoramu walikuwa na huzuni. Hawakuruhusiwa katika makanisa kwa sababu hawakuwa na nguo za gharama kubwa. Walitaka kumwabudu Mungu lakini hawakujua ni kwa jinsi gani wangefanya hivyo kama hawangeweza kwenda makanisani. Walimuuliza Alma kile walichopaswa kufanya. Alma aliwafundisha kwamba Mungu husikia sala zao bila kujali mahali walipo.

Alma 32:2-12; 33:2-11

Alma akiwa na mbegu ndogo na akionyesha ua refu na maridadi kwa mkono wake mwingine

Alma alisema Mungu alitaka watu wawe na imani. Alilinganisha mafundisho ya Mungu na mbegu. Kama watu wangepanda mafundisho ya Mungu katika mioyo yao, mbegu hiyo ingekua na wangejua kwamba mafundisho ya Mungu ni ya kweli. Alisema wanahitaji tu kuwa na hamu ya kuamini kuanza kutumia imani yao.

Alma 32:12–43

Amuleki anazungumza, na karibu naye ni picha ya Yesu Kristo akiwafundisha watu

Amuleki kisha aliwafundisha watu kuhusu mpango wa Mungu kwa ajili ya watoto Wake. Aliwaambia kwamba kupitia kwa Yesu wote wangeweza kusamehewa dhambi zao. Pia aliwafundisha kusali kwa Mungu na kusema kwamba Mungu angewasaidia na kuwalinda.

Alma 34

walinzi wakiwaangalia Wazoramu wengi masikini wakiondoka mjini

Wengi wa Wazoramu ambao walikuwa masikini waliamini kile Alma na Amuleki walichofundisha. Lakini viongozi wa Wazoramu walikasirika. Waliwafukuza nje ya mji wote walioamini.

Alma 35:1–6

Waanti-Nefi-Lehi wanawakaribisha Wazoramu maskini

Walioamini walienda kuishi na Waanti-Nefi-Lehi. Waanti-Nefi-Lehi waliwahudumia, au kuwatumikia, kwa kuwapa chakula, nguo, na nchi.

Alma 35:9