Hadithi za Maandiko
Akina mama wa Jeshi la Vijana


“Akina Mama wa Jeshi la Vijana,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Alma 24; 53; 56–57

2:9

Akina mama wa Jeshi la Vijana

Kuwafundisha watoto kumwamini Mungu

Vijana wa kiume wanasikiliza wakati mama akiwafundisha na msichana mdogo akicheza eneo la karibu

Waanti-Nefi-Lehi walimpenda Bwana na watu wote. Akina mama waliwafundisha watoto wao kwamba daima wangeweza kumtumaini Mungu. Waliwafundisha kutii amri Zake.

Alma 26:31–34; 27:12, 27–30; 56:47–48; 57:21, 26

Helamani na Wanefi wengine wakiangalia mji unaowaka moto

Wanefi na Walamani walikuwa wakipigana kwenye vita kubwa. Wanefi walikuwa wakipigana ili kuwalinda watu wao wenyewe na Waanti-Nefi-Lehi.

Alma 48–52; 53:10–13

Waanti-Nefi-Lehi wanazungumza na Helamani na Mnefi mwingine

Kwa sababu ya dhambi zao za zamani, Waanti-Nefi-Lehi walikuwa wamefanya agano, au ahadi maalum, na Mungu kamwe kutopigana na mtu yeyote. Lakini waliwapenda Wanefi na walitaka kusaidia.

Alma 24:6–19; 53:10–13

Wana wa Anti-Nefi-Lehi wanazungumza wao kwa wao na kuwaangalia wazazi wao wakizungumza na Helamani na Mnefi mwingine

Waanti-Nefi-Lehi walikuwa wanaenda kupigana vitani. Lakini nabii Helamani na viongozi wengine wa Kanisa waliwashawishi kwamba wanapaswa kutunza ahadi yao ya kutopigana. Waanti-Nefi-Lehi walilazimika kuwaangalia marafiki zao wakipitia maumivu mengi na shida, lakini walishika agano lao na Mungu.

Alma 53:13–15

vijana wa kiume wakinyanyua mikono yao, na wazazi wao na Wanefi wakiwasikiliza

Wana wa Anti-Nefi-Lehi hawakuwa wameweka ahadi ambayo wazazi wao waliiweka. Sasa walitoa ahadi yao wenyewe kwamba watapigania uhuru.

Alma 53:16–17

Wana wanapata mikuki kutoka kwa askari Mnefi, na mama zao na baba zao wakisali na kutazama

Walikuwa na ujasiri mkubwa. “Walikuwa wamejifunza kutoka kwa mama zao kwamba kama wasingekuwa na shaka, Mungu angewalinda.

Alma 53:20; 56:47

wana wanavalia vazi la kivita na kuzungumza na mama na baba zao, na Helamani anavaa vazi la kivita na anasimama karibu nao

Wana waliwaamini mama zao. Wana walikuwa waaminifu kwa Mungu na walitii amri Zake. Waliamini kwamba Mungu angewaweka salama. Akina mama walijua kwamba Mungu angewalinda wana wao.

Alma 53:20–21; 56:47–48; 57:20–21, 26